Jaji Francis Mutungi ailima barua CHADEMA, ataka ijieleze ndani ya siku 5

Kwahiyo Jaji katuzaa watanzania

Au CPA katuzaa?

Uzee unakujia kwa kasi sana πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ”₯
Pascal Mayalla unapofananisha kiongozi na baba yako mama yako au mjomba wako unakosea sana. Kinachotuunganisha sisi na viongozi iwe wa kuchaguliwa au kuteuliwa ni dhamana na majukumu tuliyowapa kisheria na kikatiba.
Hii dhana ya kuwafananisha na wazazi wetu ndio inatunyima nguvu ya kuwahoji na kuwawabisha, ni kama baba au mama afanye kosa nyumbani ni kweli siwezi kumuitisha kikao au kumtaka awajibike kwakuwa sio baba yangu kwa mujibu wa sheria na katiba. Lakini kiongozi sio mama wala baba yangu akifanya ujinga nitamwambia umefanya ujinga au upumbavu. Hili ni tatizo kubwa sana kwenye nchi za kijamaa ndio mana kuwajibishana kumekua kugumu sababu ya kuangaliana kwa jicho la undugu badala ya uongozi.
 
Hivi kwanini huku kwetu tunapenda sana kutaja hizi title mara Wakili msomi, Dokta, Enginia, CPA, Jaji, Profesa na blablaa nyingi sana ila output zero kabisa...ila ukienda Uchina au Ulaya utasikia wakijitambisha mimi ni Mr xxxx au Miss au Mrs cccc kumbe humo kumbe utamkuta ni Eng. Dr. Xxxx na amefanya tafiti na mambo kibao yaliyoleta tija mwenye jamii.
Hii tamaduni tuliambukizwa na nani? Utamkuta hadi Mhitimu wa kozi ya Uhandisi au Udaktari tayari anajiita Engineer au Doctor baada tu ya kuhutimu chuo.
 
siongezi neno
 
Katika kupambana na watu wa hovyo hovyo, Nyerere alisema heshima ya mtu itokane na huduma yake kwa umma. Huduma za kichizi kama hizi usilazimishe heshima ya kuteuliwa.
 
Mayala=njaa
 
Heshima haijengwi na cheo husika we Mayala!
Heshima hujengwa na mhusika mwenye cheo chenyewe!
Kama mwenye cheo anafanya mambo hovyo hawezi kuheshimiwa hataa kdg, na hii ipo ktk jamii yote
 
Tukiwa nje ya siasa tutafanya hivyo lakini tukiwa ndani ya siasa hizo taito zenu hatuziweki ng'o, mwenyekiti wa CCM hayuko juu ya mwenyekiti wa Chadema na hatakuwa juu yake maisha.
 
Nawaza tu
Hiyo video inaweza kuipita Ile yakulishwa keki Kwa mdomo ya yule Raisi mweusi mfupi!!!

Vitu vingine ni aibu zakujitakia
 
Wabunge walitunga Sheria kwenye mid eighties kwamba wawe addressed Kama 'mheshimiwa' lakini Kuna baadhi ya wabunge hawastahili kuitwa waheshimiwa kwasababu wao wenyewe hawajiheshimu.
Heshma Ni kitu Cha bure lakini anayestahili kuheshimiwa Ni yule anaye jiheshimu yeye mwenyewe.
Usitegemee mbunge shoga au msagaji au mwizi wa Mali ya umma au mwongo nimuite mheshimiwa.
 
Pengine anaondolewa title hiyo kwa umbumbumbu anaonesha ,perhaps
 
Ningesoma mapema ulichomjibu paskol NAMI nisingekoment chochote kwake
 
Aliwakatalia katakata wasithubuti kumbatiza kitu kinaitwa daktari na hadhi hiyo alikuwa nayo

Alikuwa tofauti Sana na wakipekee,sio haya mazee yakileo haya yanakodiwa (uchawa mwingi mpaka weledi hawataki Tena watumie)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…