Jaji Francis Mutungi ailima barua CHADEMA, ataka ijieleze ndani ya siku 5

Huyu akiheshimiwa sana ataitwa Jaji Tumbo Mutungi, Jaji Mchongo Mutungi, Jaji Fake Mutungi au Jaji Uchwara Mutungi.

Yaani kumwita huyu Mutingi Jaji, yaani sawa sawa na Jaji Lugakingira au Jaji Nyalali, itakuwa ni kuwavunjia heshima hawa wengine ambao walikuwa majaji hasa, waliouishi ujaji, siyo huyo ambaye anaishi kufuata maelekezo hata kwa mambo.ambayo yeye alistahili kuelekeza.

Hata kama ungekuwa na title gani, usipoiishi hiyo title utadharaulika tu.

'Kuna wanasiasa malaya. Wananunulika. Hawa ni malaya tu' - Mwalimu Nyerere. Kwa maneno ya Mwalimu, hata uwe Rais, Waziri, waziri mkuu, Mwenyekiti au katibu wa chama au mbunge, kama unanunulika, wewe ni mwanasiasa malaya. Title yako tunaiweka pembeni, tutakupa title yako halisi, 'Mwanasiasa malaya ......'.
 
Mutungi anatafuta kiki kupitia Chadema. Hapaswi kujibiwa huo ujinga wake mpaka alete evidence kuwa Chadema ndio waliotengeneza hako kavideo
 


Rais wa awamu ya kwanza anaheshimika sana, ndani na nje ya nchi yetu lakini hadi mauti inamkuta, title yake maarufu na iliyotumika sana ni Mwl. Bado haikuwahi kupunguza hadhi yake.

NB: Siungi mkono mtu yeyote kuvunjiwa heshima Kwa namna yeyote ile. Hata ulipoitwa "njaa" mbele ya waandishi wa habari, binafsi sikufurahia na nilichukulia kama udhalilishaji
 
Mkuu paschal mayala heshima haidaiwi Wala haiombwi huja yenyewe Kwa hili mtungi hastahili heshima hata kidogo ukiwemo wewetetezi wa wajinga
 
Sasa mbona haujaweka hiyo video
 
Ukiwa daktari wa tiba, unatibu wagonjwa, utaitwa Daktari ........ Lakini ikiwa ulisomea udaktari wa tiba lakini kumbe kazi yako kubwa ni ujambazi wa kutumia silaha, siku ukikamatwa utatajwa kwa jina lako halisi, yaani Jambazi Sugu ........, aliyekuwa amejificha kwenye udaktari tiba.

Huyu ni mhalifu aliyejificha kwenye ujaji.
 
Kwahiyo kumuita mtu kwa tittle Ndio Heshima mkuu?
 
Mimi bado sijaelewa maana kwingine nasikia sijui bango limetengernezwa huku JF naona watu wanasema ni video. Kama ni video ya kiongozi wa CCM imevuja halafu CHADEMA wanalimwa barua mbona kama haingii akilini hivi. Nafikiri busara ni huyo mhusika wa hiyo video ndio aulizwe au waipeleke kwa wataalamu wa hiyo fani waifanyie uchunguzi kama ni kweli au wahuni wameitengeneza. Halafu huyo mheshimiwa Jaji Mutungi amewatumia barua CHADEMA ikiwa imeambatanishwa ushahidi/vielezo wa hiyo video au amewatumia barua kavu kavu bila viambatanisho? Hapa JF mtu akiposti kitu watu huwa wanasema habari bila picha haiminiki nadhani basi ni busara kwa Mnyika kumwambia Jaji Mutungi kuwa barua bila hiyo video inakosa mashiko.
 
JF kuanzia moderator na members idadi kubwa ccm walivokuwa vichwa maji wataomba ushaidi.
Na jiuliza kazi search engine na internet ni television ya TBC unasubiria vibindi Wala uwezi kubadilisha
 
Teuzi utaishia kuzisikia kwenye Bomba tu.
 
Video ipi
Mbona Msajili anaasisi vitu tusivyovifahamu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…