TANZIA Jaji Mstaafu wa mahakama Kuu, Upendo Msuya afariki dunia

TANZIA Jaji Mstaafu wa mahakama Kuu, Upendo Msuya afariki dunia

Roho ya mtu haifi ila humrudia Yeye aliyeitoa..

Kwa Wakristo

Mhubiri 12:7
[7]Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa,
Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.
Umeijibu sawa kabisa Otorong'ong'o...ila ni roho siyo Roho....Najua umenielewa...Kitambo tulipokutana kwenye kudadavua vile vitabu vilivyondolewa kwenye Biblia...Shalom.
 
Natoa pole kwa wanafamilia wote Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu mnacho kipitia.
 
Dunia tunapita tu,kama alimhukumu mtu kwa upendeleo ndio hapo pabaya.Alale alipojichagulia.Poleni wafiwa,muwe na subira.
 
Aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu ambaye amejiuzulu hivi karibuni, Upendo Msuya amefariki leo Julai 19 baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa kiharusi.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu, mjomba wa marehemu, Niva Mbaga amesema kwamba marehemu amefariki akiwa Hospitali ya Kairuki alipokuwa amelazwa.

Amesema kwamba shughuli za mazishi zinafanyika nyumbani kwa marehemu Tegeta jijini Dar es Salaam.

“Amesumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa kiharusi hivyo akawa anapelekwa hospitali na kurudi nyumbani zaidi ya miezi mitatu sasa na leo hii amefariki dunia’’ amesema Mbaga
Amesema marehemu ameacha watoto wanne.
 
kwenye taaluma ya sheria kujua jaji ametoa hukumu ngapi na ipi more authoritative ni jambo la sifa na ni kawaida. RIP JAJI MSUYA.

Kajifunze Kwanza maana ya actual communication context na actual communication content kisha ukishaelewa rudi tena uendeleze huu ' Upupu / Upuuzi ' wako uliouanika hapa. Hivi huko Vyuo Vikuu mnakoenda kusoma huwa mnajifunza nini kama vitu vidogo tu hivi vya uwasilishaji wa ujumbe au taarifa mahala au kwa wakati muafaka hamjui? Halafu mnajiita Wasomi. Shame on you!
 
Pumzika kwa amani Jaji... Ulikaa kwenye kiti cha kutoa haki Duniani, sasa unaenda kukutana na haki isiyo na unafiki mbele ya kiti cha hukumu chake Muumba. I hope utapenya salama...

Nimeona hii post yako instagram kuna mbwiga kaipeleka huko, amekutaarifu?
 
Kajifunze Kwanza maana ya actual communication context na actual communication content kisha ukishaelewa rudi tena uendeleze huu ' Upupu / Upuuzi ' wako uliouanika hapa. Hivi huko Vyuo Vikuu mnakoenda kusoma huwa mnajifunza nini kama vitu vidogo tu hivi vya uwasilishaji wa ujumbe au taarifa mahala au kwa wakati muafaka hamjui? Halafu mnajiita Wasomi. Shame on you!
Will 'not argue with someone who is ignorant in law'
 
RiP Jaji Mama Msuya!!! Pole sana na familia! Pumzika kwa Amani
 
Back
Top Bottom