Jaji Elinaza Luvanda ajiondoa kuendesha kesi ya Mbowe na wenzake baada ya washtakiwa kudai hawana imani naye

Jaji Elinaza Luvanda ajiondoa kuendesha kesi ya Mbowe na wenzake baada ya washtakiwa kudai hawana imani naye

ucwe mwehu ww,mshatakiwa anayo haki hyo ucwe poyoyo
Awasilishe mahakamani kama anao ushahidi juu ya hayo anayo mtuhumu nayo, sio kumchafua Jiji bila ushahidi.

Kama hakuna ushahidi Jaji aendelee.

Kibatala anazidi kumchimbia shimo bila yeye kujielewa maskini Mbowe!!!

Hoja ya kitoto kweli hiyo eti unamkataa Jaji?!! Tena unatoa tuhuma za kizushi na majungu ya kumchafua Jaji?

Halafu hao mawakili wanamfundisha ujinga kama huo!!
 
Ngoja nikutoe tongotongo. Hati ya mashitaka inapokuwa batili kuna njia mbili za kuitibu. Moja, serikali iamue kuiondoa mahakamani na kuleta hati mpya isiyo na makosa au kuomba amri ya mahakama kuirekebisha bila kuiondoa na kesi iendelee. Pia mahakama pale inapoona kuwa hati ya mashitaka inamakosa, sheria inaipa nguvu mahakama kutoa amri kwa upande wa serikali kurekebisha hati ya mashitaka na kesi iendelee.

Alichokifanya jaji ni kutumia hiyo njia ya mwisho ambayo imepewa mahakama na sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai ambayo ni , pale mahakama inapoona hati ya mashitaka inamapungufu, mahakama inaweza kutoa amri kwa upande wa serikali kurekebisha hayo mapungufu na kesi iendee bila kuifuta kesi yenyewe. Kwa mlengo huu jaji yupo sahihi kabisa.
Kwa maana hiyo unasema katika kesi ya jinai jaji kamwe hawezi kufuta hati ya mashitaka na kufuta kesi? bali anatoa amri wa jamhuri kurekebisha hati ya mashitaka?
 
Unasema pale mahakama inapogundua hati hiyo ina makosa, je katika hii kesi mahakama iligunduaje kwamba kesi ina makosa? Kumbuka Jaji hakuwa na tatizo na hati iliyowakilishwa na jamhuri mpaka pale alipopewa somo na upande wa utetezi kwamba hati hiyo ni batili.

Jaji alikuwa tayari kuendelea na kesi kwa msingi kuwa hakuona tatizo na hati hadi pale utetezi ulipompiga stop kuendelea na kesi kwa kutoa ushahidi kuwa hati ni batili. Na kweli Jaji baada ya kusikiliza hoja ya utetezi na kukubaliana nao alitakiwa kufuta ile kesi mara moja.
Mahakama inaweza kugundua kosa yenyewe (suo moto) au kwa kushtuliwa na upande wowote kwenye kesi. Pia hata kama mahakama ikishtuliwa na upande wowote, tuseme upande wa utetezi. Mahakama inanguvu ya kisheria kutoa amri kwa upande ulioleta hiyo hati(hapa ni serikali tuseme) kurekebisha na kesi iendelee, na hichi ndicho alichokifanya jaji. He is perfectly correct under the law.
 
