Jaji Eliezer Mbuki Feleshi anafaa kuwa AG

Jaji Eliezer Mbuki Feleshi anafaa kuwa AG

NCH hii bado ina mijitu miPUMBAVU haijawahi kutokea yaani nch hii hakuna watu wengine icpokuwa wale walivurunda sehem moja wanapelekwa sehem nyingine yaani hata hii kumuwaza huyo ndg nikudhihirisha ukiAZI wa mtu

Hakuna mtakatifu ndani ya nchi yetu kwa sasa 'the Country is corrupt', tutalszimika kuwateua wale wale kati ya wachafu sababu hatuna la kufanya. Hakuna atakaeniaminisha kuwa X-DPP ni mtakatifu, kesi ngapi zimepigwa zengwe hatujui zilipoishia hasa za wakubwa na matajiri!?
 
Mwacheni Rais afanyanye kazi yake acheni kumwekea maneno mdomoni anajua kazi yake

Angelifahamu majukumu yake asingepangua baraza lake Mara NNE. Nitafutie Raisi mwingine yeyote yule duniani aliyewahi kupangua japo mara tatu tu. JK anafanya kazi kwa "test and trial".
Ni Rais aliyepewa U Dr. Akashukuru na pia U prof. Nako akajitanabaisha nayo.
Ipo siku wataalam wa Clasification watatupa nomeclature yake, time will tell.!
 
Hebu tuanzie na alipokuwa DPP mazuri yake. "outstanding perfomance" hiyo unayoizungumzia tuiangazie wapi??!!!

Bora hata wewe, angalia takwimu za kesi mfano hata kisutu tu wakati anaingia kulikuwa na kesi ngapi kwa mwaka na mpaka anaondoka kuna kesi ngapi kwa mwaka.

Kumbuka ni Feleshi ndiye aloondoa maaskari polisi kuwa waendesha mashtaka ili kuongeza nguvu katika upelelezi, hili mbeleni litajaonesha tija na ni moja ya mambo ambayo yalifanya kazi ya Feleshi kuwa ngumu maana kitendo hiki hakikuwafurahisha maaskari wengi maana waliona wamenyimwa ulaji na hivyo kumuhujumu mala nyingi katika utafutaji na uwasilishaji wa ushahidi.

Na ili kujilidhisha kwamba aliimudu vyema ofisi, ndio DPP pekee aliyekaa ofisini kwa miaka mingi zaidi katika historia ya Tanzania.
 
Kwahiyo Rais ndiye anayetakiws kuandaa mashitaka siyo? Endelea kushangaa ila hakatizi mtu nyumba ya ufisadi misingi imebomolewa tupo katika mkakati wa kulijenga taifa lenye kujiheshimu na kujisimamia!

Hivi wewe ni binadamu au mashine? Rais anapotoa msamaha kuna mtu anaeweza kuhoji au kupinga? Hiyo katiba ya nyumbani kwako na mmeo aisee.
 
kwani fereshi ni dini gani mkuu kama ni mkristo hawezi kupata.
 
Watu wanashindwa kuelewa kuwa ile ilikuwa ni kampeni tu ya kuitenga PCCB na DPP, huyo Hossea mnaemwamini mmuulize kwa nini aling'ang'ania ushahidi wa UDA ili kuwalinda akina Kisena kitu kilichopelekea Feleshi aiondoe kesi mahakamani.

Sasa kama alisusa wakati aliweza kupeleka hiyo taarifa juu ili huyo aliyebana asukumwe huko duniani kwa manyang'au si ndio atasusa nchi iuzwe mchana kweupe??!!
 
Andrew Chenge, Feleshi na Hosea wote wamekulia kwa Jaji Francis Nyalali!!! I wish Watanzania wangefumbua macho na kuangalia mambo in 3D!!! AG atakaewasaidia Watanzania kwa sasa ni Godwin Ngwilimi ...
 
Sasa kama alisusa wakati aliweza kupeleka hiyo taarifa juu ili huyo aliyebana asukumwe huko duniani kwa manyang'au si ndio atasusa nchi iuzwe mchana kweupe??!!

Mkuu, PCCB ni chombo chunguzi na kiko huru.
 
