1.Jamhuri wakaishia njiani kuleta mashahidi waliokuwa nao!
2.Jamhuri wakataka kujua majina na anuani za mashahidi wa utetezi!
3.Siku Moja kabla ya Mbowe kuanza kujitetea,Rais anakutana na viongozi wa dini na anaombwa amalize suala la Mbowe Kwa kumsamehe!
4.Siku Moja baadaye,Magereza wanasema Mbowe ni mgonjwa hivyo hawakuweza kumfikisha mahakamani!
5.Kibatala anasema hana taarifa ya mteja wake kama ni mgonjwa,anaomba basi kama ni hivyo kesi iahirishwe mpaka j3.
6.Mawakili wa serikali waomba kuwasilisha Nia DPP kutoendelea na kesi!
7.Jaji Kwa hasira,anatoa amri Mbowe aachiwe siku hiyo hiyo na si vinginevyo!
8.Mbowe anaachiwa akiwa mzima wa afya na si mgonjwa kama ilivyodaiwa na magereza!
Umejifunza Nini?