Jaji Mustapha Mohamed Siyani aliyekabidhiwa kesi ya Ugaidi ya Mbowe ni nani?

Jaji Mustapha Mohamed Siyani aliyekabidhiwa kesi ya Ugaidi ya Mbowe ni nani?

10 September 2021

Mahabusu na wafungwa wamuelezea Jaji M.M. Siyani

Source: Mubashara Studio

Tabia ya CHADEMA ya kuwasemasema vibaya mahakimu na majaji ina gharama zake. Hao mahakimu na majaji sio artificial intelligence; ni binadamu wenye feelings kama binadamu wengine. Endeleeni; mtakipata mnachokitafuta!
 
Huyo nae hakukabidhi ubongo kwa mwendazake kweli?
View attachment 1929663
1631256712944.png

2878995_images_9.jpeg
 
Kwa ufupi sana Jaji huyu Mustapha Mohamed Siyani aliapishwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu kanda ya Dodoma siku ya Ijumaa tarehe 20 April 2018, na Aliyekuwa Rais wa Tanzania wa awamu ya 5 Dr John Magufuli, Baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo tarehe 15 April 2018 .

Pia amewahi kuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma.

NOTE : Jaji wa Mahakama Kuu ni mtumishi wa Umma, kumfahamu haijawahi kuwa kosa kisheria

mmeanza WANGA
 
Ni Jaji wa Mahakama Kuu ambaye anaenda kufanya finishing ya kesi ya Mbowe na wenzie.

Hakika Nimefurahi sana nchi hii inaongozwa kwa sheria, haki na usawa.
Hongera kwa Chadema mmepewa chaguo lenu huyo sasa tusisikie kelele haki ikitendeka na kusimamiwa na Jaji Siyani.
 
Tatizo sio judge kwamba ni muadilifu au sio, tatizo ni mfumo unatumika kumchagua na kumuapisha huyo judge..mfumo ndio root of all evil...huyu na aliepita wote wamechaguliwa na mfumo ule ule....as a person anaweza akawa mtu muadilifu kweli anaependa haki na kuona haki inatendeka...but kwa mfumo ulipo sasa na kwa uzito wa case kama hii....the only way forward ni mfumo mpya utakaoletwa na katiba mpya..
Tusaidie jaji anateuliwa vipi?
 
Kwanini majaji wa Tanzania wanavaa kama majaji wa enzi za ukoloni? Sasa utakuta USA jaji anavaa suti tu.

Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
Siyo kweli mzee; majaji wa Marekani wanavaa majoho pia. Kila nchi ina staili ya majoho ya majaji wake kama ambavyo kila shule ina uniforms zake tofauti na kwingineko
1631261276277.png
 
Majaji wote walioteuliwa na marehemu siyo wa kuwaamini. Labda jaji kama alikuwa anafanya matendo anayotaka marehemu ili ateuliwe kuwa jaji.

Marehemu hakuwahi kumpenda mtu anayependa haki. Kigezo chake kikuu kwa uteuzi wowote, ni mteuliwa kumsujudia yeye na kumkubalia yeye kwa kila jambo hata kama jambo hilo ni hovyo kiasi gani.
Acha ujinga hakuna rais anamchagua mtu bila kwanza kujua ni mtiifu kwake. Upende usipende hakuna rais aliyependa haki nchi hii kuondoa nyerere kama magufuli. Alipenda haki tofauti na marais wengine aliwadhibiti kisawasawa fisadi na adui wa haki wote. Ndio wale waliyoonyesha furaha alipoaga dunia.
 
uongo utakusaidia nini ? mpenda haki anawezaje kula hela ya tetemeko ?
 
Tabia ya CHADEMA ya kuwasemasema vibaya mahakimu na majaji ina gharama zake. Hao mahakimu na majaji sio artificial intelligence; ni binadamu wenye feelings kama binadamu wengine. Endeleeni; mtakipata mnachokitafuta!

