TANZIA Jaji Mstaafu wa mahakama Kuu, Upendo Msuya afariki dunia

TANZIA Jaji Mstaafu wa mahakama Kuu, Upendo Msuya afariki dunia

Sijaelewa hata umeandika nini Mkuu. Hebu tulia halafu rudia kuandika tena ili angalau nikuelewe unachotaka kusema kusudi nisije nikachuma bure dhambi kwa Mwenyezi Mungu kwa kukufananisha Wewe na Matahaira / Wendawazimu.
nipo very certain ujumbe wangu umekujeruhi after fully understood it...ndiyo maana mwisho wa reply yako ukamalizia calling names...who cares ??For sure your green brains its not for reasoning!!
 
Roho ya mtu haifi ila humrudia Yeye aliyeitoa..

Kwa Wakristo

Mhubiri 12:7
[7]Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa,
Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.

Roho bila mwili?
Basi jua hakuna mtu anae lala sehemu salama. Mtu anapokufa hajui nini kinaendelea duniani
 
RIP Judge Upendo Msuya. Poleni Wafiwa.

Nasikitika kuwaarifu kuwa Mhe Jaji Upendo Msuya,(rtd) amefariki usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Kairuki. Hakika sisi sote ni wa Mungu na kwake yeye tutarejea.

Mada zinazomhusu Jaji Msuya
Maamuzi ya Jaji Upendo Msuya yasababisha watuhumiwa wa madawa ya kulevya kutoweka

Tetesi: - Zinazodaiwa kuwa sababu za RC Meck Sadiki, Jaji Mujulizi na Jaji Upendo Msuya kuacha kazi

RC wa Kilimanjaro, Meck Sadiki na Majaji wawili Wajiuzulu. Rais Magufuli aridhia...
 
Hakika kifo ni mawaidha na mazingatio tosha. Ishi utakavyoishi wewe ni marehemu mtarajiwa. Utakufa tu na kurejea kwa Mola wako utake usitake. Inastaajabisha sana sisi wanadamu jinsi tunavyoshobokea dunia ilhali uhai wenyewe ni mfupi!! Mbaya zaidi baadhi yetu tunakuwa madhalimu wa haki za watu, huku tukijawa na kibri utadhani tutaishi milele. Dunia ni kama nyuki daima haikumbatiwi! Kila la heri Jaji Msuya. Mungu akuweke mahali unapostahili.
 
Tunaposema RIP mara nyingi twakosea, mtu akifa amekufa hajui chochote kinachoendelea duniani

Zaidi tutoe pole kwa familia yake na ndugu zake na watu waliokuwa karibu naye
Mimi nilishaacha kutumia hicho kirai. Muhimu ni kufariji familia iliyobaki na pale inapokuwa inahitajika, kuwasaidia kwa hali na mali.
 
Mimi nilishaacha kutumia hicho kirai. Muhimu ni kufariji familia iliyobaki na pale inapokuwa inahitajika, kuwasaidia kwa hali na mali.

Kuna watu wanakesha wakiombea waliokufa, kitu ambacho si sahihi, mtu ukifa yako yameishia hapo.. kama ulikuwa mwema basi mema yako umekufa nayo, kama ulikuwa mtenda mabaya mabaya yako unaingia nayo kaburini hata watu waombe kila siku hakuna kitakacho badilika.....
 
Kwa imani yako na vitabu unavyosoma wewe hatuna haja kuviamini, wala sio lazima kufuata unachoona wewe kuwa ni sawa, kila mtu ana imani yake na maono yake na mtazamo wake jinsi anavyoamini yeye,
Wewe nani hata utuambie "sio sahihi" kwa nini tukuamini wewe kwa lipi?
Hakuna aliyekufa akarudi atuambie kama maombi hayo yalimsaidia au hayajamsaidia, kama tuna mwamini Mungu na tunaamini anatusikiliza iweje asisikilize tukiomba kwa ajili ya mpendwa wetu,
Hatuna sababu ya kuiga uvivu wako wa kufikiri. Shame on you !!!!!!
 
Kwa imani yako na vitabu unavyosoma wewe hatuna haja kuviamini, wala sio lazima kufuata unachoona wewe kuwa ni sawa, kila mtu ana imani yake na maono yake na mtazamo wake jinsi anavyoamini yeye,
Wewe nani hata utuambie "sio sahihi" kwa nini tukuamini wewe kwa lipi?????
Hakuna aliyekufa akarudi atuambie kama maombi hayo yalimsaidia au hayajamsaidia, kama tuna mwamini Mungu na tunaamini anatusikiliza iweje asisikilize tukiomba kwa ajili ya mpendwa wetu,
Hatuna sababu ya kuiga uvivu wako wa kufikiri. Shame on you !!!!!!

Mhubiri 9:5, 6
5 Kwa maana walio hai wanajua kwamba watakufa;+ lakini wafu, hawajui lolote kamwe,+wala hawana malipo tena, kwa maana kumbukumbu lao limesahauliwa.+ 6 Pia, upendo wao na chuki yao na wivu wao tayari zimepotea,+ na mpaka wakati usio na kipimo hawana fungu lolote tena katika chochote ambacho kitafanywa chini ya jua.+
 
Mungu amlaze panapostahiki, kafa lkn kaacha alama ya kazi nyingi sana alizofanya kwa mikono yake kuliangamiza Taifa letu, huyu mama kaharibu kesi nyingi sana za dawa za kulevya, huyu ni mmoja ya wale Majaji aliosema Sianga kua walitumika kuharibu kesi nyi za dawa, ni jambo lazma tuĺiseme maana hakuna namana, na pia tujifunze kwamba dunia tunapita tu, ni heri kufanya mambo mema maana kesho tutaulizwa kwa Maulana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tulio bakia duniani tutende haki na tufahamu kuwa ipo siku na wewe lazima utakufa tu, tuache kiburi na dharau sote ni mavumbi tu!
 
Back
Top Bottom