Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma: DPP ni chujio la kwanza la haki

Hata huko mahakamani kulikuwa na shida hasa kwa kesi za madai yanayohusu serikali.

Huwa nawaza labda kuna haja ya (mahakama ya rufani?) kufanyia mapitio ya kesi zote zilizoamuliwa kuanzia 2016 mpaka 2020 hivi ("suo motu"?). Ninaamini maamuzi mengi yalifanywa kufurahisha au kukwepa kuukera utawala wa wakati huo na hivyo baadhi ya watu kupoteza haki zao. Kiroho safi tu.
 
We nenda tu ukajichimbie huku
 
Biswalo aliifanya ofisi ya DPP kuwa ni sehemu mojawapo ya makazi ya shetani, naye binafsi akiwa mhudumu mkuu katika jumba la shetani.
 
Huyu Pro naye sijui Jaji Mkuu huwa sijui hata anafanya nini huyu mzee? kazi yake kubwa ni kulalamika kama wananchi wanavyolalamika. Over
Huyu jaji mkuu alikuwa anashiriki mpaka vikao vya siri vya chama kwaajili ya kupanga hukumu za wasiotakiwa na jiwe.
 
Hakuna mwenye akili anayeweza kuuliza maana ya kubambikizia mtu kesi.
 
Sasa Kama dpp atapeleka kesi za ovyo mahakmanai kwa jaji si anauwezo was kumuachia mtu huru na siyo dpp ..hvyo professional ibrahimu jumaa akiona kuwa dpp katk keai hii an uwezo wa kutupilia mbali
 
Tangu tupate uhuru, hatukuwahi kuwa na jaji mkuu asiye na msaada katika kulinda haki, ka huyu wa sasa.
 
Kama una furaha malalamiko ya nini?
Magufuli kafa, Samia ni Rais, deal with that

Na wazazi wangu wote wapo hai
 
Imagine, cases kama hizi:[emoji116]

Nimemsikia mama akisema TAKUKURU wamefuta kesi 147 walizowabambikia watu. Pigia mstari neno KUBAMBIKIA. Yani TAKUKURU wanakiri mbele ya Rais kuwa waliwabambikia watu kesi na wamekubali kuzifuta. Nimewaza sana kuhusu hao waliobambikiwa, familia zao, watoto wao na ndugu zao.

Nimemkumbuka rafiki yangu Abraham Ngoti ambaye TAKUKURU walimkamata huko Dodoma wakidai kuna kiasi kikubwa cha pesa kimeingizwa kwenye account yake. Akatakiwa kujieleza ni za nini? Wakamsafirisha usiku kama jambazi wakamleta Dar. Wakamuweka mahabusu yao kule Upanga.

Baada ya siku mbili TAKUKURU wakasema amejinyonga akiwa mahabusu. Familia haikukubaliana na taarifa hiyo kutokana na mazingira ya kukamatwa kwake hadi kufariki. Alijinyongaje mahabusu? Hakukua na ulinzi? Je inawezekana kujinyonga kwa kutumia suruali ya jeans? Inawezekana kujinyonga dirishani hadi kufa bila kujitetea kwa kushika nondo za dirisha? Inawezekana kujinyonga miguu ikiwa imegusa chini?

Maswali haya ndio yaliyofanya familia yake kuomba iundwe tume huru ifanye uchunguzi juu ya kifo cha ndugu yao. Lakini hakuna kilichofanyika. Waliambiwa maiti yenu hiyo hapo, mkazike.

Nimejaribu kuwaza hivi kama alibambikiziwa kesi kama hawa 147 anajisikiaje huko alipo. Kama wafu wanaona yanayoendelea duniani pengine anawalaani sana TAKUKURU.

Nampongeza mama kwa jitihada zake za kuibadilisha TAKUKURU. Nampongeza pia kwa kutoa maelekezo kwenye vyombo vingine kama Polisi na ofisi ya DPP. Lakini naomba atilie mkazo maelekezo hayo maana kuna wengi wamebambikiwa kesi na wanasota gerezani.

Mdude Nyagali anateseka rumande zaidi ya mwaka mmoja. Kila siku Jamhuri inaomba kesi isogezwe mbele kwa sababu ushahidi haujakamilika. Lakini ni Jamhuri hiyohiyo iliyosema imemkamata Mdude na kete za heroine nyumbani kwake. Kama kweli walimkamata na heroine ni ushahidi gani zaidi wanatafuta mwaka mzima?

Mazingira kama haya ndio yanafanya familia ya Mdude ihisi kwamba huenda kesi ya ndugu yao ni ya kubambikiziwa pia. Mama tafadhali ingilia kati. Taifa limepita kipindi kigumu sana wakati wa mwendazake, ni wakati sasa wa kuponya majeraha. We need truth and reconciliation.! MALISA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una point lakini tukiendelea kuwa na watu wanaodhani wajibu wao ni kwa aliyewateua na sio katiba waliyoapa kuilinda, basi hata iwe nzuri vipi itavunjwa with impunity.

Amandla..
 
Pole sana. Mimi mawazo yangu haitoshi kusema tu kuwa watu walioonewa wameachiwa bila kusema watesi wao wamechukuliwa hatua gani. Ujumbe unatakiwa kutolewa kuwa ukifanya uovu utalipa. Nje ya hivyo wataendelea kufanya.

Amandla...
 
Mahakama lazima iwe na uwezo wa kuingilia kazi ya DPP
 
Nurembag defense
Biswalo mnamuonea bure, ni nani aliweza kwenda kinyume na Jiwe kipindi cha utawala wake? Wengine si wamekimbia mpaka nchi kumuogopa Jiwe? Mlitaka Biswalo apingane naye yampate ya kumpata?
 
Biswalo mnamuonea bure, ni nani aliweza kwenda kinyume na Jiwe kipindi cha utawala wake? Wengine si wamekimbia mpaka nchi kumuogopa Jiwe? Mlitaka Biswalo apingane naye yampate ya kumpata?
Naunga mkono hoja kwamba kila mtu anapenda maisha yake, hao CHADEMA wenyewe wanamzomea Biswalo viongozi wao walikimbia nchi kwa kuogopa, Ila wanataka Biswalo ndo angejitoa muhanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…