Majaji wa Tanzania huteuliwa kwa usiri mkubwa bila uwazi. Hivyo ni jambo jema wananchi na vyombo vya media, asasi za kiraia, na wadau mbalimbali kuanza kuwajadili baada ya uteuzi maana kabla ya teuzi wananchi au chombo kingine huru hakihusishwi wala zoezi kuwa la wazi ili raia kuwajua wateuliwa wa nafasi hizi za kutoa hukumu. Mfano nchi za Marekani na Kenya kwa kutaja kwa uchache huwajadili mienendo ya majaji

.................................................................

Mfano:

Nairobi, Kenya

h-2-875x500.jpg

  • Apr 15, 2019

Majaji 14 Motoni Akiwamo David Maraga​

Na RICHARD MUNGUTI
CHUMA ki motoni kwa majaji 14 wa Mahakama ya Juu na Mahakama Kuu ambao huenda wakatimuliwa kazini kwa madai ya ufisadi na ukiukaji wa maadili ya kazi.

Wakipatikana na hatia, majaji hawa hawatakuwa na budi ila kufurushwa kazini kwa kuletea Idara ya Mahakama fedheha.
Kesi dhidi ya majaji hawa zinaendelea kusikizwa na majopo mawili ya Tume ya Kuajiri Watumishi Idara ya Mahakama (JSC).

Majopo haya yanaendelea kupokea ushahidi dhidi ya majaji hao katika Mahakama ya Juu na Jengo la Kenya R, Nairobi.

Majaji walioshtakiwa katika JSC wanawajumuisha majaji watano wa Mahakama ya Juu na majaji wanane wa Mahakama Kuu.

Walioshtakiwa ni Jaji Mkuu David Maraga, Jaji Mohammed Ibrahim, Jaji Smokin Wanjala, Jaji Njoki Ndung’u na Jaji Jackton Ojwang ambaye wiki iliyopita alisimamishwa kazi na Rais Uhuru Kenyatta.

Mwingine aliyewatangulia hawa ni naibu wa Jaji Mkuu Philomena Mwilu. Kusimamishwa kazi kwa Jaji Ojwang kumeyumbisha utendakazi katika mahakama hiyo ya upeo.

Rais Kenyatta aliteua jopo lenye wanachama watano kuamua hatma ya Jaji Ojwang. Mwenyekiti wa jopo hilo ni Jaji Alnashir Visram wa Mahakama ya Rufaa.
hh-3-800x439.jpg
Jaji Smokin Wanjala. Picha/ Richard Munguti
Mashtaka dhidi ya CJ Maraga ni kuwa ni mbaguzi, mwenye ukabila na mkaidi wa maadili ya mahakama kwa kuhudhuria mikutano ya kisiasa Kisii na Nyamira.

Pia inadaiwa Jaji Maraga alinukuu uamuzi ambao haukuwa umesomwa wa Wajir katika kesi dhidi ya Gavana wa Laikipia.

Madai dhidi ya Majaji Ibrahim, Wanjala na Ndung’u ni ufisadi na ukiukaji wa maadili ya kazi.
Watatu hawa pamoja na Jaji Ojwang wanadaiwa walipokea hongo na kuidhinisha ushindi wa Gavana wa Wajir Mohamed Abdi Mohamud.

JSC inaombwa na walalamishi zaidi ya 600 kutoka kaunti ya Wajir wawatimue majaji hao watatu kazini kwa kupotoka katika uamuzi kwamba Bw Mohamud anahitimu kuwa Gavana.

Majaji wa mahakama kuu ni Majaji D.K Njagi, Edward Muriithi, Martin Muya, Thripsisa Cherere, Lucy Waithaka na Amin Farah. Wengine ni Richard Mwongo na James Wakiaga.

Baadhi ya malalamishi ambayo JSC imepokea ni pamoja na kucheleweshwa kutolewa kwa maamuzi, mapendeleo na muinguliano wa kimaslahi.
Majaji hawa wameandikia JSC na kueleza watawaita baadhi ya majaji wenzao kuwa mashahidi wao na walalamishi waliowasilisha kesi dhidi yao kujitetea wakiwekwa vizimbani.

