PostGE2025 Jaji Chande: Tume ya Matukio ya Oktoba 29 inajitegemea kwa kila kitu, hatuna dalali

PostGE2025 Jaji Chande: Tume ya Matukio ya Oktoba 29 inajitegemea kwa kila kitu, hatuna dalali

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Mzee kapewa kazi ngumu sana... Bila shaka anatamani iyeyuke.....
 
Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Oktoba 29, Jaji Mohamed Chande Othman, amesema kuwa tume hiyo haiingiliwi katika maamuzi yake wala haina dalali yeyote katika utekelezaji wa shughuli zake, na kuwa tume hiyo ipo huru.

Jaji Chande ameyasema hayo leo, Aprili 08, 2026, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya kuchunguza vurugu za uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025, Jaji Othman Chande, amesema tume hiyo iko huru na haiikingiliwa na mamlaka yoyote, akikanusha madai kuwa muda wa kazi yake umeongezwa ili kuruhusu kuhaririwa kwa ripoti yake.

Tume hiyo iliyoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan Novemba 20, 2025 kuchunguza matukio yaliyojitokeza wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025, ingawa mpaka sasa imeongezewa muda mara mbili
"Tume inajitegemea kwa kila kitu 'hatuna dalali'. Tume yenyewe ndiyo mhariri, na mamlaka iliyotupa jukumu tutakutana nayo wakati wa kukabidhi ripoti ya mwisho.

Kumekuwa na madai kutoka kwa baadhi ya wadau haswa wanaharakati mitandaoni nchini Tanzania wanaoona kwamba kuongezwa kwa muda wa tume hiyo mara mbili kunalenga kutoa nafasi kwa mamlaka fulani 'kuchakachua' yaliyomo kwenye ripoti hiyo.

Hata hivyo, Jaji Chande alieleza kuwa sababu kuu ya kuongeza muda ni kupanuka kwa wigo wa kazi pamoja na ongezeko la ushahidi unaokusanywa.

Awali tume ilipanga kutembelea mikoa sita, lakini baadala yake wamefika mikoa 11 na wilaya 22.
Vilevile tume imepokea ushahidi mwingi kutoka kwa wananchi na wadau mbalimbali, pamoja na ushauri wa kitaalamu ambao unahitaji kuchambuliwa kwa kina kabla ya kukamilisha ripoti

Jaji Chande amewahakikishia watanzania kuwa hawapaswi kuwa na hofu kuhusu uadilifu wa ripoti hiyo, akisisitiza kuwa tume hiyo inafanya kazi kwa uhuru bila shinikizo la nje.

Tume hiyo iliyoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan Novemba 20, 2025 kuchunguza matukio yaliyojitokeza wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025, imeongezewa muda mara mbili.
Tume lazima iwe independent in fact and in appearance!
 
Back
Top Bottom