Jaji M.C. Othman Jaji Mkuu mpya wa Tanzania

Hivi sasa tunataka ateuliwe Pagan ndiyo tuone anafaa? Alipoteuliwa Jaji Ramadhani na huyo huyo JK mbona hapakuwa na maneno? Hivi kuna mtu anaweza ku-punch holes juu ya uwezo wa Jaji Chande ukiondoa "dhambi" yake ya kuwa Muislam. Na kwa hiyo mnachosema ni kwamba kwa vile kaka yake yuko TISS basi yeye aadhibiwe kwa kutopewa haki yake ya kutumikia taifa hili kwa sifa zinazomstahili. Mimi sioni kama hiyo ni issue maana kuna wakati nchi hii Bomani mmoja alikuwa waziri wakati Bomani mwingine akiwa ni Attorney General na wala hakuna aliyekosa usingizi.

Ni jambo la kusikitisha kwamba kuna watu wana phobia mbaya dhidi ya dini za wenzao (namaanisha wote wakristo na waislamu) na utashangaa wenyewe uumini wao unaishia kwenye majina yao tu halafu ndo wako busy kuharibu sifa nzuri za wengine. kwa wanaomfahamu Jaji Chande wanajua kwamba ana elimu nzuri sana ya kutosha, ana uwezo mkubwa sana wa kikazi na ushahidi ni hukumu na maamuzi mbalimbali aliyoyatoa. Uzoefu wake kitaifa na kimataifa hauna ubishi na sidhani kama kuna yeyote kati ya hao washindani wake wanamfikia kwa yote hayo. Kwa taarifa yenu hata ndani ya Judiciary, wengi wa Majaji waandamizi (tena wakristo) walikuwa wanaomba ateuliwe yeye ili alete mageuzi kwenye Judiciary hii yenye changamoto luluki, ikiwemo maslahi duni ya watumishi wake na rushwa iliyokita mizizi. Wafanyakazi hawana ari ya kufanya kazi na wanahitaji mtu atakayetupia jicho na Jaji Chande ni mmoja wa wale wachache wenye uwezo huo. Tukumbuke kauli ya Mwalimu kwamba hatateuliwa au kukataliwa mtu kwa sifa ya dini au kabila lake. Hatuchagui Mufti au Askofu hapa. Hii ni kazi ya kitaaluma na ifikie wakati Rais akifanya uteuzi mahiri na maridhawa apewe sifa zake!
 
Kama TISS wanashirikishwa kwenye uteuzi Wa Jaji mkuu na je Judicial Service Commission wabafanya kazi gani??
 
Kama TISS wanashirikishwa kwenye uteuzi Wa Jaji mkuu na je Judicial Service Commission wabafanya kazi gani??
Haya maswali yote yanakuja baada ya kuteuliwa muislam. Mbona walipoteuliwa majaji wakuu waliomtangulia hamkuuliza? Huyu ni jaji mkuu wa tano ndio mnauliza. Tumewachoka na chuki zenu kwa waislamu na tena wengi wenu nyie ni wapenzi wa CHADEMA, mnaboa sana. Kila kitu udini udini udini tu.
 
Hivi kuna mtu anaweza ku-punch holes juu ya uwezo wa Jaji Chande
most of his judicial experience is not local

na hata huko alikokuwa hakupata courtroom experience yeyote, unless mtuambie aliruhusiwa kuingia mahakama za nchi nyingine, jambo ambalo litaibua maswali ya uraia
 


Lazima tukemee pale tunapoona udini unachukua kasi.
Alishaahidi kila nafasi ikitokea lazima amchague m-kadhi na angalia nafasi zake nyingi za uteuzi.
 
hahahahahah, ili kukata mzizi wa fitini ilibidi awe Nyamburusi Shumbushu Mwakitwange

Au hata wangemteua Ng'wanambogolo kuepuka hisia za udini na kupendeleana.

duh hii nchi jamani!?
 

Samahani kidogo, hapo nilipopigia mstari panaendana kabisa na u-consultant ulioufanya kwa chadema kwenye ubunge wa viti maalum. Ukaamua kujaza watu wa koo fulani fulani na mikoa fulani fulani ili tu kukidhi mahitaji na matakwa ya wachache. Nchi hii watu wanaijua jinsi inavyoendeshwa kiubabaishaji, teuzi nyingi zinafanyika kiundugu, kidini, kikabila halafu hamtaki watu wa-question nia zenu mnapofanya kazi za umma.
 
We huna karatasi ndo mana huwez kurudi,ila sijaona sbb ya kututusi namna iyo aise,ingawa kwel tuna judge mambo kwa kuangalia vitu visivyo kua na maana ila huwez kututusi ivyo,we endelea kubeba box huko si tunajenga nchi huku

Sorry Madcheda, pamoja na kuona kwamba jamaa amekutusi, in practice ni kweli alichosema. Ukweli ni kwamba kuwa muislamu/mkristo maybe hakusaidii chochote kwa jamii za watu hao, na ni ukweli kwamba watanzania ni waongeaji mno kwa kila jambo hata lisilohitaji maelezo mengi kama hili-Badala ya wanaJF kutoa mapungufu kwa CJ aliyepita ili kumpa changamoto CJ huyu na hatimaye matarajio ya watz at-least kufikiwa kupitia mhimili huu, watu wamejikita kwenye muislamu-mdogo wa TISS and the like! ambavyo havimsaidii CJ huyu kushughulikia vitu ambavyo katika uhalisia Taifa linahitaji..
 