JSC linaloongozwa na naibu wa mwenyekiti Mercy Deche linaendeleza vikao vyake katika Jengo la Kenya-Re.
Source : Majaji 14 motoni akiwamo David Maraga – Taifa Leo
 
1631273436690.pnghttps://taifaleo.nation.co.ke › ...
JSC kuamua majaji 11 wanaofaa kwa Mahakama ya Rufaa
30 Jun 2019 — Jaji Maureen Onyango, msimamizi wa mahakama ya kutatua mizozo ya waajiri na wafanyakazi alisema

bb-16-875x500.jpg

  • Jun 30, 2019

JSC Kuamua Majaji 11 Wanaofaa Kwa Mahakama Ya Rufaa​

Na SAM KIPLAGAT
TUME ya Huduma za Mahakama imekamilisha shughuli ya kuhoji majaji wanaotaka kujaza nafasi 11 katika Mahakama ya Rufaa.

Majaji waliofika katika mahojiano hayo walitakiwa kutoa msimamo wao kuhusu masuala tata kama vile uavyaji mimba, haki za mashoga, umri unaofaa kwa vijana kuanza kujihusisha na masuala ya mapenzi na uhalalishaji wa bangi.

Majaji hao walikuwa na kibarua kigumu kufafanua hukumu walizotoa hapo awali.

Tume hiyo ya watu 11 pia ilitaka majaji waliohojiwa kuelezea maoni yao kuhusu ugavi wa mali wanandoa wanapotalikiana na mbinu mbadala za kutatua mizozo nje ya mahakama.

Watu 35 walihojiwa katika mahojiano hayo yaliyodumu kwa wiki mbili na sasa tume hiyo inayoongozwa na Jaji Mkuu David Maraga itakuwa na jukumu la kuhakikisha kuwa majaji 11 watakaoteuliwa wanatoka katika maeneo mbalimbali ya nchi na kuna usawa wa kijinsia.

Jaji Maureen Onyango, msimamizi wa mahakama ya kutatua mizozo ya waajiri na wafanyakazi alisema kuwa amekuwa akitofautiana na Mahakama ya Rufaa inapotoa uamuzi wa kupunguza fidia iliyotolewa na mahakama ya chini bila kutoa sababu.

“Kuna wakati mwingine ambapo ninahisi kutofautiana na Mahakama ya Rufaa haswa inapoamua kupunguza fedha za fidia iliyoagizwa na mahakama ya chini ilipwe bila kutoa sababu ya kufanya hivyo,” akasema.

Jaji Onyango alisema Mahakama ya Rufaa inafaa kuwa na jaji aliye na ufahamu kuhusu mizozo ya wafanyakazi ili kuhakikisha kuwa inatoa maamuzi yanayofaa.

Jaji Pauline Nyamweya, msimamizi wa Mahakama ya Masuala ya Kikatiba, Milimani jijini Nairobi, alikataa pendekezo la kutaka bangi ihalalishwe huku akisema madhara ya bangi ni mengi kuliko faida.
“Hata bangi ikihalalishwa kwa ajili ya matibabu hospitalini?” akauliza Jaji David Majanja mmoja wa wanajopo.

“Bado imepigwa marufuku. Mimi nikiwa jaji naangalia madhara ya muda mrefu ya bangi,” akasema Jaji Nyamweya.

Jaji Jessie Lesiit wa Kitengo cha Jinai katika Mahakama Kuu, alisema ngono miongoni mwa vijana wa umri mdogo inafaa kuhalalishwa kwa sababu watoto wanaojihusisha na mapenzi mapema wana tabia mbaya na wala halifai kuwa kosa.

Jaji Lessit alisema watoto wanaoshtakiwa kwa kushiriki mapenzi na wenzao wanafaa kupewa ushauri nasaha badala ya kukamatwa.

Dkt Imana Laibuta, wakili na mhadhiri aliambia JSC kuwa Wakenya hawafai kukimbia kukumbatia utamaduni wa watu wengine kwa sababu ni maarufu katika nchi nyingine alipoulizwa kuhusu msimamo wake kuhusiana na haki za mashoga.

