Hehehe! Mbona Watanzania mumebabaika hivi, mara nyingi huwa mnasema hamhitaji chochote Kenya, ila ukiangalia takwimu za uhamiaji, mpo mnakuja huku kwa maelfu sio mchezo, hili lisiwababaishe wala kuwapa wasiwasi, ni kauli za mwanasiasa aliyeishiwa sera, hana lolote la maana tangu aingie kwenye uongozi, huyu jamaa sijaona chochote alichokifanya, hapo anajaribu kutafuta pa kutokea.
Raia wa Afrika mashariki wako huku wanajituma kuliko maelezo na tunafaidi sana kiuchumi, rais wetu mwenyewe alishasema mwana Afrika mashariki yeyote ajihisi kama Mkenya, anahitaji tu kitambulisho basi.