Jaji Mkuu Masaju: Mishahara ya Majaji ni duni sana, hawana fursa kama mihimili mingine ya dola

Jaji Mkuu Masaju: Mishahara ya Majaji ni duni sana, hawana fursa kama mihimili mingine ya dola

Jaji Mkuu wa Tanzania George Mcheche Masaju akifungua Mkutano wa Tisa wa Kamati ya Utatu (Tripartite Users Committee) kwenye ukumbi wa PSSSF TOWER - Mawasiliano jijini Dar es Salaam, leo 25 Agosti, 2025 amesema, "Kwa sasa, kuna Majaji wanahangaika, Mafao yao hawalipi, wanaleta na vikwazo ambavyo havipo, Katiba iko, Sheria zipo, watu wengine humu Serikalini wanatafsiri vipi Sheria?"

"Jaji wa Mahakama ya Rufaa, au Jaji wa Mahakama Kuu, aanze kuishi kwa manung'uniko! Kwanza Watu hawa Mishahara yao ni duni sana, hawana fursa kama ya watu wengine kwenye hii Mihimili miwili mingine ya dola..."

Mh! Sisi huwa tunawaona majaji wanapata peaa ndefu, ulinzi wa polisi 24hrs lakini hawatosheki. Kweli pesa haitoshi!
 
Si haba hiyo pesa nimesikia huko mnaweza pata heka karibu tano za ardhi huko kjjn

Kuna sehem Kisarawe huko panaitwa marumbo

Heka ya shamba ni 70,000 kufyeka 5000
Kwa jinsi ninavyopenda Kilimo, Wacha nipeleke 1,400,000 nipate hizo ekari 20

Zinaweza kuja kuwafaa Wajukuu zangu miaka 50 ijayo

Naomba namba ya wahusika kama unayo
 
Muelewe vizuri Jaji amefanya comparison na mihimili mingine na hapo analilenga bunge, hoja yake ni sahihi lakini si haki kwa Watanzania hajui kuna Watanzania wanalipwa laki tatu kwa mwezi ambayo ni posho tu ya siku hapo kwenye vikao vyao.

Kinachotakiwa ni haki kwa Watanzania wote kusiwe na gap kubwa ya vipato.

Sasa Jaji anazidiwa mshahara na Kibajaji si dharau hizo.
Hahahahahah sheria ipitishwe ya kulipa wages kwa masaa. Ni muda muafaka wa wizara ya kazi kufanya jambo la maana. Bila hivyo watu wataendelea kulipwa laki 2 na nusu kama mshahara wa kufanya kazi siku 26 kila mwezi.
 
Masaju alipaswa odondoshe hata na kafiga ka.mshahara anakolipwa jaji ili tufanye ulinganifu na hiyo mihimili mingine.

By the way majaji wanatakiwa waishi kwa uadilifu mkubwa mishahara minono itawafanya waishi kwa anasa.
Maoni yangu wapunguziwe hiyo mishahara sasa majaji kama wale wanaoelekezwa na.katuga nn cha kufanya kwa nn wapewe mshahara mkubwa?
 
kuna watu wanadhania kwamba wana hati miliki na serkali.Unajua wewe mwenye fursa ya kufanya marekebisho ya sera au taratibu halafu ukanyamaza ujue kuna wakati itakula kwako tu kama si kwako basi kwa mkeo au kwa mumeo au kwa mwanao ambaye ni mtumishi wa umma .Maana na wewe yanakuhusu.Jifanye Mungu mtu, utakutana nayo huko mbele.

Ni hatari sana kwa mtu anayesimamia haki akifanya hivyo akiwa na njaa
Jambo ambalo huwa nawasihi watu siku zote,mavi yaliyonyeka njia muhimu hayakwepwi kwa kuyaruka,utayakuta tena kesho,fanya uyaondoe kabisa.

Matumbotumbo huwa wanashida hizo za kujisahau kuwajibika,wakistaafu akili zinarudi eneo lake,pale usafiri wa serikali haupo,maji,nyumba,umeme,ulinzi hakuna,wala bima ndipo unavundua kumbe laki 5 ni kweli ni pesa ndogo sana kuwa mshahara wa mtu.
 
Back
Top Bottom