Hata hivyo, Dkt Laibuta alisema ikiwa sheria itabadilishwa na ushoga kuhalalishwa atahakikisha sheria inatekelezwa kikamilifu.
Wakili Paul Lilan aliambia Tume kwamba madai kuwa Idara ya Mahakama ndiyo inatatiza vita dhidi ya ufisadi hayana mashiko.
Profesa Nixon Sifuna Wanyama, mtaalamu wa sheria ya mazingira, alijimiminia sifa huku akisema kuwa yeye ni msuluhishaji wa utata.

Dkt Kipkoech Chebii, mkuu wa Kitivo cha Sheria katika Chuo cha Moi alisema kuwa atakuwa kiungo muhimu katika Mahakama ya Rufaa haswa katika kesi zinazohusiana na mazingira.
Source : JSC kuamua majaji 11 wanaofaa kwa Mahakama ya Rufaa – Taifa Leo

https://habarileo.co.tz › habari
Samia ateua majaji 28 - Habarileo

12 May 2021 — Iliwataja walioteuliwa kuwa majaji wa Mahakama Kuu ni Katarina Revocati ambaye alikuwa Katibu Tawala ...
 
  • Feb 12, 2021

Majaji Waogopa Kazi Ya Maraga​

Nairobi, Kenya
Na BENSON MATHEKA
MAJAJI wenye tajriba kubwa, wakiwemo wote watano kwenye Mahakama ya Juu, wamekataa kuomba nafasi iliyoachwa na Jaji Mkuu Mstaafu David Maraga.

Wengi walitarajia majina ya majaji Philomena Mwilu, Dkt Smokin Wanjala, Njoki Ndungu, Mohammed Ibrahim na Isaac Lenaola katika orodha ya waliotuma maombi lakini hayakuwemo.

Hali hiyo imeibua mjadala mkubwa nchini, huku baadhi ya wanasheria wakisema kuogopa huko huenda kulitokana na jinsi Bw Maraga alivyoweka viwango vya juu vya utendakazi na kutoelekezwa na serikali, jambo linalookekana kukosekana kwa sasa.

Wanasema majaji hawaamini atakayeteuliwa atakuwa na uhuru unaohitajika kutekeleza majukumu ya wadhifa huo.

Wanasema kwamba, waliyopitia majaji wa Mahakama ya Juu, hasa masaibu ya Naibu Jaji Mkuu Mwilu, hawaamini mchakato wa kumtafuta mrithi wa Bw Maraga aliyestaafu Januari 11 utakuwa huru na haki.

Kulingana na wanasheria, hatua ya Rais Uhuru Kenyatta ya kukataa kuidhinisha uteuzi wa majaji 41 walioteuliwa na JSC mwaka jana akidai maadili yao yalikuwa ya kutiliwa shaka na anayopitia Jaji Mwilu iliwafanya wengi kukataa kutuma maombi.

Rais Kenyatta na maafisa wakuu serikalini wamekuwa wakilaumu majaji kwa kuhujumu serikali hasa wale wa Mahakama ya Juu ambao aliwaita wakora kwa kubatilisha ushindi wake kwenye uchaguzi wa urais wa Novemba 2017.

Kumekuwa na juhudi za kumuondoa Jaji Mwilu ofisini kupitia kesi mahakamani na mbele ya JSC na wadadisi wanasema ingekuwa kupoteza wakati kutuma maombi kwa tume ambayo tayari inasukumwa kumtimua ofisini.