shukrani Mkuu, ila haitakuwa na sababu kama umeamua kushikilia msimamo wako, bahati mbaya sana msimamo wako sio sahihi sana sasa tutakuwa tunapoteza muda tu Mkuu. Ila ukipata muda jaribu kujifunza Mgongono wa kimaslahi na maadili ya Jaji/Hakimu, kazi za Jaji/Hakimu na wakati gani Jaji/Hakimu anaweza kujitoa kwenye kesi na sababu za kufanya hivyo itakupa mwanga mzuri sana Mkuu, then tutaendelea kupeana elimu.
Hapa nachoona unachotaka kufanya ni kuficha udhaifu wa jaji, hizo sababu ulizoorodhesha za kimazingira na nyinginezo sioni kwanini uzipe kipaumbele wakati inajulikana wazi hati ya mashtaka ikikosewa nini kinafuata, jaji sio kocha ni refarii, anatakiwa awe kati, asijigeuze mwalimu wa upande mwingine wa kesi, hilo naamini hata mtoto mdogo atakubaliana nami, na ndio sababu Mbowe na wenzake wanaamini jaji anatumiwa na mamlaka zake za uteuzi, he is simply under pressure avunje sheria ili kuwalinda jamhuri kwenye hii kesi feki.
 
Jaji asikubali upuuuzi na ushenzi huu wa Mawakili wa Mbowe na Mbowe mwenyewe.

Huko ni kumtusi Jaji na Mahakama,

Mbowe na mawakili wake hawana sababu ya msingi zaidi ya kutaka kumyumbisha Jaji, tuhuma wanazo zitoa dhidi ya Jaji ni za kipuuuzi na hazina uthibitisho wowote zaidi ya kudhania na kuhisia tu, hakuna hoja hapo, kwa hiyo anamtaka Jaji ambaye ni RAFIKI YAKE ili asikilize kesi yake.

kwa hiyo imefikia sasa Mtuhumiwa kuchagua Jaji wa kusikiliza kesi yake aisee! hata marekani hakuna kitu kama hicho.

ninacho sema Jaji angeweza kujitoa kama tuhuma zinazo tolewa na Mbowe zina uthibitisho la sivyo Jaji aendelee tu kungurumisha kesi.......asikubali kubabaishwa na hoja za kipuuzi na za kuokoteza na zenye lengo la kuchelewesha haki kutendeka.
Ameshakubali kujitoa,ata kusoma pia hujui au?
 
Samahani mkuu; ni wakati gani hati ya mashitaka hufutwa na mstakiwa kuachiwa? mimi niliwahi kuachiwa huru mara tano na hati ya mashitaka inafunguliwa upya.
Mwisho wa siku niliishinda Jamhuri baada ya kushindwa kuleta mashahidi mahakamani licha ya kupewa upendeleo na serikali zaidi ya mara tano.

Swali langu: Ni muda/wakati gani Jaji/Hakimu anatakiwa kufuta hati ya mashitaka?
Kuna mazingira tofauti Mkuu, ila Jaji/Hakimu anaweza kufuta mashtaka kama Jamhuri ikishindwa kuonesha kuwa una kosa la kujibu, yaani wakiwa na stori tu alafu bado usionekane uhalifu wako.

wakati meingine ni pale hakuna ushahidi wowote/wakutosha hii sana sana ndio kubwa, hapa utaweka na pale ambapo Jamhuri inasema tu upelelezi haujakamilika kila mara Mkuu.

Kwa haraka ni mazingira haya sana sana, ila sasa unaweza ukatoka mahakamani wakakukamata tena na tena na tena.
 
Mahakama inaweza kugundua kosa yenyewe (suo moto) au kwa kushtuliwa na upande wowote kwenye kesi. Pia hata kama mahakama ikishtuliwa na upande wowote, tuseme upande wa utetezi. Mahakama inanguvu ya kisheria kutoa amri kwa upande ulioleta hiyo hati(hapa ni serikali tuseme) kurekebisha na kesi iendelee, na hichi ndicho alichokifanya jaji. He is perfectly correct under the law.
Hii inazidi kudhihirisha tu udhaifu wa mahakama zetu katika kutoa haki. Jaji anajua kwamba akitenda haki katika kesi kama hii na yeye atakuwa anajitafutia matatizo, hivyo bora kukaa pembeni. Bila shaka ulishuhudia mahakama ilivyopigwa butwaa pale Mbowe alipotoa hoja ya kumkataa Jaji. Jaji alionekana kama vile kautua mzigo mzito aliotwishwa na ulioonekana wazi kabisa kumwelemea.
 
