Jaji Mkuu anapaswa akemee matumizi mabaya ya Mhimili wa mahakama kukomoa wananchi wasiokuwa na hatia

Jaji Mkuu anapaswa akemee matumizi mabaya ya Mhimili wa mahakama kukomoa wananchi wasiokuwa na hatia

Naam, ila ninachoshangaa ni jinsi mnavyokuwa selective kukemea, hadi vifanywe na utawala msioupenda .[emoji23]

Sisi kazi yetu siyo kufuatilia vitendo vya kipumbavu vinavyofanywa na office ya DPP, lakini pale vinapojianika vyenyewe, kama hivi, tunavikemea!
 
Kumekuwepo na kesi za kisiasa ambazo kimsingi hazina ushahidi wa kuthibitisha madai husika.

Raia wamekua wakikaa mahabusu muda mrefu kwa kesi za kubumba kabisa.

Ushahidi wa hayo ni kesi za sabaya ambazo zilifunguliwa kisiasa tu na imethibitika hivyo baada ya mahakama kuona katika kesi zote mbili ushahidi ulikua na utata au hakukuwa na kesi kabisa.

Ukiachana na kushinda kwa kesi hizo zote mbili bado DPP ameruhusu kufungua kesi nyingine kama zile zilizokwisha mkoa mwingine. Mwisho wa kesi hii nao hautakua tofauti sana na hizo nyingine kwani tuhuma zinafanana.

Kutokana na hali hiyo ipo wazi kabisa kwamba mahakama inatumika kama fimbo ya kuumiza Raia.

Na sio jambo jema kwa Jaji mkuu kuruhusu mhimili anao uongoza kutumika vibaya.

Jaji mkuu anapaswa kusimama kidete na kulinda heshima ya mahakama dhidi ya vitendo vinavyopelekea heshima yake kushuka kama hiki cha kutumia mahakama kuadhibu watu.
Mahakama hazikusema kwamba Sabaya hana hatia lahasha! Bali procedural errors tu ndo zimefanya kesi iwe quashed otherwise hatia ipo pale pale endapo all procedures zingezingatiwa.

Acha kujidanganya kwamba Sabaya hana hatia ama hakutenda jinai. Sheria ilivyo unaweza kuthibitika kwamba umefanya mauaji ila kama taratibu zote za kuanzia investigation, arrest, instituting na mambo yote yanayohusiana na proceedings kwa ujumla kama hazikufuatwa vema basi mtu anaweza kuachiliwa huru kwenye rufaa.
 
Mahakama imethibitisha hivyo katika kesi mbili tofauti.

Ushahidi wa kubumba tu.
Mahakama inapomuachia mtu huru haina maana kwamba ameonewa bali katika sheria mtu anaweza kuwa na hatia iliyo wazi kabisa ila upande wa mashitaka ukikosea baadhi ya taratibu za mwenendo wa kesi unavyotaka basi chance ya mtu kuchomoka ni kubwa.

Mfano katika hukumu ya rufaa ya Sabaya hakuna mahali mahakama ya rufaa ilisema kwamba Sabaya hana hatia bali ilitoa sababu zake hasa baadhi ya procedural requirements kutozingatiwa kwenye mwenendo wa utoaji ushahidi ikiwa ni pamoja na shahidi namba mbili kutohojiwa kama sheria inavyotaka.
 
taswira ya ofisi ya DPP imechafuka mbele ya jamii.

Mahakama isikubali kutumika kisiasa.

DPP aonywe anachokifanya sio haki kabisa yeye na ofisi yake.
Mmechafuka nyinyi watetezi wa jambazi
 
Kumekuwepo na kesi za kisiasa ambazo kimsingi hazina ushahidi wa kuthibitisha madai husika.

Raia wamekua wakikaa mahabusu muda mrefu kwa kesi za kubumba kabisa.

Ushahidi wa hayo ni kesi za sabaya ambazo zilifunguliwa kisiasa tu na imethibitika hivyo baada ya mahakama kuona katika kesi zote mbili ushahidi ulikua na utata au hakukuwa na kesi kabisa.

Ukiachana na kushinda kwa kesi hizo zote mbili bado DPP ameruhusu kufungua kesi nyingine kama zile zilizokwisha mkoa mwingine. Mwisho wa kesi hii nao hautakua tofauti sana na hizo nyingine kwani tuhuma zinafanana.

Kutokana na hali hiyo ipo wazi kabisa kwamba mahakama inatumika kama fimbo ya kuumiza Raia.

Na sio jambo jema kwa Jaji mkuu kuruhusu mhimili anao uongoza kutumika vibaya.

Jaji mkuu anapaswa kusimama kidete na kulinda heshima ya mahakama dhidi ya vitendo vinavyopelekea heshima yake kushuka kama hiki cha kutumia mahakama kuadhibu watu.
Kama haki yake ipo ipo tu, Jaji mkuu anaingiliaje badala ya kusubiri kesi ije mahakamani. Kesi ikikaribia kwisha Moshi itafunguliwa nyingine Dar, Mwanza, Morogoro, Tanga, hata Zanzibar, na bahati yote ni matukio tofauti. Unajua kabisa kuwa swahiba wako hasingiziwi hata moja, wewe unafikiri mzee Mroso ambaye kweli amenyang'anywa 90m, Diwani Msangi aliyepigwa makofi, wale waliotobolewa kwa misumari wanajisikiaje, hawana haki wao?! kuna kesi itakayokutana na mahakimu na Majaji sahihi biashara itaisha. Tumieni muda mwingi kuwaomba msamaha wahanga wa matendo ya Sabaya. Kama unaishi nje ya Arusha na Moshi , tembelea maeneo hayo upate habari kamili.
 
Leo kwa Sabaya mnaona ni kaonewa et kesi ya kisiasa mpaka manaitolea povu mahakama mmesahau nyie ndie wale mashabiki mnaoihamasisha mahakama kutumika kwenye kesi dhidi ya wapinzani wenu wa kisiasa. Mlikuwa mnatoa maneno ya kejeli dhidi ya kesi za kina Mbowe na Lisu n.k acheni na nyie muoneshwe inavyokuwaga na uchungu
Mkuki mtamu sana kwa Nguruwe
 
Back
Top Bottom