Kulingana na mwanasheria mmoja ambaye hakutaka tutaje jina lake kwa kuwa ni mmoja wa majaji 41 ambao Rais alikataa kuidhinisha, kuna uwezekano majaji wa Mahakama ya Juu waliamua kusimama na Jaji Mwilu.
“Ninajua kwamba majaji wa Mahakama ya Juu hawafurahishwi na kuhangaishwa kwa Naibu Jaji Mkuu Mwilu. Wanaamini madai yote dhidi yake yalilenga kumzuia asiwe Jaji Mkuu,” asema.
Anasema wanasheria wanahisi mchakato huo umeingiliwa na watu wenye ushawishi.
“Mipango ya urithi wa Maraga ilianza kitambo na inachofanya JSC ni mchakato wa uhusiano mwema tu. Hakuna anayeweza kushiriki shughuli analojua mwisho wake umeamuliwa. Ikiwa rais alikataa kuidhinisha uteuzi wa majaji 41, je ataidhinisha mmoja wa aliotaja kuwa wakora kukalia kiti moto cha Jaji Mkuu?” alihoji.

JSC ilisema itakagua maombi ya watu 13 wanaotaka kumrithi Maraga na kuorodhesha watakaohojiwa kwa wadhifa huo.
Mawakili wenye tajiriba pana kama Profesa Makau Mutua na Ahmednassir Abdullahi waliotarajiwa kutuma maombi yao pia hawakufanya hivyo. Kulingana na Profesa Mutua, waliyopitia majaji wakuu wawili waliotangulia yanaonyesha kwamba atakayeshikilia wadhifa huo hatakuwa na uhuru wa kutekeleza majukumu yake.

“Nimeulizwa kwa nini sikutuma ombi la kuwa Jaji Mkuu. Baada ya kutafakari, nilifikia uamuzi kwamba, tajiriba ya majaji wakuu wawili wa hivi punde inavyoonyesha, ni vigumu kuwa Jaji Mkuu huru na mwenye nguvu nchini Kenya,” Profesa Makau alisema kwenye ujumbe kupitia Twitter.

Miongoni mwa waliotuma maombi ni majaji wa Mahakama ya Rufaa William Ouko na Martha Koome,Wakili Fred Ngatia aliyemwakilisha Rais Kenyatta kwenye kesi ya uchaguzi 2017, Majaji wa Mahakama Kuu D.K. Marete, Mathew Nduma Said Juma Chitembwe.

Wengine ni Profesa Otinga Mare, Profesa Moni Wekesa, Alice Jepkoech Yano, Profesa Patricia Mbote, mawakili Philip Murgor, Otondi Ontweka na Brian Matagaro.

Kulingana na msajili mkuu wa mahakama ambaye pia ni katibu wa JSC Anne Amadi, tume itaorodhesha watakaohojiwa ndani ya siku 14.
Source : Majaji waogopa kazi ya Maraga – Taifa Leo
 
10 September 2021
Mahakama Kuu
Divisheni ya makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi
Dar es Salaam, Tanzania

MAHAKAMA KUU DIVISHENI MAALUM KUSIKILIZA KESI YA FREEMAN MBOWE NA WENZIWE 3, MFULULIZO KUANZIA TAREHE 15 SEPTEMBER 2021

Jaji Mustapher Siyani ameanza jukumu lake na kupanga kuanza kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi / ugaidi namba 16 /2021 ya Mbowe na wenzie 3 ambao kwa pamoja wa wakabiliwa na tuhuma za ugaidi kwa mujibu wa upande wa mashtaka wa serikali.

Mahakama hiyo chini ya jaji Mustapher Siyani imekubali pia ombi la upande wa utetezi unaoongozwa na wakili Peter Kibatala kuwa upande wa utetezi una mashahidi wake kadhaa na kuiomba Mahakama Kuu kuwa miongoni mwao mashahidi hao, wapo mashahidi 4 walindwe na Mahakama wasitangazwe anuani zao wala majina yao kwa kuhofia kufuatwa na vyombo vya serikali.

Jaji Mustapher Mohamed Siyani ataanza kusikiliza kesi hiyo kwa mfululizo pasi kusimama kuanzia tarehe 15 September 2021 hadi imalizike.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake wamesomewa maelezo ya awali baada ya kupangiwa Jaji Mpya, katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu “Mahakama ya Mafisadi”.

