Jaji Joachim Tiganga ameikosesha Mahakama point tatu muhimu dhidi ya Serikali

Jaji Joachim Tiganga ameikosesha Mahakama point tatu muhimu dhidi ya Serikali

Kitendo cha Jaji Joachim Tiganga aliyekuwa anasikiliza kesi ya ugaidi dhidi ya Mbowe na wenzake watatu kuamua kuwa wana kesi ya kujibu na baadaye serikali kupitia kwa DPP kusema hawana nia ya kuendelea na kesi kimeidhalilisha sana mahakama.

Endapo Jaji Tiganga angemaliza kesi hii mara baada ya Jamuhuri kumaliza ushahidi wake kwa kuamua kuwa akina Mbowe na wenzake hawana kesi ya kujibu, mahakama ingejijengea heshima kubwa sana kwa Watanzania na Dunia kwa ujumla. Hivi sasa mahakama imedhihirisha haiko huru na inategemea maoni ya serikali kuamua kesi.

Udhaifu huu wa mahakama umemfanya Samia kuwa shujaa (heroine) na kijizolea sifa asizostahili ndani na nje ya nchi. Sifa ambazo mahakama ingezipata kama ingetoa hukumu ya haki.

Jaji Mkuu anapaswa kujitafakari sana na hasa kwa kauli yake ya kuwataka majaji kutoa hukumu kwa kuzingatia maoni ya Jamuhuri.
Kuna watu mabogus hasa vijaji vya mishe mishe kama ilivyotokea kwenye kesi hii. Kikubwa walioshiriki kuanzia polisi na hivo vijaji uchwara wamefaidika Sana na pesa au Kodi za wananchi maposho waliyolipana yalikuwa hayana audit sijui...walikuwa hawapendi mradi wao uishe mapema, umbwa kabisa
 
Japo amepiga pesa Ila Tinganga amejishushia heshima Sana pia ameidharirisha mahakama, Sisi wenye akili timamu toka wale mashahidi wa serikali Kina Inspector Kingai, Mahita Na wenzake walipoanza kutoa ushahidi tukahundua hapa hamna kesi Bali kukomoana tu Ila nimesikitika Sana Kwa Mbowe kuonekana Ikulu punde tu baada ya kuachiwa.
 
Jaji Tiganga alionyesha ukilaza wake pale alipojifanya kusoma na kutolea maamuzi kurasa zaidi ya 1000 za maelezo ya mashahidi kwa masaa chini ya 24 kuwa watuhumiwa wana kesi ya kujibu!
 
1.Jamhuri wakaishia njiani kuleta mashahidi waliokuwa nao!
2.Jamhuri wakataka kujua majina na anuani za mashahidi wa utetezi!
3.Siku Moja kabla ya Mbowe kuanza kujitetea,Rais anakutana na viongozi wa dini na anaombwa amalize suala la Mbowe Kwa kumsamehe!
4.Siku Moja baadaye,Magereza wanasema Mbowe ni mgonjwa hivyo hawakuweza kumfikisha mahakamani!
5.Kibatala anasema hana taarifa ya mteja wake kama ni mgonjwa,anaomba basi kama ni hivyo kesi iahirishwe mpaka j3.
6.Mawakili wa serikali waomba kuwasilisha Nia DPP kutoendelea na kesi!
7.Jaji Kwa hasira,anatoa amri Mbowe aachiwe siku hiyo hiyo na si vinginevyo!
8.Mbowe anaachiwa akiwa mzima wa afya na si mgonjwa kama ilivyodaiwa na magereza!

Umejifunza Nini?
Bonge la picha ya kihindi.
 
[emoji871]Wacha kupotosha Umma wa watanzania.

[emoji871]Chadema hiyo hiyo ndio mliomtuma makamu mwenyekiti wenu Tundu Lissu kwenda kumuombea msamaha huko Ubelgiji.

[emoji871]Ni Chadema hao hao mliomtuma Askofu mkuu KKKT Gideon Shoo akiandamana na Kada mtiifu wenu Askofu Dk Benson Bagonza.

[emoji871]Kumuomba Mh Rais kumuachia huru Mbowe.

[emoji871]Kisheria hiyo kesi kama ingeanza kusikilizwa,kulikuwa Ni no Point of Return.

[emoji871]Wafuasi wa Chadema busara zenu ndogo sana.