Bora hata wewe, angalia takwimu za kesi mfano hata kisutu tu wakati anaingia kulikuwa na kesi ngapi kwa mwaka na mpaka anaondoka kuna kesi ngapi kwa mwaka.

Kumbuka ni Feleshi ndiye aloondoa maaskari polisi kuwa waendesha mashtaka ili kuongeza nguvu katika upelelezi, hili mbeleni litajaonesha tija na ni moja ya mambo ambayo yalifanya kazi ya Feleshi kuwa ngumu maana kitendo hiki hakikuwafurahisha maaskari wengi maana waliona wamenyimwa ulaji na hivyo kumuhujumu mala nyingi katika utafutaji na uwasilishaji wa ushahidi.

Na ili kujilidhisha kwamba aliimudu vyema ofisi, ndio DPP pekee aliyekaa ofisini kwa miaka mingi zaidi katika historia ya Tanzania.

Kwa hiyo hizi ndizo sifa zinazomfanya awe mwanashria bora sana kuliko wengine ili akalie hiyo ofisi??!!!
Kama ingekuwa ni interview hiyo nafasi ingebase kwenye historia tu au pamoja na mengine??!!
Kukaa ofisini kwa muda mrefu kwa tulipofikia asee kuna watu wako ofisini yaani hadi wahudumu tu wanshangaa kwanini bado wapo, yaani tangu tunasoma mpaka leo wapo!!!!
 
Wana JF, naomba tujikumbushe majina ya AG (mwanasheria mkuu) waliopita na sehemu walizotoka tuone kama kuna kitu chochote tunaweza kujifunza. Waswahili husema Historia ni mwalimu mzuri.
  1. Judge Joseph Sinde Warioba Mara
  2. Andrew Chenge Simiyu
  3. Mwanyika (???)
  4. Judge Frederick Werema Mara
  5. .........
  6. ..................

Naomba kuwasilisha
 
Huyo unaempendekeza wewe ni mume wako au kakutuma uje kumpigia chapuo humu. Mfyuuuuuuu wewe
 
Huyo mnyaruanda tumpeleka wapi! Keshaharibu toka alipokua DPP

Unamaanisha sio raia? sina hata cha kukujibu, angekuwa ameharibu Rais wala asingesikiliza mapendekezo yake juu ya nani anafaa kuliendeleza gurudumu, huyo ni kijana wake aliyempika akapikika kiuadilifu na kiuchapakazi.
 
hahahaaaaa. wazee wa fununu. wanaosikia wanajhua zaidi ya wanaotenda! ndio nchi yetu. na wewe ni mmoja ya wanaodhihirisha ulemavu wetu
 
Kwanza Feleshi ashitakiwe kwa kupokea rushwa kutoka kwa Iddi Simba na Simon Kisena aliyopokea kwa ajili ya kuondoa kesi ya UDA
 
Hivi wewe ni binadamu au mashine? Rais anapotoa msamaha kuna mtu anaeweza kuhoji au kupinga? Hiyo katiba ya nyumbani kwako na mmeo aisee.

Tunkamanini: Sitaki kuingia kwenye mabishano yako na AME. Lakini kwa faida wa wasomaji naomba kuweka jambo hili sawasawa

Kulingana na katiba yetu RAIS anayo mamlaka ya kumsaheme mtu/mfungwa yeyote aliyeapatikana na kosa mbele ya mahakama wakati wowote na hakuna chombo au mtu yeyote anayeweza kuhoji.

Lakini pia kulingana na katiba yetu, Rais hana mamlaka ya KUMSAMEHE mtuhumiwa yeyote wa makosa anayetarajiwa/aliyefikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Hivyo Rais kuwasamehe wezi wa EPA waliorudisha pesa wizi kwa hiari yao ilikuwa ni kuvunja katiba ya JMT.

Kama Rais alikuwa anawapenda sana hao watuhumiwa EPA, angesubiri kwanza wapatikane na kosa mbele ya mahakama halafu ndio awasamehe, hakuna mtu/chombo chochote kingehoji kwani mamlaka hayo amepewe na katiba ya JMT
 
Back
Top Bottom