Haya yako wazi hata kwenye Katiba na Sheria ya vyama vya siasa, alichofanya Prof Ibrahim Juma ni kukumbusha tu. Bahati mbaya anakumbusha mambo ya msingi wakati uongozi wa JPM haujali misingi ya utawala wa Sheria, demokrasia na katiba yenyewe.
Yeye mwenyewe Prof Juma kama Chief Justice yuko mfukoni mwa JPM. Hawezi kuamua kwa namna anavyoelewa na anavyoamini bali kwa vile anavyotaka JPM. Mfano ni maamuzi ya kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Advocate Sanga vs AG juu ya haki ya dhamana. Au kesi ya Bob Wangwe vs Ag juu ya Wakurugenzi kuwa wasimamizi wa uchaguzi.
Tukubali tu JK alituingiza mkenge kutomaliza mchakato wa Katiba Mpya mwaka 2015.