[emoji871]Mkipewa fare deal bado mnaendekeza chokochoko tu.

[emoji871]Ndio maana maaskofu makini wa TEC walikataa kuhudhuria kikao kile ili kulinda heshima zao.
Wahi Lumumba chukua buku zako 7
 
Tuvute subira, iko siku mambo yote yatakuwa hadharani. Kama mkapa alifikia kujutia matendo yake, tusubiri wengi zaidi.
 
Hivi hapa Tanzania mtuhumiwa yeyote wa uhalifu akiombewa msamaha kwa rais basi kesi inafutwa ndio sheria za Tanzania zilivyo.

Siku nyingine usikubali watu watambue kwamba wewe ni mpumbavu.
Kama hajaelewa haya maneno mujarabu na machache hivi basi atakuwa katika asilimia zile za TWAWEZA.
 
Jaji angemaliza mapema angekosa kupiga perdiem hapo watu wamepiga pesa ndefu sn kila mmoja siyo chini ya 40M toka kesi ianze nje na mishahara yao
Yawezekana alikuwa ana focus per diem [emoji2]

Too bad kazi yake haina matokeo chanya

Angemaliza mchezo huu mapema ange CEMENT!! (kwa sauti ya jiwe) jina lake kwenye tasnia ya sheria na haki.

Anarudi zake huko mwanza until further notice nobody will care about him
 
1.Jamhuri wakaishia njiani kuleta mashahidi waliokuwa nao!
2.Jamhuri wakataka kujua majina na anuani za mashahidi wa utetezi!
3.Siku Moja kabla ya Mbowe kuanza kujitetea,Rais anakutana na viongozi wa dini na anaombwa amalize suala la Mbowe Kwa kumsamehe!
4.Siku Moja baadaye,Magereza wanasema Mbowe ni mgonjwa hivyo hawakuweza kumfikisha mahakamani!
5.Kibatala anasema hana taarifa ya mteja wake kama ni mgonjwa,anaomba basi kama ni hivyo kesi iahirishwe mpaka j3.
6.Mawakili wa serikali waomba kuwasilisha Nia DPP kutoendelea na kesi!
7.Jaji Kwa hasira,anatoa amri Mbowe aachiwe siku hiyo hiyo na si vinginevyo!
8.Mbowe anaachiwa akiwa mzima wa afya na si mgonjwa kama ilivyodaiwa na magereza!

Umejifunza Nini?
Uongo una njia fupi
 
Baada ya Mbowe na wenzake kuachowa huru bila masharti, nini hatma yetu kufuatia maamuzi kadhaa yaliyofanywa na majaji kwenye kesi ndogo ndani ya kesi iliyofutwa? Nachelea maamuzi yale yaliyotiliwa shaka yanaweza kuwaathiri wengine kama yatatumika. Asante wajuzi kwa kufafanua.
 
Hakuna kitakacho tokea. Maadam ni makada wa chama. Kulindana ndiyo jadi yao.
 
Yatafutwa tu...maamuzi ya kijinga kutoka kwa majaji wa kijinga
 
Mahakama itende haki wakati ilikuwa inapewa maagizo na system namna ya kuendesha hiyo kesi?
Katiba mpya ndiyo suluhisho la madhila yote haya!
 
Ni wapiga dili
Pamoja na yoye haya yaliyojiri, je ile hukunu ya Jaji Tiganga iliyowakuta washtakiwa wana kesi ya kujibu inaweza kupatikana? Tunataka tuichambue kwenye vijiwe vyetu, kwenye vyama vya taaluma za kisheria ndani na nje ya nchi, kwenye law schools na kwengineko. Hiyo hukumu itapatikana?
 
Hivi hapa Tanzania mtuhumiwa yeyote wa uhalifu akiombewa msamaha kwa rais basi kesi inafutwa ndio sheria za Tanzania zilivyo.

Siku nyingine usikubali watu watambue kwamba wewe ni mpumbavu.

[emoji871]Sawa mkuu!

[emoji871]Kubishana na Mpumbavu mwenzangu Sio vizuri ila ngoja uongee kwa macho
[emoji116]

JamiiForums1670963544.jpg
JamiiForums1035408020.jpg
FB_IMG_1646304118714.jpg
JamiiForums-917568599.jpg
JamiiForums308255935.jpg
 
Back
Top Bottom