Jaji Elinaza Luvanda ajiondoa kuendesha kesi ya Mbowe na wenzake baada ya washtakiwa kudai hawana imani naye

Jaji Elinaza Luvanda ajiondoa kuendesha kesi ya Mbowe na wenzake baada ya washtakiwa kudai hawana imani naye

sio lazima Mawakili waombe, mahakama ipo pale kuhakikisha haki inatendeka kwa pande zote mbili; yaani mtuhumiwa na hata upande wa Jamuhuri, hivyo Jaji yuko sahihi kabisa kutoa maelekezo kwa upande wa Jamuhuri kwenda kurekebisha hati ya mashitaka hata kama wao hawajaomba.

Ondoa umajinuni hapa!! Kesi hii ililetwa na mawakili wa Mbowe wakidai hati ya mashtaka ina kasoro na ifutwe. Ili jaji aone hivo au la akasilikiza hoja za pande zote mbili! Ameamua hati ina kasoro na hivo haki iko upande wa Mbowe kuwa kesi ifutwe!! Mawakili wa serikali walikuwa wakitetea kuwa hati ni sahihi na haina makosa. Si juu ya Jaji kusema irekebishwe hivi ai vile - ni juu ya jamhuri kufungua kesi mpya. Yeyote mwenye akili (sio wewe) hawezi kukubali kuwa mwamuzi neutral anayepaswa kuegamia upande mmoja kwa haki sasa anataka kuegamia na upande mwingine ili mradi tu kesi iendelee!! Mwenye jukumu la kuendeleza kesi hii ni jamhuri!! Sio jaji wala Mbowe!! Mbowe aachiwe na kesi mpya ifunguliwe! Simple!

Unapoona mwamuzi anakunyima haki lakini pia yuko na upande wa pili - una haki ya kulalamika!! Mambo yote haya yana sheria zake.

Cha ajabu ni hiki na kiazi wewe utakuwa hukijui. Kesi hii sasa itakuwa ngumu na mbaya upande wa jamhuri. Kama jaji katoa hukumu kuwa ni batili, basi jamburi inabidi ikate rufaa kwa hati hii hii! Na mawakili wa Mbowe watatoa reference za kesi hii hii kuwa hati ile ile ni batili!! Lakini kwa kuwa ni goroko - huwezi kuona hili!!
 
Mahakama no

Hati ya mashtaka inapokuwa proved ni batili..sheria inasemaje kuhusu shitaka lililoletwa na hati hiyo batili....does the law stipulates that judge awaambie mawakili waibadilishe...au kesi huwa inafutwa na mtuhumiwa kuachiwa?
Hati ya mashtaka ndio batili au mashtaka pia ni batili?
 
Ondoa umajinuni hapa!! Kesi hii ililetwa na mawakili wa Mbowe wakidai hati ya mashtaka ina kasoro na ifutwe. Ili jaji aone hivo au la akasilikiza hoja za pande zote mbili! Ameamua hati ina kasoro na hivo haki iko upande wa Mbowe kuwa kesi ifutwe!! Mawakili wa serikali walikuwa wakitetea kuwa hati ni sahihi na haina makosa. Si juu ya Jaji kusema irekebishwe hivi ai vile - ni juu ya jamhuri kufungua kesi mpya. Yeyote mwenye akili (sio wewe) hawezi kukubali kuwa mwamuzi neutral anayepaswa kuegamia upande mmoja kwa haki sasa anataka kuegamia na upande mwingine ili mradi tu kesi iendelee!! Mwenye jukumu la kuendeleza kesi hii ni jamhuri!! Sio jaji wala Mbowe!! Mbowe aachiwe na kesi mpya ifunguliwe! Simple!

Unapoona mwamuzi anakunyima haki lakini pia yuko na upande wa pili - una haki ya kulalamika!! Mambo yote haya yana sheria zake.

Cha ajabu ni hiki na kiazi wewe utakuwa hukijui. Kesi hii sasa itakuwa ngumu na mbaya upande wa jamhuri. Kama jaji katoa hukumu kuwa ni batili, basi jamburi inabidi ikate rufaa kwa hati hii hii! Na mawakili wa Mbowe watatoa reference za kesi hii hii kuwa hati ile ile ni batili!! Lakini kwa kuwa ni goroko - huwezi kuona hili!!
Umefafanua vyema kabisa.
 
mambo sio mepesi hivi mkuu,
hali ni ngumu sana kwenye ilo swala,
ingekua rahisi, uyo kamanda angeshapigwa namba mda sana..
Basi watueleze hakuna utawala wa sheria nchini tujue wazi...a criminal ni criminal tu haijalishi ni mwanasiasa au kibarua wa shambani.
 
