Hivi sasa tunataka ateuliwe Pagan ndiyo tuone anafaa? Alipoteuliwa Jaji Ramadhani na huyo huyo JK mbona hapakuwa na maneno? Hivi kuna mtu anaweza ku-punch holes juu ya uwezo wa Jaji Chande ukiondoa "dhambi" yake ya kuwa Muislam. Na kwa hiyo mnachosema ni kwamba kwa vile kaka yake yuko TISS basi yeye aadhibiwe kwa kutopewa haki yake ya kutumikia taifa hili kwa sifa zinazomstahili. Mimi sioni kama hiyo ni issue maana kuna wakati nchi hii Bomani mmoja alikuwa waziri wakati Bomani mwingine akiwa ni Attorney General na wala hakuna aliyekosa usingizi.
Ni jambo la kusikitisha kwamba kuna watu wana phobia mbaya dhidi ya dini za wenzao (namaanisha wote wakristo na waislamu) na utashangaa wenyewe uumini wao unaishia kwenye majina yao tu halafu ndo wako busy kuharibu sifa nzuri za wengine. kwa wanaomfahamu Jaji Chande wanajua kwamba ana elimu nzuri sana ya kutosha, ana uwezo mkubwa sana wa kikazi na ushahidi ni hukumu na maamuzi mbalimbali aliyoyatoa. Uzoefu wake kitaifa na kimataifa hauna ubishi na sidhani kama kuna yeyote kati ya hao washindani wake wanamfikia kwa yote hayo. Kwa taarifa yenu hata ndani ya Judiciary, wengi wa Majaji waandamizi (tena wakristo) walikuwa wanaomba ateuliwe yeye ili alete mageuzi kwenye Judiciary hii yenye changamoto luluki, ikiwemo maslahi duni ya watumishi wake na rushwa iliyokita mizizi. Wafanyakazi hawana ari ya kufanya kazi na wanahitaji mtu atakayetupia jicho na Jaji Chande ni mmoja wa wale wachache wenye uwezo huo. Tukumbuke kauli ya Mwalimu kwamba hatateuliwa au kukataliwa mtu kwa sifa ya dini au kabila lake. Hatuchagui Mufti au Askofu hapa. Hii ni kazi ya kitaaluma na ifikie wakati Rais akifanya uteuzi mahiri na maridhawa apewe sifa zake!