Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi: Nimezuiwa kuingia kwenye kaburi la mume wangu. Nimechoka na sitakubali

Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi: Nimezuiwa kuingia kwenye kaburi la mume wangu. Nimechoka na sitakubali

Kyline kila akiongea anawatumia watoto kama ngao. Anatuaminisha familia inawatenga wote.

Hivi inawezekanaje yeye kama mke halali wa marehemu familia nzima imtenge, iwe karibu na watoto wa mke wa zamani?

Akubali tu kukaa mezani, aachane na mambo ya mahakamani, mbona mali za kugawana ni nyingi kuliko kugombana?

Mtaka yote kwa pupa hukosa yote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaodai mali ni watoto wa Mengi ndugu yangu, sio ndugu!.. Mengi ana watoto 4, watoto wawili wakubwa ni wa mke mkubwa na watoto wawili wadogo ni wa mke mdogo.. Waliokuwa wanasimamia mali za marehemu mfano ITV, Kiwanda cha soda (bonite) nk, ni watoto wakubwa!.. Sasa changamoto inakuja baada ya mengi kufariki wosia umetoka hao watoto wakubwa waliokuwa wanasimamia mali za baba yao hawatakiwi kupewa chochote, mali zote unazozijua za Mengi wamepewa watoto wadogo na mke mdogo wa Mengi, kibaya zaidi wosia unasema hata wakienda mahakamani na kushinda kesi, watalipwa sh 1000... Sasa swali ninalotaka kukuuliza ni hili!.. Wewe ungekuwa miongoni mwa wale watoto wakubwa wa mengi ambao mpaka sasa ndio wanaosimamia sehemu kubwa ya mali ya baba yao ungekubali kuondoka na kwenda kuanza maisha upya huku ukiwa masikini huna chochote.. Kumbuka kuwa hao watoto wakubwa wa Mengi hawana nia ya kuchukua mali yote, wao wanataka mali ya baba yao igawanywe kwa watoto wote yaani wao na wale wadogo.. Hata kaka yake Mengi alihojiwa akasema wao kama ndugu wa damu wa Mengi hawataki mali yoyote ila wanataka na watoto wa mke mkubwa wapewe urithi!.. Tatizo mke mdogo hataki watoto wakubwa wapate chochote isipokuwa wale wadogo wa kwake tu!. Kumbuka watoto wadogo wa Mengi ni wadogo sana (kati ya miaka 6), hiyo inamaanisha mali zoooote za mzee zitakuwa za mke mdogo mpaka watoto wake watakapokuwa!.. Sasa wewe huwezi kujiuliza kama huyu mkr mdogo angekubali hawa watoto wakubwa nao wapate chochote angepata hasara gani?.. Wanawake mnapoolewa pendeni watoto wote wa mme, sio kupenda wa kwako tu!

Sent using Jamii Forums mobile app

Kylin ana Pepo la kupenda kushindana na kua mshindi, alitaka kuwakomesha wale watoto wakubwa kwa Sababu wanajuana kitambo kimtaani mtaani alikua anaenda kuwasujudia enzi hizo kabla hajawa na Mzee Mengi wamsaidie kupiga nyimbo zake sasa ndio anaenda kukosa vyote kwa kushindana kwake ili awe mshindi
 
Tumeruka naye sana Reggae, alikuwa mtu poa sana katika kujimix na watu. Rodney mnaweza kukaa naye ki grocery local Mwenge anajimix vizuri, na kwenye crowd za Masaki anajimix.

Alikuwa si mtu wa kujimwambafy "mimi mtoto wa Mengi", to the contrary alikuwa hataki kujulikana hivyo. Business skills zake tulikuwa tunaona kabisa Mzee Mengi amemuandaa vizuri.

Alisaidia sana muziki wa vijana uthaminiwe upigwe East Africa FM.

Alivyofariki Jay-Moe alimuandikia wimbo mzuri sana "Tutakukumbuka" wa tribute.