Huyu Mbowe si alisema yeye haogopi gereza? Mtu asiyeogopa gereza hawezi kuhangaika kama anavyohangaika Mwamba, kwanza hakutakiwa hata kuweka mawakili 300 kumtetea! Au kabadili gia angani akiwa huko gerezani! So sad, akitoka sasa asirudi tena TZ, atuachie amani yetu, mtu wao aliyekuwa anawatumia JK hana mamlaka tena kwa sasa.
 
Mawakili wa serikali wao wakiona kuna hati batili kukimbilia kumuomba Jaji alitoe shauri hilo mbele ya Mahakama na kulitupilia mbali. Ila upande wa utetezi ukiwa na hoja nzito kama hiyo upande wa Jamhuri hawataki precedent hiyo itumike.

Turejee mfano wa shauri lingine ambapo upande wa Jamhuri mawakili wake walitaka mheshimiwa Jaji alitupilie mbali pingamizi:

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania​

OFISI YA WAKILI MKUU WA SERIKALI​

Aug, 31 2021

MAHAKAMA YAKUBALI KUSIKILIZA HOJA ZA UTETEZI KATIKA SHAURI LA MBOWE KWA MAANDISHI.​

News Images

Mapingamizi yaliyowasilishwa leo yanalenga kuiomba Mahakama hiyo kuliondoa Shauri hilo Mahakamani kwa kuzingatia kuwa taratibu zilizotumika kufungua na kuwasilisha shauri hilo la kikatiba zilikiuka taratibu za kisheria.
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imekubali maombi ya Mawakili wa Serikali waliyoiomba Mahakama hiyo kusikiliza utetezi wa mapingamizi yaliyowasilishwa mahakamani hapo na upande wa Serikali kwa njia ya maandishi.
Uamuzi huo umefikiwa leo Agosti 30 mbele ya Mahakama hiyo baada ya upande wa Mlalamikaji kushindwa kuwasilisha viapo vya ziada kama walivyotakiwa kuwasilisha viapo hivyo mahakamani hapo tangu tarehe agosti, 2021 na badala yake wameamua kuendelea na viapo vilivyowasilishwa awali.

Akizungumza mbele ya Mahakama hiyo, Wakili wa Serikali Mkuu, Bw. Hangi Chang’a ameiomba Mahakama kuridhia ombi hilo kwa madai kuwa baada ya upande wa mlalamikaji kushindwa kuwasilisha hoja zao za ziada, kama walivyotakiwa na Mahakama hiyo wao walitekeleza wajibu wao wa kisheria kwa kuwasilisha mapingamizi manne kwa lengo la kupinga hoja za upande wa mlalamikaji.
Mapingamizi yaliyowasilishwa leo yanalenga kuiomba Mahakama hiyo kuliondoa Shauri hilo Mahakamani kwa kuzingatia kuwa taratibu zilizotumika kufungua na kuwasilisha shauri hilo la kikatiba zilikiuka taratibu za kisheria.
Mlalamikaji katika shauri hilo analalamikia utaratibu uliotumika kumkamata na kumfikisha Mahakamani katika shauri analotuhumiwa kufadhili vitendo vya kigaidi kuwa ulikiuka na kuvunja haki zake za kikatiba.
Baada ya kusikiliza maelezo kutoka pande zote mbili Jaji anayesikiliza shauri hilo Mhe. John Mgetta ameutaka upande wa serikali kuwasilisha hoja zake kwa maandishi ifikapo tarehe 6 Septemba huku upande wa mlalamikaji ukitakiwa kujibu hoja hizo tarehe 09 Septemba na kama kutakuwa na hoja za kujibu kutoka upande wa serikali basi wawasilishe hoja hizo tarehe 13 Septemba mwaka 2021.
Mhe. Jaji. Mgetta ameahirisha Shauri hilo mpaka tarehe 23 septemba saa 8:00 mchana litakapotajwa tena Mahakamani hapo huku akueleza kuwa hakutakuwa na sababuMhe. Mbowe kuhudhuria Mahakamani hapo na badala yake atawakilishwa na wakili wake.
leo yanalenga kuiomba Mahakama hiyo kuliondoa Shauri hilo Mahakamani kwa kuzingatia kuwa taratibu zilizotumika kufungua na kuwasilisha shauri hilo la kikatiba zilikiuka taratibu za kisheria.

Source : Habari |Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali
 
Ondoa umajinuni hapa!! Kesi hii ililetwa na mawakili wa Mbowe wakidai hati ya mashtaka ina kasoro na ifutwe. Ili jaji aone hivo au la akasilikiza hoja za pande zote mbili! Ameamua hati ina kasoro na hivo haki iko upande wa Mbowe kuwa kesi ifutwe!! Mawakili wa serikali walikuwa wakitetea kuwa hati ni sahihi na haina makosa. Si juu ya Jaji kusema irekebishwe hivi ai vile - ni juu ya jamhuri kufungua kesi mpya. Yeyote mwenye akili (sio wewe) hawezi kukubali kuwa mwamuzi neutral anayepaswa kuegamia upande mmoja kwa haki sasa anataka kuegamia na upande mwingine ili mradi tu kesi iendelee!! Mwenye jukumu la kuendeleza kesi hii ni jamhuri!! Sio jaji wala Mbowe!! Mbowe aachiwe na kesi mpya ifunguliwe! Simple!

