Jaji Mustapha Mohamed Siyani aliyekabidhiwa kesi ya Ugaidi ya Mbowe ni nani?

Jaji Mustapha Mohamed Siyani aliyekabidhiwa kesi ya Ugaidi ya Mbowe ni nani?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
MFAHAMU_JAJI_MUSTAPHER_SIYANI_ALIYEPANGIWA_KESI_NA.16_2021_INAYOMKABILI_MBOWE_NA_WENZAKE.__Jaj...jpg

Kwa ufupi sana Jaji huyu Mustapha Mohamed Siyani aliapishwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu kanda ya Dodoma siku ya Ijumaa tarehe 20 April 2018, na Aliyekuwa Rais wa Tanzania wa awamu ya 5 Dr John Magufuli, Baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo tarehe 15 April 2018 .

Pia amewahi kuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma.

NOTE : Jaji wa Mahakama Kuu ni mtumishi wa Umma, kumfahamu haijawahi kuwa kosa kisheria

Mustapha_Mohamed_Siyani._Jaji_wa_Mahakama_Kuu,_pia_amewahi_kuhudumu_kama_Jaji_Mfawidhi_wa_Maha...jpg
 
Muhimu aitendee haki taaluma yake ili wengi wawe na imani na muhimili wa mahakama Tanzania ambao umekuwa ukipoteza heshima yake kila kukicha.
Na hasa akihukumu bila kuangalia sura ya mtu.
 
Muhimu aitendee haki taaluma yake ili wengi wawe na imani na muhimili wa mahakama Tanzania ambao umekuwa ukipoteza heshima yake kila kukicha.

Uwepo wa mhimili uliojichimbia zaidi kwa mujibu wa katiba ya Tanzania kunatia ukakasi sana:

1. Hawa ni sehemu ya vigogo wanufaika wa lile saga la kutolipa kodi kwa mujibu wa katiba.
2. Hawa hawawajibiki kwa lolote katika maamuzi yao.
3. Hawa ni wateuliwa wa ule mhimili ule wenyewe.

Salama zaidi ya haki kutendeka ilikuwa kwenye kuonyeshwa kwa jitihada za kudai katiba mpya kwa ari zaidi.

Kusikia miito tu kwa masikio yakiwa makavu hakujawahi kuwa uwezekano kwenye dunia yetu.
 
Tatizo sio judge kwamba ni muadilifu au sio, tatizo ni mfumo unatumika kumchagua na kumuapisha huyo judge..mfumo ndio root of all evil...huyu na aliepita wote wamechaguliwa na mfumo ule ule....as a person anaweza akawa mtu muadilifu kweli anaependa haki na kuona haki inatendeka...but kwa mfumo ulipo sasa na kwa uzito wa case kama hii....the only way forward ni mfumo mpya utakaoletwa na katiba mpya..
 
Majaji wote walioteuliwa na marehemu siyo wa kuwaamini. Labda jaji kama alikuwa anafanya matendo anayotaka marehemu ili ateuliwe kuwa jaji.

Marehemu hakuwahi kumpenda mtu anayependa haki. Kigezo chake kikuu kwa uteuzi wowote, ni mteuliwa kumsujudia yeye na kumkubalia yeye kwa kila jambo hata kama jambo hilo ni hovyo kiasi gani.
 
Uwepo wa mhimili uliojichimbia zaidi kwa mujibu wa katiba ya Tanzania kunatia ukakasi sana:

1. Hawa ni sehemu ya vigogo wanufaika wa lile saga la kutolipa kodi kwa mujibu wa katiba.
2. Hawa hawawajibiki kwa lolote katika maamuzi yao.
3. Hawa ni wateuliwa wa ule mhimili ule wenyewe.

Salama zaidi ya haki kutendeka ilikuwa kwenye me wa jitihada za kudai katiba mpya kwa ari zaidi.

Kusikia miito tu kwa masikio yakiwa makavu hakujawahi kuwa uwezekano kwenye dunia yetu.

Mkuu una majibu yako. Mana kuna watanzania Zaidi ya Elfu Kumi na tano jela. Sasa sijui hawa haya ya katiba yanawahusu au hayawahusu. Toka 1977 wangapi wamehukumiwa. Je katiba itafanya muuaji asiwe muuaji au Vipi. You are boring.
 
You think you are not boring?

1. Hawa vigogo wanalipa kodi?
2. Ule mhimili uliojichimbia zaidi kwa mujibu wa katiba haupo?
3. Hawa vigogo wana wajibika kwa lolote katika maamuzi yao?

I repeat: "you're boring!"
 
Mkuu una majibu yako. Mana kuna watanzania Zaidi ya Elfu Kumi na tano jela. Sasa sijui hawa haya ya katiba yanawahusu au hayawahusu. Toka 1977 wangapi wamehukumiwa. Je katiba itafanya muuaji asiwe muuaji au Vipi. You are boring.
Inafaa apendekeze kesi ya Mbowe isiendelee kwanza huku akisubiria kwa kukaa ndani mpaka ipatikane Katiba mpya ili apatikane Jaji wanae mridhia atakaetenda haki.
 
Back
Top Bottom