Mbowe na wenzake wamesomewa maelezo hayo mbele ya Jaji Mpya, Mustapha Siyani baada ya Jaji wa awali, Elinaza Luvanda kujitoa kusikiliza kesi hiyo baada ya kukubaliana na maombi ya washitakiwa hao kwamba ajitoe hawana imani naye.

Miongoni mwa maelezo waliyoyakubali washitakiwa hao baada ya kusomewa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando.

Mashtaka yao ambayo wameyakana, huku wakikubaliana na wasifu wao ikiwemo Majina na kwamba mshitakiwa wa Kwanza, Pili, Tatu waliwahi kuwa Wanajeshi na Makomando, pia walikuwa Kambi ya Jeshi Kuke Ngerengere mkoani Morogoro na wanafahamiana maana wote walikuwa Kikosi Kimoja jeshini

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo namba 16/2021 ni Halfan Bwire Hassan, Adam Kasekwa na Mohammed Abdillah Lingwenya.
 
10 September 2021

JAJI MPYA MH. M.M SIYANI, AKUBALI MAOMBI MAALUM YA MAWAKILI WA MBOWE / KESI KUANZA KUUNGURUMA SEPTEMBA 15

Source : MwanaHALISI TV
 
Majaji wa Tanzania huteuliwa kwa usiri mkubwa bila uwazi. Hivyo ni jambo jema wananchi na vyombo vya media, asasi za kiraia, na wadau mbalimbali kuanza kuwajadili baada ya uteuzi maana kabla ya teuzi wananchi au chombo kingine huru hakihusishwi wala zoezi kuwa la wazi ili raia kuwajua wateuliwa wa nafasi hizi za kutoa hukumu. Mfano nchi za Marekani na Kenya kwa kutaja kwa uchache huwajadili mienendo ya majaji

.................................................................

Mfano:

Nairobi, Kenya

h-2-875x500.jpg

  • Apr 15, 2019

Majaji 14 Motoni Akiwamo David Maraga​

Na RICHARD MUNGUTI
CHUMA ki motoni kwa majaji 14 wa Mahakama ya Juu na Mahakama Kuu ambao huenda wakatimuliwa kazini kwa madai ya ufisadi na ukiukaji wa maadili ya kazi.

Wakipatikana na hatia, majaji hawa hawatakuwa na budi ila kufurushwa kazini kwa kuletea Idara ya Mahakama fedheha.
Kesi dhidi ya majaji hawa zinaendelea kusikizwa na majopo mawili ya Tume ya Kuajiri Watumishi Idara ya Mahakama (JSC).

Majopo haya yanaendelea kupokea ushahidi dhidi ya majaji hao katika Mahakama ya Juu na Jengo la Kenya R, Nairobi.

Majaji walioshtakiwa katika JSC wanawajumuisha majaji watano wa Mahakama ya Juu na majaji wanane wa Mahakama Kuu.

Walioshtakiwa ni Jaji Mkuu David Maraga, Jaji Mohammed Ibrahim, Jaji Smokin Wanjala, Jaji Njoki Ndung’u na Jaji Jackton Ojwang ambaye wiki iliyopita alisimamishwa kazi na Rais Uhuru Kenyatta.

Mwingine aliyewatangulia hawa ni naibu wa Jaji Mkuu Philomena Mwilu. Kusimamishwa kazi kwa Jaji Ojwang kumeyumbisha utendakazi katika mahakama hiyo ya upeo.

Rais Kenyatta aliteua jopo lenye wanachama watano kuamua hatma ya Jaji Ojwang. Mwenyekiti wa jopo hilo ni Jaji Alnashir Visram wa Mahakama ya Rufaa.
hh-3-800x439.jpg
Jaji Smokin Wanjala. Picha/ Richard Munguti
Mashtaka dhidi ya CJ Maraga ni kuwa ni mbaguzi, mwenye ukabila na mkaidi wa maadili ya mahakama kwa kuhudhuria mikutano ya kisiasa Kisii na Nyamira.

Pia inadaiwa Jaji Maraga alinukuu uamuzi ambao haukuwa umesomwa wa Wajir katika kesi dhidi ya Gavana wa Laikipia.