Unapoona mwamuzi anakunyima haki lakini pia yuko na upande wa pili - una haki ya kulalamika!! Mambo yote haya yana sheria zake.

Cha ajabu ni hiki na kiazi wewe utakuwa hukijui. Kesi hii sasa itakuwa ngumu na mbaya upande wa jamhuri. Kama jaji katoa hukumu kuwa ni batili, basi jamburi inabidi ikate rufaa kwa hati hii hii! Na mawakili wa Mbowe watatoa reference za kesi hii hii kuwa hati ile ile ni batili!! Lakini kwa kuwa ni goroko - huwezi kuona hili!!
Kisheria siyo kila makosa kwenye hati ya mashtaka yanaletea mashtaka yote kufutwa. Kuna makosa yanarekebishwa na kesi inaendelea. Hata wewe ukijaza sehemu fulani vibaya kwenye form, haimaanishi kwamba jambo hilo sasa lifutwe. Mfano ufutwe chuo, ufutwe kazini, ufutiwe mkopo wa elimu n.k. Haki ni kupima uzito wa makosa. Anayepima uzito huo ni Jaji na siyo mwingine.
 
Baada ya Jaji Luvanda kutupa mapingamizi yote yaliyotolewa na Mawakili wanaomtetea Mbowe na wenzake, Mbowe amesimama na kumtaka Jaji Luvanda ajiondoe kuendesha kesi hiyo kwani ameonyesha upendeleo na taarifa zinasema ana maelekezo ya kupindisha sheria ili amfunge Mbowe na wenzake.

Jaji Luvanda amesema hati ya mashtaka ni batili amewashauri Mawakili wa serikali wakaibadilishe, Mawakili upande wa utetezi wamegoma wamemwambia kama hati ya mashtaka ni batili basi futa kesi Jaji akakataa ila amekubali kujiondoa kuendesha kesi.

UPDATE: Jaji Luvanda akubali
Jaji Elinaza Luvanda aliyekuwa anaisikiliza kesi ya Uhujumu Uchumi nyenye mashtaka 6 yakiwemo ya ugaidi, amejitoa kusikiliza kesi hiyo, sababu ya kujitoa kwake, ni kutokana na mshtakiwa wa nne katika kesi hiyo, Mhe. Freeman Mbowe na wenzake kuwa hawana imani na Jaji huyo.

Pia soma >
Mahakama ya Uhujumu Uchumi: Mvutano mkali kesi ya Mbowe na wenzake. Hatma ya kesi kujulikana Septemba 6
. "Jaji Mwenzangu Luvanda" Machozi ya samaki majini hayatakufikia wewe na kizazi chako mpaka cha nne, tekeleza maagizo
. CHADEMA tusimpe vitisho Jaji Luvanda, mpaka sasa hajapendelea pande yoyote. Kibatala na jopo lake walichemka
Sasa Mbowe ajue jela inamsubiri. Ameharibu serikalini, ameharibu na mahakamani.
 
mkuu hii sio kesi ya wizi wa kuku.
hii ni kesi "sensitive" haiwezi kufutwa kienyeji.
nenda kasome vizuri sheria ya makosa ya Ugaidi.
Jaji yupo kwaajili ya kuhakikisha haki inatendeka pande zote, kwa jinsi alivyo ona kuna dosari kadhaa ktk hati ambazo kimsingi zinaweza kupelekea haki isitendeke hivyo kaelekeza marekebisho yafanyike.
Masilahi ya Jaji ni Haki itendeke sio vinginevyo.

Mpumbavu tena. Kesi ililetwa mahakamani na Mbowe, jamhuri hapa alisema hati ya mashtaka ni sahihi. Kama hati imeonekana ni batili, i akuwa batili in its fullest - sio visehemu!! Usichojua ni kuwa hakima anasema wakatekebishe hati maana yake hiyo hati mpya ndiyo itakayotumika kumshtaki Mbowe na wenzie!! Maana yake ni kuwa kesi hii haiwezi kuendelea kwa hati hii iliyotolewa uamuzi kuwa ni batili!! Mbowe akamatwe upya na kushtakiwa upya! Period.

Najua kinachokuuma ni kuwa Mbowe anaweza kuwa huru kwa jambo hili. Ukweli ni kuwa hawezi kuwa huru - akamatwe na kushtakiwa kwa hati mpya!!

