Jaji Mustapha Mohamed Siyani aliyekabidhiwa kesi ya Ugaidi ya Mbowe ni nani?

Jaji Mustapha Mohamed Siyani aliyekabidhiwa kesi ya Ugaidi ya Mbowe ni nani?

Kwa ufupi sana Jaji huyu Mustapha Mohamed Siyani aliapishwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu kanda ya Dodoma siku ya Ijumaa tarehe 20 April 2018 , na Aliyekuwa Rais wa Tanzania wa awamu ya 5 Dr John Magufuli , Baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo tarehe 15 April 2018 .

Pia amewahi kuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma .

NOTE : Jaji wa Mahakama Kuu ni mtumishi wa Umma , kumfahamu haijawahi kuwa kosa kisheria

View attachment 1929656
Ndio huyo kavaa gagulo la Mo Extra?
 
Ni ngumu sana uongo kukaa na kujificha kwenye ukweli huyo aliyesimama nae inatoa jibu yuko upande gani.

....... wafananao huruka kwa makundi.
 
Huyu bwana mdogo kapewa fursa ya kipekee kabisa anayoweza kupewa mtu kuonyesha heshima ya kazi anayoitenda.

Kazi pekee anayotakiwa kuifanya ni kufuata matakwa ya sheria inavyoelekeza bila kuyumbishwa na mtu yeyote. Atakuwa amejijengea heshima kubwa akifanya hivyo.
 
Mbowe akitaka na huyu abadilishwe nayo pia sio shida, kitu cha muhimu afahamu aliyeko mahabusu ni yeye sio majaji
Mbowe huenda maisha ya huko mahabusu ameyapenda na kuyafurahia. Siri anaijua mwenyewe
 
Mbowe akitaka na huyu abadilishwe nayo pia sio shida, kitu cha muhimu afahamu aliyeko mahabusu ni yeye sio majaji
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kwamba wamejipanga anamkataa huyu anakuja mwingine. Yeye anaendelea kujea ndoo. Wa mwisho anapiga mvua
 
Ukiwaza kwa kutumia kijambio uko sahihi.lkn kiukweli nchi nzima iko lock up.mbowe anatuwakilisha tuu
Anakuwakilisha wewe. USITUSEMEE. Mnajidanganya vingi. Kuna Uhuni wa serkali lkn kuna Uhuni Mkubwa kwenu. Tuko kati hatuoni wa maana
 
Tutegemee kesi ayakayosimamia Mh. Mustapha Siyani itakuwa ya kihistoria na kuandikwa sana jinsi mawakili watakavyotoana jasho kumshawishi jaji kwa hoja na vifungu vya sheria n.k

Rejea

Tuesday September 17 2013​


Mwananchi
Advertisement


Hati ya Notisi , Mawakili watoana jasho kesi ya dawa za kulevya​

Tuesday September 17 2013​


Kesi ya dawa za kulevya inayomkabili raia wa Kenya, Mwanaidi Ramadhani Mfundo, maarufu kwa jina la Mama Leila au Naima Mohammed Nyakiniwa na wenzake wanane, imeendelea kugubikwa na utata wa kisheria na kuzua mvutano uliosababisha iahirishwe kwa mara nyingine ili kusubiri uamuzi wa Mahakama.


