DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania Mohammed Chande Othman ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani Yaliyotokea Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu(Oktoba 29, 2025) leo Desemba 01, 2025 ameainisha mambo 6 ambayo yatachunguzwa na tume hiyo.
1. Kuchunguza na kubaini chanzo halisi cha matukio wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi
2. Kuchunguza lengo lililokusudiwa na wale ambao tutaona walikuwa wamepanga na kutekeleza vitendo hivyo yaani lengo lao.
3. Kuchunguza na kubainisha madhara yaliyojitokeza ikiwemo vifo majeruhi uharibifu wa mali na madhara ya kiuchumi na kijamii
4. Kuchunguza mazingira na hatua mbalimbali zilizochukuiliwa na serikali na vyombo vyake na mtu yeyote mwingine.
5. Kupendekeza maeneo yanayohitaji kuimarishwa zaidi ili kuongeza uwajibikaji wa viongoz na raia kwenye kulinda amani ya nchi yetu, utawala bora, haki za binadamu, utawala wa sheria hadi kufikia maridhiano ya kitaifa.
6. Kuchunguza jambo lolote ambalo tume itaona ni muhimu na litaendana na majukumu ya tume
Pia Soma: Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi 2025