Kwa maana hiyo unasema katika kesi ya jinai jaji kamwe hawezi kufuta hati ya mashitaka na kufuta kesi? bali anatoa amri wa jamhuri kurekebisha hati ya mashitaka?
Hati ya mshitaka ni mali ya jamhuri sio mahakama . Mahakama haina nguvu yoyote ya kisheria kufuta hati ya mashitaka ila kufuta kesi pale tu inapojiridhisha kuwa jamhuri wameshindwa kuthibitisha madai yao yaliyowekwa kwenye hati ya mshitaka. Hivyo ni jukumu la jamhuri kuomba kufuta hati ya mashitaka na sio kufuta kimsingi ni kuiondoa hiyo hati mahakamani na kesi kufutwa. Tofautisha kati ya kesi na hati ya mashitaka. Hivi ni vitu viwili tofauti.
 
Hii inazidi kudhihirisha tu udhaifu wa mahakama zetu katika kutoa haki. Jaji anajua kwamba akitenda haki katika kesi kama hii na yeye atakuwa anajitafutia matatizo, hivyo bora kukaa pembeni. Bila shaka ulishuhudia mahakama ilivyopigwa butwaa pale Mbowe alipotoa hoja ya kumkataa Jaji. Jaji alionekana kama vile kautua mzigo mzito aliotwishwa na ulioonekana wazi kabisa kumwelemea.
Msomi udhaifu uko wapi wakati tuna mahakama zinazofata sheria.
 
Tuhuma alizozitoa Mbowe dhidi ya Jaji Luvanda sio tu zinamchafua yeye bali zinawachafua Majaji wote na Muhimili wa Mahakama.
Hivyo Mbowe na Mawikili wake walipaswa wathibitishe tuhuma hizo nzito.
Mbwa wabwekeao Lori hawana uwezo wa kulikatisha safari yake! Unajionyesha utupu wako uliokujaa kichwani juu ya taratibu za kimahakama! Kazitafute ujitunze ili ujisaidie badala ya kubweka humu! Kama jaji kakiri kuwa hati ya mashtaka kukosewa kimsingi kesi inajifuta automatically kwani ni kupoteza muda na rasilimali pesa kusikiliza kesi isiyokuwepo! Unaelewa Sasa wewe bush lawyer?
 
Kuna mazingira tofauti Mkuu, ila Jaji/Hakimu anaweza kufuta mashtaka kama Jamhuri ikishindwa kuonesha kuwa una kosa la kujibu, yaani wakiwa na stori tu alafu bado usionekane uhalifu wako.

wakati meingine ni pale hakuna ushahidi wowote/wakutosha hii sana sana ndio kubwa, hapa utaweka na pale ambapo Jamhuri inasema tu upelelezi haujakamilika kila mara Mkuu.

Kwa haraka ni mazingira haya sana sana, ila sasa unaweza ukatoka mahakamani wakakukamata tena na tena na tena.
Hii paragraph yako ya mwisho hasa mstari wa mwisho ndio ingeweza kuelezea hoja zako vizuri, kwanza jamhuri ishindwe kesi kwa kukosea hati ya mashtaka, pili Mbowe aachiwe huru, then akitoka nje tu, wamkamate tena wamfungulie mashtaka upya, lakini sio jaji kuwaambia jamhuri warekebishe hati ya mashtaka, hii kitu sijawahi kuiona popote.
 