Madai dhidi ya Majaji Ibrahim, Wanjala na Ndung’u ni ufisadi na ukiukaji wa maadili ya kazi.
Watatu hawa pamoja na Jaji Ojwang wanadaiwa walipokea hongo na kuidhinisha ushindi wa Gavana wa Wajir Mohamed Abdi Mohamud.

JSC inaombwa na walalamishi zaidi ya 600 kutoka kaunti ya Wajir wawatimue majaji hao watatu kazini kwa kupotoka katika uamuzi kwamba Bw Mohamud anahitimu kuwa Gavana.

Majaji wa mahakama kuu ni Majaji D.K Njagi, Edward Muriithi, Martin Muya, Thripsisa Cherere, Lucy Waithaka na Amin Farah. Wengine ni Richard Mwongo na James Wakiaga.

Baadhi ya malalamishi ambayo JSC imepokea ni pamoja na kucheleweshwa kutolewa kwa maamuzi, mapendeleo na muinguliano wa kimaslahi.
Majaji hawa wameandikia JSC na kueleza watawaita baadhi ya majaji wenzao kuwa mashahidi wao na walalamishi waliowasilisha kesi dhidi yao kujitetea wakiwekwa vizimbani.

JSC linaloongozwa na naibu wa mwenyekiti Mercy Deche linaendeleza vikao vyake katika Jengo la Kenya-Re.
Source : Majaji 14 motoni akiwamo David Maraga – Taifa Leo

Mijadala yao sio ya aina ya mijadala wanayoendesha CHADEMA!
 
Mijadala yao sio ya aina ya mijadala wanayoendesha CHADEMA!
Walipita huko na ndiyo maana katiba mpya ikapatikana, na siyo mwiko kujadili mwenendo wa jaji pia uteuzi wa majaji upo ktk hali ya uwazi na wanafanyiwa usaili ktk uwazi na umma mpana wanapata nafasi ya uelewa weledi, uzoefu, maadili na muegamio wa jaji upo wapi ktk masuala Kadhaa yenye manufaa kwa jamii kupata haki yao wanayostahili.
 
Uwepo wa mhimili uliojichimbia zaidi kwa mujibu wa katiba ya Tanzania kunatia ukakasi sana:

1. Hawa ni sehemu ya vigogo wanufaika wa lile saga la kutolipa kodi kwa mujibu wa katiba.
2. Hawa hawawajibiki kwa lolote katika maamuzi yao.
3. Hawa ni wateuliwa wa ule mhimili ule wenyewe.

Salama zaidi ya haki kutendeka ilikuwa kwenye kuonyeshwa kwa jitihada za kudai katiba mpya kwa ari zaidi.

Kusikia miito tu kwa masikio yakiwa makavu hakujawahi kuwa uwezekano kwenye dunia yetu.
Katiba haitaondoa matatizo yote. Bado hata tukipata katiba kuna cgamoto zingine, na hazitaepukika. Mfano huko Marekani kunakosifika kuwa na katiba nzuri, bado kuna changamoto za uteuzi wa majaji. Kama kutakuwa na raisi na awe nna chama chake kina maseneta wengi, basi hao masenata watahakikisha uteuzi wa majaji unapita bila shida. Sasa ile koti kuu ya USA ina majority ya majaji (7) ambao ni conservatives. TZ tukisema majaji wapendekezwe na raisi na kuteuliwa na bunge, matatizo yatakuwa palepale. Kama CCM ndiyo majority bungeni, itateua wale wenye mwelekeo wa CCM, na kama upinzani utakuwa na wabunge wengi na raisi pia uteuzi utakuwa ni wa wale wenye mwelekeo wa upinzani. Na hii itakuwa hata kwenye tume mbalimbali. Wajumbe, makamishina, na wakuu wa tume, kamisheni, na bodi mbali mbali watateuliwa na kupata support ya bunge kufuatana na ni nani mwenye majority bungeni.
 
Mahakama hiyo chini ya jaji Mustapher Siyani imekubali pia ombi la upande wa utetezi unaoongozwa na wakili Peter Kibatala kuwa upande wa utetezi una mashahidi wake kadhaa na kuiomba Mahakama Kuu kuwa miongoni mwao mashahidi hao, wapo mashahidi 4 walindwe na Mahakama wasitangazwe anuani zao wala majina yao kwa kuhofia kufuatwa na vyombo vya serikali.

Sheria ya Makosa ya Uhujumu
Uchumi kinachoweka masharti kuhusu ulinzi wa mashahidi yaani witness protection

24 Juni 2016 Makala ya mtandao (online document) parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1468490491-24JUNI,2016.pdf
Mheshimiwa jaji aliitazama sheria ya Uhujumu Uchumi na kukubaliana na upande wa utetezi juu ya ulinzi wa mashahidi hoja ambayo upande wa serikali / mashtaka waliipinga mashahidi kupewa ulinzi.

Nakala ya Mtandaoni

Mheshimiwa Naibu Spika, Ibara ya 11 ya Muswada inapendekeza
marekebisho katika kifungu cha 53(1) cha Sheria ya Makosa ya Uhujumu Uchumi kinachoweka masharti kuhusu ulinzi wa mashahidi yaani witness
protection.

Kwa sasa kifungu hicho kinaelekeza kuwa inapoonekana kuwa kuna uwezekano wa kesi kuingiliwa kwa kutishia kumdhuru shahidi, basi Inspekta Jenerali wa Polisi kwa kushauriana na Mkurugenzi wa Mashtaka waweke utaratibu wa kuhakikisha usalama wa shahidi huyo pamoja na familia yake.

Kwa kuwa sasa hivi Bunge limetunga Sheria ya Usalama wa Watoa Taarifa na Mashahidi, Sura ya 446 yaani Whistleblower and Witness Protection Act, Cap. 446 ambayo inaweka utaratibu unaojitosheleza kuhusu usalama wa mashahidi, Muswada unapendekeza kuwa masharti yanayohusu usalama wa mashahidi yaliyomo katika Sheria ya Usalama wa Watoa Taarifa na Mashahidi, Sura 446 (The Whistleblower and Witness Protection Act, Cap. 446) yatumike pia katika masuala yanayohusiana na usalama wa mashahidi chini ya Sheria ya Uhujumu Uchumi.

Mhesimiwa Naibu Spika, hatua hii itasaidia usalama wa mashahidi wa kesi za makosa ya rushwa na uhujumu uchumi na hivyo kuwezesha mashahidi hao
kutoa ushahidi wao bila woga.

Ikumbukwe kuwa kesi hizi zinahusisha watu wenye fedha na makosa haya yanafanyika kwa kupanga yaani organized crime.

Hivyo, Serikali ina wajibu wa kuhakikisha usalama wa mashahidi hao unatolewa ipasavyo na huu ndio msingi wa marekebisho yanayopendekezwa katika kifungu hicho cha 53.

Mheshmiwa Naibu Spika, Ibara ya 12 ya Muswada inapendekeza kuongeza kifungu kipya cha 59A ili kuweka masharti ya kuzuia sheria zinazohusu ufilisi au maamuzi ya kufilisi kampuni kutumika kwa mali ambayo inachunguzwa chini ya Sheria ya Makosa ya Uhujumu Uchumi. Marekebisho hayo yanalenga kukabili vitendo vya watu au kampuni kujifilisisha pindi uchunguzi unavyoanza dhidi yao na pia kuhakikisha kuwa mali zote zinazohusika na kosa
linalochunguzwa au linaloendelea Mahakamani, inaendelea kuwepo hadi uchunguzi au kesi husika itakapohitimishwa.

Hatua hii itaiwezesha Serikali kutaifisha mali hiyo pindi kesi husika itakapokamilika na ikathibitika kuwa ina uhusiano wa kosa la rushwa na uhujumu uchumi lililothibitishwa Mahakamani.
 
Back
Top Bottom