Sent using Jamii Forums mobile app

oh, ahsante mkuu kwa taarifa
pia umenijibu swali langu kuhusu huo wimbo, muda mrefu humu niliuliza sikujibiwa ule wimbo aliimbiwa nani
ahsante

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Aliyewahi kuwa Mwanamuziki Nchini na ambaye ni mke wa Marehemu Regnald Mengi, Jacqueline Mengi maarufu kama K-Lyinn amedai kuzuiwa kuingia kwenye kaburi la mumewe, Reginald Mengi

Bila kusema ni nani anaowazungumzia, kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter ameandika “Nimenyamaza kwa mengi sana tu. Mmefikia hatua ya kunizuia mimi na wanangu kuingia kwenye kaburi la mume wangu.”

Ameendela na kuandika “Tunafukuzwa eti mpaka tuombe ruhusa ya kuingia kwenye kaburi la mume na Baba wa watoto wangu. Nimechoka, sitakubali kuendelea kuona wanangu wakisononeka na sitakaa kimya.”

Reginald Mengi ambaye alikuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP alifariki dunia Mei 2, 2019 na kuacha mke (Jacqueline Mengi) na watoto wanne ambao ni Regina, Abdiel, Jayde na Ryan. Watoto hao amezaa na Mercy Mengi pamoja Jackline Mengi

View attachment 1365926

BAADHI YA MAONI YA WADAU:

View attachment 1365927
View attachment 1365928
View attachment 1365929
View attachment 1365930
View attachment 1365931
View attachment 1365932
Mambo ya kifamilia iachiwe familia especially when money is in equation.
 
Mambo yamegoma, kaambiwa kwa mila za kichaga anatakiwa aende kaburini akatambike, wazee wameliona hilo.

Kosa kubwa sana aliofanya huyo ni kuruhusu Dr Mengi azikwe Machame
Wazee wakifanya yao, huyo dada ataishia kupata uchizi
Vitu kama hivi siku hizi havipo. Unakuta wazee wa siku hizi wanatambika wamevaa Kaunda suit na jeans mizimu ipi itakubali upuuzi kama huu? Tambiko ili likubalike na mizimu lazima mlifanye mkiwa uchi. Unafanya Tambiko huku unakula soseji, burger na pizza? Mizimu niyakuheshimiwa bana!
 
Waafrika aloturoga kafa!!
Hivi kuna mtu mwenye uchungu na watoto wa mtu kuliko mama yao mzazi!! Ni wangapi tumeshuhudia baada ya baba kufa na ndugu kung'ang'ania mali watoto walivyobaki wakiteseka!!
Cha ajabu utakuta kuna mwanamke anashadadia Jacky kunyimwa mali as if atapewa yeye hizo mali[emoji57]

Gold digger my foot!!! Kwani Mengi alikuwa mtoto au hakuwa na akili hadi akaamua kumuoa Jacky?
Hivi ni nani anapenda ufukara hapa duniani, au kwakuwa tunapambana na kajamba nani wetu basi ni wivu tu!! Roho za kimasikini zitatumaliza walah!

Hivi mama umejiandaa lakini na mapovu ya ndugu wa Mengi wa mtandaoni?
 
