Jaji Joachim Tiganga ameikosesha Mahakama point tatu muhimu dhidi ya Serikali

Na bado kuna watu wanashupaza misuri kwamba Mbowe na wenzake watatu walikua na vitendo vya kigaidi na kwamba "wamesamehewa"
 
Kama kulikuwa na suala lenye utata kihivyo, jaji asingehitimisha kwamba Mbowe ana kesi ya kujibu. Kama alikuwa na mashaka na lolote basi angedai ufafanuzi toka upande wa mashtaka au utetezi au wote kabla ya kuhitimisha kuwa kuna kesi au hakuna.

Ruling ya jaji katika kila hatua ina uzito mkubwa sana na haitakiwi kutolewa akiwa na mashaka yoyote. Certainly, DPP ame-undermine sana credibility ya mahakama kwa kuiondoa kesi baada ya ruling ile ya jaji. It’s a bizarre contradiction. Tena inaelekea aliwa-surprise wote. It was embarrassing.
 
100% proved with evidence
 
Jaji alikuwa na kibri sana na majivuno. Ameambulia aibu.

Mawakili walimuomba wawakilishe Mhitasari wao kwa mdomo akakataa. Akaahidi kufanya maamuzi ya kesi yenye kurasa 1500 ndani ya siku 2.

Hata kama ni uongo basi ufanyike japo kwa akili kidogo jamani.
 
mahakama au Samia?
usichanganye vitu.
Mahakama walikomaa nae akasoma upepo akashtuka.
Ila vinginevyo ingekuwa bye bye baba jane
Huna habari kuwa mahakama imemwachia huru? Hiyo ndiyo hukumu!
 
Siasa ngumu mno
 
Ndiyo. Au angemgomea DPP na kumtaka aendelee na kesi kwa maslahi ya Taifa. Kama alikwisha thibitisha kwamba Mbowe na wenzake wana kesi ya 'ugaidi' yakujibu, ni aibu kubwa kuifuata kwa urahisi namna hiyo.
Sijui huko aliko anajionaje
 
Na bado kuna watu wanashupaza misuri kwamba Mbowe na wenzake watatu walikua na vitendo vya kigaidi na kwamba "wamesamehewa"
Hawa ni wale watu wanye tabia za kujipendekeza na kiherere ambao Robert Heriel amewaandikia Barua leo
 
namba 4. Kulikuwa na jitihada za kumbembeleza Mbowe na kumuomba msamaha kwa yote waliyomtendea
 
Jaji hakuwa makini na kesi hii kabisa kama ilivyokuwa upande wa mashtaka. Hawakujua kuwa kutunga kesi kunahitaji intelligence ya hali ya juu sana.

Naamini walitegemea mazingira kama ya awamu ya tano ambapo wangeweza kusema chochote na kuamua chochote bila kupingwa wala kujali aibu kwani mamlaka ya uteuzi ingekuwa solidly behind them.
 
mahakama au Samia?
usichanganye vitu.
Mahakama walikomaa nae akasoma upepo akashtuka.
Ila vinginevyo ingekuwa bye bye baba jane
Serikali baada ya kuona haina hoja zisizo na shaka kumfunga Mbowe ikaamua kuweka mpira kwapani kitu ambacho Jaji Tiganga alishindwa kukiona mara baada ya Jamuhuri kumaliza ushahidi wake. Uamuzi sahihi ulikuwa "NO CASE TO ANSWER" lakini Jaji Tiganga akapuyanga!
 

Kama ulifuatilia vizuri hii kesi, majaji wote wawili walionekana kabisa maamuzi yao yako programmed. Na kesi ilipokuwa imefikia ilikaa kisiasa zaidi.
 
umemfanya Samia kuwa shujaa (heroine) na kijizolea sifa asizostahili ndani na nje ya nchi.
mama kachukua point tatu muhimu mno ugenini wakati dunia nzima ikishuhudia, lakini tuliulize je Mahakama zetu zipo huru kiasi tunachofikiria? jibu linaweza kumwokoa Jaji aliyetolea hukumu ndogo suala hili.
 
Lakini kusema mtu ana kesi ya kujibu si sawa na kusema ana hatia.

Mtu anaweza kuwa na kesi ya kujibu bila ya kuwa na hatia.
 
Lakini kusema mtu ana kesi ya kujibu si sawa na kusema ana hatia.

Mtu anaweza kuwa na kesi ya kujibu bila ya kuwa na hatia.
Uko sawa. Lakini Jaji hawezi kutoa ruling kwamba mtuhumiwa ana kesi ya kujibu kama hajawa convinced na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka kwamba mtuhumiwa ana hatia ya makosa mahsusi (specific offenses).

Inawezekana pia akawa hana hatia. Ndio maana, kufikia hatua hiyo, LAZIMA upande wa utetezi upewe nafasi kujitetea kwa ushahidi na vielelezo kupinga ruling hiyo ili kuthibitisha kuwa mtuhumiwa hana hatia.

Kwa DPP, hiyo ni point of no return - in a credible juridical process.
 
Jaji Mkuu anapaswa kujitafakari sana na hasa kwa kauli yake ya kuwataka majaji kutoa hukumu kwa kuzingatia maoni ya Jamuhuri.
Ukweli na usemwe!

Tangu mahakama imekuwa chini ya Jaji Ibrahim kwa sehemu kubwa sana imepoteza imani kwa wananchi. Kwa wa enzi hizo JokaKuu Mag3 Pascal Mayalla watakumbuka mahakama ilikuwaje.

Tuna wa miss sana akina Jaji Nyalali, Kisanga, Samatta n.k

CJ nadhani ni wakati ajitathmini na atoe nafasi kwa mwingine kurudisha heshima ya Mahakama
 
Hakika huyu Jaji Ibrahim aondoke kwa heshima yake kabla mahakama haijapoteza kabisa imani ya wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…