Mawakili watoana jasho kesi ya dawa za kulevya

IN SUMMARY​

Wakili wa utetezi, Evod Mmanda alisema haikuwa sahihi kwa upande wa mashtaka kuwasilisha taarifa hiyo mahakamani hata kabla ya uamuzi wa Mahakama.
Advertisement
Dar es Salaam. Kesi ya dawa za kulevya inayomkabili raia wa Kenya, Mwanaidi Ramadhani Mfundo, maarufu kwa jina la Mama Leila au Naima Mohammed Nyakiniwa na wenzake wanane, imeendelea kugubikwa na utata wa kisheria na kuzua mvutano uliosababisha iahirishwe kwa mara nyingine ili kusubiri uamuzi wa Mahakama.
Jana, Mahakama Kuu ilitengua hoja iliyozua mvutano mkubwa juzi kwa kuruhusu upande wa mashtaka kuwasilisha notisi ya kuongeza shahidi muhimu kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Eva Mamuya jambo lililopingwa na upande wa utetezi.
Mbali ya Mama Leila, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Anthony Arthur Karanja na Ben Ngare Macharia (wote Wakenya). Wengine ni Watanzania watano, Sarah Munuo, Almas Said, Yahya Ibrahim, Aisha Kungwi, Rajabu Juma Mzome na John William.
Wakati upande wa utetezi ukipinga uamuzi huo wa jana, upande wa mashtaka ulitoa hoja nyingine ya kuongeza shahidi wa pili, ASP Neema na kuibua mvutano mkali wa kisheria uliomlazimu Jaji Grace Mwakipesile anayesikiliza kesi hiyo, kuiahirisha hadi Ijumaa wiki hii atakapotoa uamuzi kama upande wa mashtaka ulikuwa sahihi au la kuwasilisha notisi hiyo mahakamani kabla ya uamuzi wa jana.
Mvutano wa kisheria
Ubishi ulianza mapema mahakamani wakati Jaji Mwakipesile alipokuwa akijiandaa kusoma uamuzi wake juu ya maombi ya upande wa mashtaka kuwasilisha notisi ya kuongeza shahidi.
Wakili wa utetezi, Yassin Member alisimama na kumwomba jaji kutokusoma uamuzi wake kwani tayari walikuwa na notisi ya upande wa mashtaka ya kuongeza ushahidi wakati ni kinyume cha sheria.
Member alilalamika kuwa upande wa mashtaka uliomba kuongeza shahidi mmoja lakini notisi ilionyesha walikuwa wanataka kuongeza mashahidi wawili.
“Mheshimiwa tunaomba usisome kwani tunashangaa tayari tumepewa notisi ya upande wa mashtaka wakati ukiwa bado hata hujatoa uamuzi wa maombi yao ya kuwasilisha notisi ya kuongeza shahidi. Kibaya zaidi wanataka kuongeza mashahidi wawili na siyo mmoja,” alisema Member.
Jaji Mwakipesile alijibu kwa kutaka upande wa utetezi kuipa nafasi mahakama kutoa uamuzi wake wa maombi ya upande wa mashtaka yaliyosababisha kesi hiyo kuahirishwa juzi.
Advertisement
“Ipe nafasi Mahakama kutoa uamuzi wake wa ombi la upande wa mashtaka la kuahirisha kesi ili waweze ku-file notice (kuwasilisha taarifa) ya additional witness (shahidi wa nyongeza), jambo ambalo ninyi mlipinga,’’ alisema Jaji Mwakipesile na kisha kutoa uamuzi wake na kukubali upande wa mashtaka kuongeza shahidi.
Uamuzi huo ulisababisha mvutano mkali mawakili wa utetezi wakisema haikuwa sahihi kwa upande wa mashtaka kuongeza mashahidi wakati ulishindwa kwenye Mahakama za chini wakati wa usikilizwaji wa mwanzo.
Wakili wa utetezi, Evod Mmanda alisema haikuwa sahihi kwa upande wa mashtaka kuwasilisha taarifa hiyo mahakamani hata kabla ya uamuzi wa Mahakama.
“Mheshimiwa Jaji, Prosecution (upande wa mashtaka) waliomba jana ahirisho ili waweze ku- file (kuwasilisha) hicho walichokiomba (taarifa ya kumwongeza shahidi), ruhusa umeitoa leo kwenye uamuzi wako, hivyo walitakiwa wa-file notice yao hiyo baada ya uamuzi wako (wa leo),” alisema na kuongeza:
“Hivyo hakuna notisi halali hapa mahakamani. Notisi halali ni ile watakayoiwasilisha baada ya uamuzi wako. Kwa hiyo sisi tunasema kuwa hadi sasa hakuna notisi halali ya kuita mashahidi wa ziada.”
“Kama Mahakama yako itaikubali hii wanayoita notisi, ingawa sisi tunasema siyo notisi halali, basi tunaomba Mahakama yako ione kuwa haikutolewa ‘in a reasonable time’ (wakati mwafaka).”
Pia alidai kuwa hata hiyo taarifa inayodaiwa na upande wa mashtaka kuwasilishwa, walipewa muda mfupi baada ya kuingia mahakamani na kwamba upande wa mashtaka katika maombi yao juzi walimtaja shahidi mmoja, Mamuya, lakini taarifa waliyopewa inawataja mashahidi wawili.
Wakili Mmanda aliiomba Mahakama chini ya Kifungu cha 289 (3) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), iamue kama huo ni wakati mwafaka, kwa kuzingatia vigezo vya mazingira na wakati ambao upande wa mashtaka ulibaini umuhimu wa kuwaongeza mashahidi hao.
“Hawa wanatajwa kuwepo katika mchakato tangu mwanzo. Mamuya anakiri kupokea kifurishi (bahasha yenye vielelezo) Juni 16, 2011, hadi leo ni miaka miwili na miezi mitatu imepita. Hivyo walijua uwepo wa Mamuya mapema. Huu si wakati mwafaka,’’ alisema Wakili Mmanda.
Hata hivyo, alisema hawana maelezo ya maandishi ya Mamuya wala ya ASP Neema huku akidai kuwa maelezo ya ASP Neema yanaonyesha kuwa yameandikwa Juni 11, mwaka huu wakati hatua ya maelezo ya kesi ilishakamilika.
Hoja hizo za Wakili Mmanda ziliungwa mkono na Wakili mwingine wa utetezi, Jamhuri Johnson ambaye pia alidai hadi wakati huo alikuwa hajaona taarifa ya upande wa mashtaka kuongeza mashahidi.
Akijibu hoja hizo, Wakili wa Serikali, Prosper Mwangamila alidai kuwa katika kesi zote za jinai si jukumu la upande wa mashtaka kuwapatia upande wa utetezi nyaraka mbalimbali wanazokusudia kuzitumia katika kesi, bali Mahakama.
“Notisi wanayoitaja iko mahakamani tangu jana, hivyo utaratibu uliotumika wao kupata nyaraka nyingine ndiyo unaotumika kuwapatia notisi hii. Hivyo hoja ya upande wa mashtaka kuchelewa kuwa ‘serve’ (kuwapatia) haina msingi,” alisema Wakili Mwangamila.
Alisema taarifa hiyo iko mahakamani kisheria kwa mujibu wa Kifungu cha 289 (1) na (2) cha CPA na kuiomba mahakama ione kuwa imewasilishwa katika muda mwafaka.
Alisema endapo itaona kuwa haikuwasilishwa kwa muda mwafaka, kinachopaswa kufanyika si kuiondoa, bali kuwapa muda zaidi upande wa utetezi ili kuipitia.
Baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Jaji Mwakipesile aliahirisha kesi hiyo hadi keshokutwa, Ijumaa, atakapotoa uamuzi wake.
Washtakiwa wawavaa waandishi
Washtakiwa wa kesi hiyo jana walizua patashika wakati waandishi wa habari walipokuwa wakipiga picha mahakamani hapo.
Mshtakiwa wa nane katika kesi hiyo, Mzome alianza kuwa mkali ndani ya Ukumbi wa Mahakama alipotaka kwenda kuwavamia wapigapicha hao. Washtakiwa wenzake nao walicharuka wakizuia kupigwa picha jambo lililowalazimu askari wa Magereza kuwadhibiti na kisha kuwafunga pingu.
Muda mwingi, washtakiwa katika namna ya kukwepa kupigwa picha walificha nyuso zao kwa vitabu huku wanawake wakijifunika kwa mitandio. Source : Mawakili watoana jasho kesi ya dawa za kulevya | Mwananchi
 