Wanaodai mali ni watoto wa Mengi ndugu yangu, sio ndugu!.. Mengi ana watoto 4, watoto wawili wakubwa ni wa mke mkubwa na watoto wawili wadogo ni wa mke mdogo.. Waliokuwa wanasimamia mali za marehemu mfano ITV, Kiwanda cha soda (bonite) nk, ni watoto wakubwa!.. Sasa changamoto inakuja baada ya mengi kufariki wosia umetoka hao watoto wakubwa waliokuwa wanasimamia mali za baba yao hawatakiwi kupewa chochote, mali zote unazozijua za Mengi wamepewa watoto wadogo na mke mdogo wa Mengi, kibaya zaidi wosia unasema hata wakienda mahakamani na kushinda kesi, watalipwa sh 1000... Sasa swali ninalotaka kukuuliza ni hili!.. Wewe ungekuwa miongoni mwa wale watoto wakubwa wa mengi ambao mpaka sasa ndio wanaosimamia sehemu kubwa ya mali ya baba yao ungekubali kuondoka na kwenda kuanza maisha upya huku ukiwa masikini huna chochote.. Kumbuka kuwa hao watoto wakubwa wa Mengi hawana nia ya kuchukua mali yote, wao wanataka mali ya baba yao igawanywe kwa watoto wote yaani wao na wale wadogo.. Hata kaka yake Mengi alihojiwa akasema wao kama ndugu wa damu wa Mengi hawataki mali yoyote ila wanataka na watoto wa mke mkubwa wapewe urithi!.. Tatizo mke mdogo hataki watoto wakubwa wapate chochote isipokuwa wale wadogo wa kwake tu!. Kumbuka watoto wadogo wa Mengi ni wadogo sana (kati ya miaka 6), hiyo inamaanisha mali zoooote za mzee zitakuwa za mke mdogo mpaka watoto wake watakapokuwa!.. Sasa wewe huwezi kujiuliza kama huyu mkr mdogo angekubali hawa watoto wakubwa nao wapate chochote angepata hasara gani?.. Wanawake mnapoolewa pendeni watoto wote wa mme, sio kupenda wa kwako tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa kama mwenyewe Reginald alitaka hivyo...lazima kuna sababu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gold digger huyu atueleze kwanza vizuri tuelewe mzee Mengi alikufaje? Utata huo bado majibu halafu anatuletea mara mali zinaingiliwa mara kabiri. Mwambieni kuwa binadamu hatuujui mwisho wetu hivyo atulie sindano iingie taratibu. Na bado.
 
Lazaro Nyalandu, dr Janabi ( mume wa Sophia Byanaku) Luka ( mume wa Nancy Sumari)

Wajiandae wajifunze kupitia hili sakata la Mzee Mengi maana hao wote ni Waume za watu na wana watoto wakubwa tu kutoka kwenye ndoa zao za kwanza
Kumbe nyalandu Ana watoto wengine Zaid ya Sarah na Christopher
 
Katika hao wote walio-comment hiyo post ya Jacque
nimeona mtu mmoja ndiye ameandika Jambo la kufikiri kidogo juu ya hili Jambo:

"NI REFLECTION YA ULIVOISHI NAO PINDI MZEE YUPO HAI"

Meaning huenda kwa sababu ya umaarufu, kiburi, majivuno, roho mbaya, n.k
ILA
alisahau usilipe baya kwa baya
bali Baya kwa Jema!
hata wakati huo wangekuwa wanakutenda vibaya wewe ungezidi kutenda wema ipo siku nafsi zao zingewasuta kuwa hapana wanakukosea
nao wangejirudi kwako!

sasa wewe ukaona hiyo ndiyo nafasi ya kuongeza gepu kati yao plus utumie hiyo nafasi kwa manufaa yako binafsi na Leo hii hicho unachokipitia ni matunda ya ulichokipanda!
ulisahau ule msemo kuwa
UTAVUNA ULICHOKIPANDA!

Sent from my iPhone using JamiiForums
Mkuu umenena sawia bila chenga. Keep it up. Chukua 5.
 
Kama uko upande wa Jack that's fine. Kila mtu yuko free kuchagua upande wake. but hey kuna ya kujifunza hapa. Ukikubali kuwa mchepuko au ukabahatika kuolewa na mtu ambae ana familia tayari, ingia kwenye familia huku uki balance mambo,sio kuwa selfish na kuhakikisha attention yote unapata wewe na watoto hawapati attention waliyokua wanapata kutoka kwa baba yao...hii deprivation inabuild up resentiment....na kukuchukia kila uchwao..especially kama ilikua close-knit family,
The best comment ever!! ongeza sauti mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom