Kwa wakili yeyote Jaji ni mwalimu ndio maana tunasoma kesi tofauti tofauti kupata mamlaka yakusema jambo.
Mkuu kuna jambo bado haujaweza kulifahamu vizuri, nitakupa mifano hapa, tuseme haya Jaji angeamua kumuachia huru Mbowe, alafu akatoka tu akakamatwa tena. Unadhani public ingechukuliaje hiyo hali? (Sasa kuna Majaji wanaitwa Grand Judges) hawa ni wazee wakuangalia public sana, pengine Hon. Luvanda ni miongoni mwao. (Sio kosa wala)
Sasa turudi kwenye hili jambo, kwanini sasa kaamua kutolifuta?, kuna mambo mengi miongoni ni
1. Kuitafuta haki kwa pande zote mbili
Hapa haimaanishi kuwa umeona kuna mapungufu na yanaweza kurekebishika basi ukaamua kama Jaji/Hakimu kufuta kesi kwa kuangalia 'teknikaliti'
2. Kuwarahisishia muda wao watuhumiwa
Kumbuka Mh. Mbowe na wenzake wapo ndani bila dhamana, sasa ni vipi kawarahisisgia muda na kuondoa usumbufu?, Akifuta hati watakuwa huru dakika chache wakitoka tu nje pale wakamatwe tena, kesi ianze upya pengine ikachukua muda mrefu zaidi kosa halina dhamana, sasa kwanini Mahakama ipoteze muda kiasi hicho?.
Kumbuka moja ya malengo ya Mahakama Kuu Tz ni kuendesha kesi kwa muda mfupi ziishe.
Unaweza ukasema angejuaje kama angekamatwa tena?, Ipo wazi tu sababu bado Jamhuri ina 'interest' na kesi angekamatwa tu na wangerudi pale pale sasa maana yakr ni nini kwanini asiwaambie warekebishe wailete ikiwa sawa ili hali zipo kesi zinamruhusu kufanya hivyo.
Mkuu hili swala ni lakitaaluma sio kisiasa, tuliangalie kwa jicho la taaluma.