Jaji John Ruhangisa: Kwenye Katiba inayopendekezwa, askari hatakiwi kutekeleza amri ambayo sio halali

tucker carlson

Senior Member
Joined
Oct 5, 2025
Posts
182
Reaction score
759
Aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Prof. John Ruhangisa, ametoa onyo kali kwa vyombo vya ulinzi na usalama, akisisitiza kuwa kwa mujibu wa misingi ya Katiba, askari yeyote hatakiwi kutekeleza amri kutoka kwa bosi au kiongozi wake ikiwa amri hiyo si halali.

"Hata nilikuwa ukisoma Katiba inayopendekezwa, inasema kabisa, hata askari, kwa mujibu wa hii Katiba inayopendekezwa, ambayo ni sawa, hatakiwi kutekeleza amri ambayo sio halali.

Maana yake kuna uelewa mbaya wa kwamba, mimi askari na na kiongozi wangu akitoa amri, nafanya nini? Natekeleza. Iwe amri halali! Wajibu uko kwako kujua je, hii amri ni halali? Kama sio halali, amri inayokupeleka kukinzana na Katiba, hiyo sio halali. Najaribu kufafanua.

Kwa hiyo, ni mapendekezo hayo ili mtu ukishakuwa kiongozi, usije ujione kwamba, 'ah mimi ni Mkuu wa Nchi, au Mkuu wa Polisi, kwa hiyo naweza nikaamuru kamata huyu mtu, piga."

kumbe ni kwenye mapendekezo tu ya katiba. Bas sawa 🐒
 
Ikitokea hivyo policcm watapunguza kujipendekeza kwa watawala.
 
Tunatii amri kwa kuwa tunaogopa kufukuzwa kazi asikuambie mtu kulima kunauma
 
Kama kifungu cha rais kutoshitakiwa akiwa au ametoka madarakani, hakuna sheria yoyote itakuwa na nguvu kuliko amri toka juu. Na amri toka juu ni kutoka kwenye madaraka ya urais.
 
Back
Top Bottom