Tunkamanini
JF-Expert Member
- Jul 18, 2014
- 377
- 93
Kutokana na kujiuzulu kwa aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali Jaji Werema ni wazi sasa nafasi hiyo inabaki wazi.
Kwa walio wadau wa tasnia hii ya sheria nadhani wataungana nami pasina shaka lolote kuwa kutokana na nafasi hiyo kuwa nyeti kwa ustawi wa Taifa lolote lile duniani, inahitaji kushikiliwa na mtu mwenye nidhamu, weredi na mwenye uadilifu wa hali ya juu.
Kwa wasomi na wanataaluma wa sheria nchini wenye sifa hitajika ni adimu sasa kwa taifa letu hili kwa sasa, binafsi namfahamu vyema Mhe. Jaji Feleshi licha ya kufanya nae kazi kwa muda wa miaka michache lakini ni mtu ambaye ukimweka na viongozi waandamizi wenye hadhi yake ni kama mtu aliyeshushwa toka peponi.
Hakuna mtu wa kada yeyote anaeza ongea swala la hongo kwa Mhe. Jaji Feleshi, kwa kipindi chote nlichofanya kazi pale Sukari sijawahi ona mfanyakazi wa kawaida akimtangulia kufika ofisini na alikuwa wa mwisho kutoka ofisini, sikuelewa nia ya Mhe Rais kumtoa kwenye uDPP lakini huenda alikuwa akiandaliwa kushika nyazifa za juu katika muhimili huo muhimu ili kuusuka upya lakini kutokana na ombwe hili katika nafasi ya AG bado sijaona mtu mbadala.