Tatizo hapa watu hwaelewi wanachobishana, MC Othman, ana sifa nzuri za kuwa CJ hata zaidi ya sifa alizonazo Kikwete kuwa rais, ana sifa bora zaidi ya kiongozi yeyote yule mwingine wakuteuliwa na rais; however, kuwa na ndugu wawili kwenye jopo la maamuzi inaweza kuraise "conflict of interest". Tunachoitaji ni mtu au taasisi inayatambua kazi za CJ na kazi za TISS (director's order) hatuandikie hapa, then tutajudge na kujua kama JK alikosea au la, siamini kama hakuna mtu mwingine (hata kama muislam) ambaya ana sifa kama zake (othamn) au pengine zaidi yake, na ikumbukwe watu wana doubt si kwa ajili ya uwezo wake bali kuweka ndugu wawili kwenye decisive points siyo vizuri...pengine labda Kikwete angepindisha sheria kidogo apeleke jina lake bungeni lijadiliwe like how they do in the US (senate wanamconfirm):Biography of John G. Roberts
 
Udini udini tu kati ya waisilamu na wakiristu mbona sisi wapagani hatulalamiki na tuko wengi hapa nchini na hatuna waziri hata mmoja!!!!!!
 
Sikubaliani, hata kama ni ndugu haiwezekani wakafanyakazi kwa misingi uliyoandika, wakifanya hivyo waishia kuwa very unpopular katika jamii hii, kitu ambacho sidhani kama wanakihitaji ,
 
Chande ni jaji wa ccm na ndio maana kesi zote za uchaguzi dhidi ya makada maarufu wa chama hicho alizisikiliza yeye na kuwapa ushindi kama vile ile kesi ya uchaguzi dhidi ya Chrisant Majiyatanga Mzindakaya kule sumbawanga!! He is not a judge at par with distingished judges lile the late Mwalusanya and Lugakingira or even Kisanga for that matter!! Kesi zote za ccm watapeta na ndio maana Mkwere alikimbilia kuteua majaji wengi wasiostahili professionally lakini wa------- yake!!
 
Your a great thinker
 
Jamani tusiangalie majina ya watu na dini zao. tukienda hivi na wasilamu naowakiliza ni lini jaji mkuu alikuwa muislamu kabal ya huyu mutawajibuje. Hivi ni nani aliyemteua Jaji Augustino Ramadhani kuwa jaiji Mkuu kumbkumbu zangu ni JK mbona hamkubeba mabango mtaani kumpinga?

Juzi mulimsangilia JK alipomchagua Magufuli na mwakyembe inakuwaje leo munamuona mdini. hembu kuweni neutral alafu muangalie qualification na experience za candidates wote.
Haya munayazungumza lakini mwisho wake ni mbaya itafika wakati tutayakataa majina yetu ya kiarabu na kizungu tubakie na kiasili. tubamie na majina kama Mizengo Pinda na yale ya kati kama Peter tutayakataa ili tuchaguliwe.

soma gazeti la CITIZEN wasifu wakila mtu umewekwa analyse alfu ndiyo uje kutuambia hoja zako.
infact katika watatu hawa wanakaribiana au kulingana experinece yao angalia hata umri unakaribiana inaonyesha muda walikuwa kwenye profession ni sawa laba Othmani ana internation experience zaid ya wenzake.
 
we nawe acha uongo wako,angekua hana imani na wagalatia angemteua mkuu wa majeshi kutoka upande huo?mbona mnapenda kupotosha mambo na kuyakuza bila sababu za msingi.DCI Manumba anaswali msikiti gani?
 

Mi nakuunga mkono ndugu yangu, kuwa chadema sio kupinga tuu kila jambo hata lenye maana. kila kitu udini udini sasa hembu onyesheni mapungufu ya Jaji Othmani ili tuyaone na tulinganishe na mapungufu ya cadidates wengine alafu ndiyo museme museme Othmani hafai.

Kama tutabaki na udini udini kila kitu hata CHADEMA yenyewe tutahama na kurudi zetu CCM

Inashanaza watu kujadili udini ooh mdogo wa nani alfu wanajiita GREAT THINKERS waapi. hembu semeni kama tukiamua asichaguliwe muislamu au mkiristo nani sasa atachaguliwa
 
Siamini sana katika udini..kwasababu nauona kama agenda tu inayomwagwa na wakubwa kwa wananchi wa kawaida..sisi wananchi hatuna udini,na ndio maana wengine tumekuwa darasani kwa zaidi ya miaka 4 bila kufahamu nani ni wa dini gani haswa au wa kabila gani..labda kwa ku-guess tu tukisikia jina lake.
Katika hili la Jaji Mkuu mpya, napata shida kidogo na 'profile yake' aliyeteuliwa..kwamba siioni kama ni ya kuweza kuleta mabadiliko kivile..labda katika hicho alichojipatia ndio ajenge 'profile'.
Kila la kheri Jaji Mkuu mpya..nakubaliana na aliyesema ni kama JK wakati huu anatimiza wajibu tu..lakini si kwa moyo wa 'kuwiwa, na kuumia'!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…