Hapa nachoona unachotaka kufanya ni kuficha udhaifu wa jaji, hizo sababu ulizoorodhesha za kimazingira na nyinginezo sioni kwanini uzipe kipaumbele wakati inajulikana wazi hati ya mashtaka ikikosewa nini kinafuata, jaji sio kocha ni refarii, anatakiwa awe kati, asijigeuze mwalimu wa upande mwingine wa kesi, hilo naamini hata mtoto mdogo atakubaliana nami, na ndio sababu Mbowe na wenzake wanaamini jaji anatumiwa na mamlaka zake za uteuzi, he is simply under pressure avunje sheria ili kuwalinda jamhuri kwenye hii kesi feki.
Kwa wakili yeyote Jaji ni mwalimu ndio maana tunasoma kesi tofauti tofauti kupata mamlaka yakusema jambo.

Mkuu kuna jambo bado haujaweza kulifahamu vizuri, nitakupa mifano hapa, tuseme haya Jaji angeamua kumuachia huru Mbowe, alafu akatoka tu akakamatwa tena. Unadhani public ingechukuliaje hiyo hali? (Sasa kuna Majaji wanaitwa Grand Judges) hawa ni wazee wakuangalia public sana, pengine Hon. Luvanda ni miongoni mwao. (Sio kosa wala)

Sasa turudi kwenye hili jambo, kwanini sasa kaamua kutolifuta?, kuna mambo mengi miongoni ni

1. Kuitafuta haki kwa pande zote mbili
Hapa haimaanishi kuwa umeona kuna mapungufu na yanaweza kurekebishika basi ukaamua kama Jaji/Hakimu kufuta kesi kwa kuangalia 'teknikaliti'

2. Kuwarahisishia muda wao watuhumiwa
Kumbuka Mh. Mbowe na wenzake wapo ndani bila dhamana, sasa ni vipi kawarahisisgia muda na kuondoa usumbufu?, Akifuta hati watakuwa huru dakika chache wakitoka tu nje pale wakamatwe tena, kesi ianze upya pengine ikachukua muda mrefu zaidi kosa halina dhamana, sasa kwanini Mahakama ipoteze muda kiasi hicho?.

Kumbuka moja ya malengo ya Mahakama Kuu Tz ni kuendesha kesi kwa muda mfupi ziishe.

Unaweza ukasema angejuaje kama angekamatwa tena?, Ipo wazi tu sababu bado Jamhuri ina 'interest' na kesi angekamatwa tu na wangerudi pale pale sasa maana yakr ni nini kwanini asiwaambie warekebishe wailete ikiwa sawa ili hali zipo kesi zinamruhusu kufanya hivyo.

Mkuu hili swala ni lakitaaluma sio kisiasa, tuliangalie kwa jicho la taaluma.
 
Nimejifunza kitu, kumbe kama unaona huyu Jaji ama hakimu haelewekia ama hasomeki kumbe naweza kumkataa tu kisha nikachagua Jaji au Hakimu ninaye mtaka na akasikiliza kesi yangu.
Kumbe siku hizi unaweza kuchagua Jaji ama Hakimu wa kusikiliza kesi yangu. aise!!
Hujaelewa na wala hujajifunza kitu! Unaweza kumkataa hakimu kwa kutokua na imani naye, lakini haimaanishi unachagua jaji au hakimu unaye mtaka! Ukitaka kujifunza au kuelewa, subiri mchakato wa hii kesi utakavyo endelea!
 
Tuwe tunasoma sheria.
Screenshot_20210906-182235.jpg
 
Kesi iendelee. Mawakili wa mbowe wanasumbua mahakama ili kupiga hela ya wafadhili kwamba wanamtetea mteja wao kibaraka wa wazungu.
Unazijua taratibu za mahakama? Jaji kakiri mwenyewe kuwa hati za mashtaka zimekosewa na kashindwa kuitupa kesi yenyewe! Hata mimi ningemkataa Kwa kushindwa kufanya maamuzi kwani hakutakiwa kuwa biased Kwa kiasi kile! Mbowe anakwenda kuwa huru kwani jaji atakayepangiwa anakwenda kuifuta kesi bila masharti ili jamhuri ijifunze kuandaa hati za mashtaka ya kubumba!
 
Back
Top Bottom