Imagine, cases kama hizi:[emoji116]
Nimemsikia mama akisema TAKUKURU wamefuta kesi 147 walizowabambikia watu. Pigia mstari neno KUBAMBIKIA. Yani TAKUKURU wanakiri mbele ya Rais kuwa waliwabambikia watu kesi na wamekubali kuzifuta. Nimewaza sana kuhusu hao waliobambikiwa, familia zao, watoto wao na ndugu zao.
Nimemkumbuka rafiki yangu Abraham Ngoti ambaye TAKUKURU walimkamata huko Dodoma wakidai kuna kiasi kikubwa cha pesa kimeingizwa kwenye account yake. Akatakiwa kujieleza ni za nini? Wakamsafirisha usiku kama jambazi wakamleta Dar. Wakamuweka mahabusu yao kule Upanga.
Baada ya siku mbili TAKUKURU wakasema amejinyonga akiwa mahabusu. Familia haikukubaliana na taarifa hiyo kutokana na mazingira ya kukamatwa kwake hadi kufariki. Alijinyongaje mahabusu? Hakukua na ulinzi? Je inawezekana kujinyonga kwa kutumia suruali ya jeans? Inawezekana kujinyonga dirishani hadi kufa bila kujitetea kwa kushika nondo za dirisha? Inawezekana kujinyonga miguu ikiwa imegusa chini?
Maswali haya ndio yaliyofanya familia yake kuomba iundwe tume huru ifanye uchunguzi juu ya kifo cha ndugu yao. Lakini hakuna kilichofanyika. Waliambiwa maiti yenu hiyo hapo, mkazike.
Nimejaribu kuwaza hivi kama alibambikiziwa kesi kama hawa 147 anajisikiaje huko alipo. Kama wafu wanaona yanayoendelea duniani pengine anawalaani sana TAKUKURU.
Nampongeza mama kwa jitihada zake za kuibadilisha TAKUKURU. Nampongeza pia kwa kutoa maelekezo kwenye vyombo vingine kama Polisi na ofisi ya DPP. Lakini naomba atilie mkazo maelekezo hayo maana kuna wengi wamebambikiwa kesi na wanasota gerezani.
Mdude Nyagali anateseka rumande zaidi ya mwaka mmoja. Kila siku Jamhuri inaomba kesi isogezwe mbele kwa sababu ushahidi haujakamilika. Lakini ni Jamhuri hiyohiyo iliyosema imemkamata Mdude na kete za heroine nyumbani kwake. Kama kweli walimkamata na heroine ni ushahidi gani zaidi wanatafuta mwaka mzima?
Mazingira kama haya ndio yanafanya familia ya Mdude ihisi kwamba huenda kesi ya ndugu yao ni ya kubambikiziwa pia. Mama tafadhali ingilia kati. Taifa limepita kipindi kigumu sana wakati wa mwendazake, ni wakati sasa wa kuponya majeraha. We need truth and reconciliation.! MALISA
Sent using
Jamii Forums mobile app