Kauli alizowahi kuzitoa Mh. Jaji Mustapher Mohamed Siyani kusisitiza haki na weledi ili Mahakama zijijengee imani kwa umma mpana.

Jaji Mfawidhi M.M. Siyani asisitiza mahakimu wafawidhi kusikiliza mashauri kwa kuzingatia weledi na kutenda haki ili wasiathiri Imani ya wananchi kwa Mhimili wa Mahakama.
Jaji Mfawidhi Mustapher Mohames Siyani alisema Mahakama haiwezi kujitenga na mchakato wa kidemokrasia wa nchi yetu,hivyo ushiriki wa muhimili uko katika hatua zote ikiwemo kabla ya kuanza kwa uchaguzi na hata baada ya matokeo kutangazwa.

Jumatatu, 31 Agosti 2020​

MASHAURI YA UCHAGUZI YASIATHIRI IMANI YA WANANCHI KWA MAHAKAMA – JAJI SIYANI​

Na Innocent Kansha – Mahakama Dodoma.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dodoma Mhe. Mustapher Siyani amewataka Mahakimu Wakazi Wafawidhi wa Mahakama ya Tanzania kusikiliza mashauri uchaguzi kwa kuzingatia weledi na kutenda haki ili wasiathiri Imani ya wananchi kwa Mhimili wa Mahakama.

Akifungua awamu ya tatu ya mafunzo ya namna bora ya uendeshaji wa Mashauri ya uchanguzi kwa Waheshimiwa Mahakimu Wakazi Wafawidhi wa Mahakama za Hakimu Mkazi Tanzania, Jaji Siyani amewataka Mahakimu hao wafawidhi kusimamia masjala kwa karibu zaidi, ili mashauri yanayofunguliwa yaweze kushughulikiwa ndani ya muda stahiki.

Jaji Mfawidhi aliwakumbusha Mahakimu hao kutilia mkazo matumizi ya Teknologia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili mashauri yanayofunguliwa kwa njia ya mtandao (E-Filing) yaweze kusikilizwa na kumalizika kwa wakati.

“Mafunzo haya ni muhimu kwenu binafsi na Mahakama kama taasisi, umuhimu wake hauelezeki kwa maneno mepesi, kwa wale ambao wamewahi kusikiliza mashauri ya uchaguzi wanaelewa nini ninachozungumzia hapa”, alisistiza Jaji Siyani.

Alisema, katika kuyashughulikia mashauri yatokanayo na uchaguzi, suala la muda ni jambo la muhimu kwani viongozi wa ngazi za juu wa Mahakama pia wameelekeza mashauri hayo kutodumu Mahakamani kwa zaidi ya miezi minne tu na si vinginevyo, hivyo amewataka Mahakimu hao kujiandaa kutekeleza majukumu maelekezo hayo muhimu.

Jaji Mfawidhi alisema Mahakama haiwezi kujitenga na mchakato wa kidemokrasia wa nchi yetu,hivyo ushiriki wa muhimili uko katika hatua zote ikiwemo kabla ya kuanza kwa uchaguzi na hata baada ya matokeo kutangazwa. Aliongeza kuwa Ibara ya 107 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka dhahiri kuwa Mahakama ndicho chombo chenye kauli ya mwisho katika kutoa haki. Source : MASHAURI YA UCHAGUZI YASIATHIRI IMANI YA WANANCHI KWA MAHAKAMA – JAJI SIYANI
 
Waandishi wa habari mahiri wa kuripoti yanayojiri mahakamani wajipange kupata nafasi ndani ya Mahakama ili waweze kuripoti mwenendo mzima wa kesi hii ya kihistoria Tanzania.
 
Back
Top Bottom