PostGE2025 Jaji Chande ataja mambo 6 yanayoenda kuchunguzwa na Tume ya uchunguzi

PostGE2025 Jaji Chande ataja mambo 6 yanayoenda kuchunguzwa na Tume ya uchunguzi

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Hili ni jukwaa huru.Watu watapost chochote hata usichokitaka.Kwa ujinga wenu mnajiita wanademokrasia lakini hamtaki watu wawe na mtazamo na hoja tofauti na zenu.Nyie ni madikteta mliokosa madaraka.@Choosen85
Mkuu umeona eeh!
Hawa ni watu wa hovyo Sana eti wanadai demokrasia ila Cha ajabu wenyewe hiyo demokrasia hawana na hawaitekelezi,Kuna kiongozi wao anahamasisha vijana kuwa unfollow wasanii kisa sio upande wao!!

Tujiulize siku wakitawala nchi itakuwaje?
Kwa wale ambao hawapo upande wao so wataishi Kwa mashaka.

Hawa watu wanasambaza chuki na kuzipamdikiza Kwa vijana ambao wanajiita ni kizazi kinachoweza kupambanua mambo ni aibu.

Inalazimishwa kila mtu awe upande wao.
 
Yaani sirikali inatofanyia maigizo as if wameshushwa kutoka sayari ya Mars oct 30 ,yaani hawajui nini kilisababisha maandamano ya Oct 29? Wakuu wa vyombo vya dola na wasaidizi wao hadi ngazi ya nne wapigwe chini.
Mfano tu angalia huko South africa sahv wanavyowabana wakuu wa vyombo vya ulinzi,kutokana na skendo za rushwa nk
Hizi tume za huku hakuna lolote linalofanyika

Ova
 
Mfano tu angalia huko South africa sahv wanavyowabana wakuu wa vyombo vya ulinzi,kutokana na skendo za rushwa nk
Hizi tume za huku hakuna lolote linalofanyika

Ova
Serikali ya SA ipo vizuri sana kihaki ukiacha mambo ya hovyo ya raia wao mmoja mmoja.

Tume za huku ni za kupihga hela tu hamna kitu ,kabla hata hawajaenda wanajua kila kitu maana wao ndiyo waliofanya hayo madudu ,tume zinaenda kupotosha tu uhalisia....Kama Zero Brain Balozi Thabit kombo anakwambia nchi nzima waliokufa ni 10 tu.
 
Hivi viongozi na CCM wanasoma na wanajua yanayoendelea mitandaoni..??Watu wamechafukwa sio mchezo
 
Samia si alikwishawaambia Nini wakachunguze? Au wanakaidi amri ya miri jeshi nkuu?
 
Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania Mohammed Chande Othman ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani Yaliyotokea Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu(Oktoba 29, 2025) leo Desemba 01, 2025 ameainisha mambo 6 ambayo yatachunguzwa na tume hiyo.

1. Kuchunguza na kubaini chanzo halisi cha matukio wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi

2. Kuchunguza lengo lililokusudiwa na wale ambao tutaona walikuwa wamepanga na kutekeleza vitendo hivyo yaani lengo lao.

3. Kuchunguza na kubainisha madhara yaliyojitokeza ikiwemo vifo majeruhi uharibifu wa mali na madhara ya kiuchumi na kijamii

4. Kuchunguza mazingira na hatua mbalimbali zilizochukuiliwa na serikali na vyombo vyake na mtu yeyote mwingine.

5. Kupendekeza maeneo yanayohitaji kuimarishwa zaidi ili kuongeza uwajibikaji wa viongoz na raia kwenye kulinda amani ya nchi yetu, utawala bora, haki za binadamu, utawala wa sheria hadi kufikia maridhiano ya kitaifa.

6. Kuchunguza jambo lolote ambalo tume itaona ni muhimu na litaendana na majukumu ya tume

Pia Soma: Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi 2025
Huu wote ni wendawazinu...wanaweza kumuita nani publicly atoe maelezo na akigoma wana nguvu gani..hawa ni kama mwanasesere wa maonesho
 
Back
Top Bottom