Jaguar: Wakenya kuwaondoa kwa kipigo Watanzania, Wachina, Waganda na Wapakistani nchini mwao

Jaguar: Wakenya kuwaondoa kwa kipigo Watanzania, Wachina, Waganda na Wapakistani nchini mwao

Sevenjr

Member
Joined
Aug 3, 2018
Posts
32
Reaction score
127
Mbunge wa Jimbo la Starehe Charles Njagua maarufu kwa jina la kisanii Jaguar amesema hawataki wafanyabiashara kutoka Tanzania na Uganda kwenye jimbo lake na ameahidi waondoke la sivyo atawapiga.
.
"Watanzania na Wachina wanaofanya biashara Kenya, hatuwataki, tunawapa masaa 24 waondoke, wasipoondoka tutawapiga na hatuogopi mtu."
--------------
Wakenya wametoa saa 24 kuhakikisha wafanyabiasha raia wa China, Pakistan,Tanzania na Uganda wameondoka nchini mwao na kuwaachia maeneo yao, la sivyo wageni hao watatembezewa kipigo cha mbwa koko.
 
Aisee
IMG_20190625_062135.jpeg
 
Mpaka wageni wachukua biashara zenu mlikuwa wapi?

Hivi Ulaya na Marekani wakisema foreigners wote watoke, mbona nchi nyingi zitaathirika ki uchumi. Wageni wameona opportunity ambayo haitumiki.

Oman pia wanalalamika biashara zao zimeshikiliwa na Wapakistan pamoja na Wahindi. Hawa watu ni wafanyabiashara kwa asili. Ingawa wana dodge ways of business dealings but they keep things going. Waondoeni muwe kama Uganda baada ya kuwafukuza.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] yaani samaki tu wa china wapogoma Kenyatta alisafiri kwenda kuomba msamaha sasa ndo wawapige[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nchi ishanunuliwa hio
Wakenya wametoa saa 24 kuhakikisha wafanyabiasha raia wa China, Pakistan,Tanzania na Uganda wameondoka nchini mwao na kuwaachia maeneo yao, la sivyo wageni hao watatembezewa kipigo cha mbwa koko.View attachment 1138015
FB_IMG_15473432151437689.jpeg
FB_IMG_15455593019015756%20(1).jpeg

Sent from my SM-N910U using JamiiForums mobile app
 
Ninakumbuka sana hotuba ya baba wa Taifa la Tanzania, Mwl. Julius Nyerere kuhusu Ubaguzi, alisema hivi " Ubaguzi ni sawa sawa na kula nyama ya MTU, ukishaanza kubagua huwezi kuacha, mtaendelea". Hiki ndicho kinachotokea kwa Kenya, baada ya kubaguana wenyewe kwa wenyewe kwa misingi ya ukabila na maeneo wanayotoka, sasa wameona ni vyema waelekeze ubaguzi wao kwa mataifa jirani.

Kitu cha kushangaza na kusikitisha ni kwamba, kwa miaka mingi wakenya wamekuwa wakijinasibu kwamba wao hawaogopi ushindani wa biashara, na sio watu wanaolinda ajira zao (Protectionists).

Walianza na kampeni ya "Play Kenyan Music", walipoona imeshindikina, sasa wanataka kuanzisha fujo na kuwapiga wageni wote wanaofanya biashara huko kwao, hata kama wanafanya biashara halali.

Swali kwa watanzania wa JF, kwasababu imekua ni tabia ya wakenya kuanzisha fujo Mara kwa Mara kama njia ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo yao badala ya kutumia mfumo wao wa sheria, kama kweli watawadhuru watanzania, waganda, Rwanda au Burundi, tuwachukulie hatua gani?.
 
Hili tatizo sio rahisi kama unavyolisemea hapa....

Unawacheka Wakenya wakati Kariakoo kuna Wachina walishachinjwa sometimes ago...

Issue hapa sio eti tuwafanyie nini au tuwachukulie hatua gani maana ninaona ni solution ya jino kwa jino which is nonsense in a long run!

Nadhani ni suala la kuelimisha wanasiasa na wananchi wetu mpaka waelewe...

Naona ni ignorance on both sides...wananchi bado hawajajua maana ya soko huria na maana ya competition!

Ni elimu tu hapa!

Sio kwamba Tanzania au UG au RW ni bora sana katika kuruhusu biashara huria,nao ni wabovu vilevile...ni kuelimisha EA yote mpaka kila mtu aelewe!
 
Wakenya wametoa saa 24 kuhakikisha wafanyabiasha raia wa China, Pakistan,Tanzania na Uganda wameondoka nchini mwao na kuwaachia maeneo yao, la sivyo wageni hao watatembezewa kipigo cha mbwa koko.View attachment 1138015
Hilo tamko,limetolewa na mbunge wao,na amelitoa kisiasa zaidi.
Watu wenye maisha magumu,siku zote huwa wanatafuta wa kumtwisha lawama kutokana na umaskini wao.
Sasa jiulize,mpakistan,aliyeingia Kenya,na mtaji wake wa mabilioni ya dola,akafungua show room,amesababisha vipi umaskini wa wananchi wa kawaida?hata akiondoka huo umaskini hauishi zaidi utaongezeka maana ajira alizokuwa anatoa,zitasitishwa.
Watakao umia ni wale wageni wanaomiriki biashara ndogo,kama za maduka,
MTz anayemiriki kampuni kama ya IT,tena imeajiri wakenya kibao,unaanzia wapi kumgusa?huyo anaweza kuguswa tu na sera za nchi kama zikibadirika
 
Back
Top Bottom