Tanzania haijawahi kupata Jaji Mkuu wa hovyo kabisa kama Prof. Ibrahim Juma ambaye alikuwa mwalimu wangu pale UDSM na kwa namna alivyokuwa mtu wa staha na mpole na mcheshi kiasi sikutarajia kumbe ana uwezo mdogo wa uongozi wa Mahakama kiasi hiki.
Toka ameteuliwa hii nafasi hajawahi kuitendea haki Kama majaji wakuu wengine waliopita kama Samatta, nk ukiacha majaji wa Mahakama za juu kama marehemu Mwalusanya J, Lugakingira J as he then was.
Ameishia kuwa Jaji Mkuu wa matamko tu Kama mwanasiasa. Ameharibu sana muundo wa seniority kwenye Mahakama na staff ikiwemo muundo wa mawakili, practice, seniority, uchaguzi wa TLS, namna ya ushiriki nk.
Ameishushia Mahakama hadhi yake kwa kuruhusu kuendeshwa kwa kesi zenye utata wa kisheria na kiutendaji pia kesi za uhujumi uchumi ambazo zilikataza dhamana kwa watuhumiwa ingali anafahamu kabisa kwamba right to bail ni haki ya msingi katika utekelezaji wa haki ya mtu binafsi na dhana nzima ya innocence before the court.
Hajawahi kukemea na kuzitamka Sheria kandamini kwamba zipo kinyume na Katiba ya nchi. Amezipokea Sheria kama ya vyombo vya habari, Sheria ya mitandao, Sheria ya uhujumu uchumi, Sheria ya terrorism, na Sheria nyingine nyingi ambazo zipo kinyume na Katiba yetu.
Magufuli alimteua akijua kabisa huyu hajakulipa kwenye judiciary alikuwa lecturer tu hana ethics za uhakimu au judiciary.
Majaji wakuu waliokulia kwenye judiciary Wana sifa ya kutoendeshwa na serikali kuu (executive). Wamekuwa wakikemea sheria mbovu zinazotungwa bungeni na wamekuwa wakizikataa kuzitumia Mahakamani kwa kuwa zilikuwa kinyume na Katiba Ila huyu aliyepo yeye ni matamko ya jukwaani na sio akiwa functus officio.
Ndio maana judiciary imekuwa jalala la lawama za ukandamizaji wa haki ingali mwarobaini wake anaufahamu huyu Shemeji yake Mzee Shimbo.