Huko jamhuri ni matumbo kuuma kwa sababu makosa yaliyo kwenye hati hii batili hayawezi kutumika tena kumshtaki Mbowe. Wakati waambiwa makosa yamejirudiarudia walikuwa vichwa ngumu - sasa makosa yote waliyoyarudia hayawezi hata kutumika tena!! Ni vema wakamsingizia jambo lingine ili wamkamata!!

Katika round hii mpokeaji wa haki ni Mbowe!! Ndiye aliyefungua kesi ya kupinga hati ya mashtaka!!
 
Kwa sasa ndicho kinachojiri huko Kesi dhidi ya Mbowe ya Kisiasa. Jaji Luvanda ameamua kuitema ndoano baada ya kugundua hataki laana na mikosi itokanayo na ukiukwaji wa Haki za binadamu wasio na kosa

Amefanya kama alivyofanya Pilato wakati wa Yesu.

Yesu alishtakiqa ktk mahakama ya Kayafa kwa makosa ya kuhubiri uongo na kuleta taharuki kwa watu wa Yerusalem. Pamoja na Kuwa Hakum Pilato akipitia hati ya mashtka na kusikiliza mashahidi wa upande wa mashtaka( jamhuri) akajiridhisha pasipo na shaka kuwa Yesu hana kosa. Hivyo akajitoa kwenye mkenge wa kumhukumu mtu asiye na hatia.

Akanawa Mikono akawalaani wale wanaoendelea na keai yake. Aksasema Fanyeni mnavyooni nyinyi mimi mtu huyu sioni kama ana hatia. Na Damu Yake itakuwa juu yenu na watoto wenu.

Hadi Leo wayahudi hawajapata amani na hawatapata amani hadi Masihi Issa Bin Maryam arudi.

Asalam Aleykum
 
Afadhali jaji kajitoa. Sasa mvua itamyeshea gaidi kihalali kabisa.
Umewahi kusikkia wapi Mahakama Ina rule kuwa hati ya mashtaka Ni defective, alafu eti inaomba walokosea wakarebishe? Hiyo ni Mahakama au Baraza la usuluhishi?

Siku utakapong'olewa pum*b zako, ndio utakapojua Kuna watawala wa hovyo nchi hii!
 
Huyo Jaji anachafua taaluma yake.Kama hati ya mashtaka ni batili, utawapaje nafasi ya kuandaa nyingine kama huna maagizo toka juu?.Unapata wakati mgumu kwa sababu unakubali kutumika
 
Kwa sasa ndicho kinachojiri huko dhidibya kesi ya Mbowe ya Kisiasa. Jaji Kuvanda ameamua kuitema ndoano baada ya kugundua hataki Laana na mikosi itokanayo na ukiukwaji wa Haki za binadamu wasio na kosa

Amefanyankama akigyofanya Pilato wakati wa Yesu.

Yesu alishtakiqa ktk mahakama ya Kayafa kwa makosa ya kuhubiri uongo na kuleta taharuki kwa watu wa Yerusalem. Pamoja na Kuwa Hakum Pilato akipitia hati ya mashtka na kusikiliza mashahidi wa upande wa mashtaka( jamhuri) akajiridhisha pasipo na shaka kuwa Yesu hana kosa. Hivyo akajitoa kwenye mkenge wa kumhukumu mtu asiye na hatia.

Akanawa Mikono akawalaani wale wanaoendelea na keai yake. Aksasema Fanyeni mnavyooni nyinyi mimi mtu huyu sioni kama ana hatia. Na Damu Yake itakuwa juu yenu na watoto wenu.

Hadi Leo wayahudi hawajapata amani na hawatapata amani hadi Masihi Issa Bin Maryam arudi.

Asalam Aleykum
😅😅😅Jaji Luvandaaaaaa
 
Lisu yupo wapi? Kwanini anamuacha mwenyekiti akiteketea?
 
Mawakili wa serikali mmepewa changamoto

Jul, 15 2021

PROF.KILANGI AWATAKA MAWAKILI WA SERIKALI KUJIELIMISHA KILA UCHAO​

“Lazima muwe na ujuzi wa kusimamia na kuendesha mashauri haya kwa weledi ndani na nje ya nchi inaweza kuwa kwenye Mahakama za Kimataifa au Mabaraza ya kimataifa,” amesema Prof.Kilangi .....

Akielezea changamoto zinazoikabili Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Ndg. Malata amezitaja changamoto hizo kuwa ni uhaba wa mawakili ambapo mpaka sasa ofisi hiyo inao mawakili 88 tu huku mahitaji halisi ya Mawakili ikiwa ni Mawakili 308, uhaba wa watumishi kutoka kada nyingine pamoja na vitendea kazi mbalimbali ikiwemo magari kwa ajili ya kupeka Mawakili Mahakamani.
soma zaidi source : Habari |Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali
 
Back
Top Bottom