Jaji Mutungi: Vyama vyote vimefika, isipokuwa kile kimoja kinachojitafuta

hiki kakao kimefanyika lini?
 
chadema waianue ngoma yao juani haraka kabla haijapasuka.

Anaeweza kukusajili anaweza kukufuta, na anaeweza kukuajili kazi anaweza pia kukufukuza kazi.
 
Kama TADEA wangekosekana sidhani kama angesema chochote kuhusu chama fulani kutokuwepo au kujitafuta.
 

If USSR changed, everything can change. Tuendelee kujidanganya kama tumeshakamilisha kila kitu
 
Siku nchi ikipinduliwa,Automatically CCM,itakuwa imepinduliwa
Ni kweli kabisa, hata China kuna wanaofikiria kama wewe kuwa siku China ikipinduliwa Automatically chama cha Mao Tse Tung kitakuwa kimepiduliwa. Hakuna kisichowezekana, lakini ni ngumu kuliko ngamia kupita kwenye tundu la sindano. Kuwaza mawazo kama hayo haina tofauti na kutoa tangazo la msiba wako mwenyewe kabla hujafa. CCM kuna wakati inapata mafua na upele na kusababisha ipige chafya nyingi na kujikuna kusiko kwa kawaida lakini kufa kabisa sio rahisi. Na hii inatokana na mfumo wa ubepari duniani na nchi za kibepari kuanza kudhoofika sana kiuchumi, kijeshi, na kitechnolojia. Sarafu zao zinapoteza maana kila siku, bidhaa zao zinakosa umaarufu sokoni na silaha zao hazina maajabu kwenye uwanja wa vita.

Umasikini umebisha hodi kule Ufaransa, wanafunzi wanakaa chini, shule inavuja, walimu hakuna. Hawa ni watoto wa shule lakini wamefuata principles zote za kuandamana. wamebeba mabango yenye ujumbe wa kero zao. Waandamanaji wetu hapa ni mungiki, hawana bango hata moja, wamebeba viberiti tu na madumu ya petroli

View: https://youtu.be/GC-5TxC6Hbk?si=PLHbrIuYU6uTrMXt
 
Elimu ya hapa na pale
 
Kwenye huo ukumbi likidondoka hata jiwe juu ya bati kuna watu hutajua hata wamepita wapi ,hizi kauli hizi zinawapa watu jeuri sana but wacha waendlee kukaza shingo
 

CCM na CCM B, CCM C, CCM D...!!

Bila Chadema wanapoteza muda tu.
 

Halafu Wazenji wanazidi kutuout number kila siku utafikiri wao ni wengi kama sisi.
 
Sasa vyama vyote ni vya Msajili ina maana yeye ndiye baba na mlezk wa vyama. Sasa ukiwa kama baba ama mlezi unawezaje kusema watoto wangu hawa wamefika ila yule mmoja hajafika kwasababu bado anajitafuta? Kama Mlezi kwanini usimsaidie ili ajipate??
 
Chadema ya sahv imejaa upumbavu mwingi, ni viongozi wasiojitambua, utafikiri sijui watoto? Sijui wanafikiri watabembelezwa? Nafikiri wanategemea siku moja wataingia madarakani kwa njia ya uasi na mapinduzi km walivyojaribu mwaka jana. Sema kwanza wanajipotezea muda, wanamtumia huyu Rais vibaya, siku akiingia mtu km Magufuli anawafutilia mbali km ambavyo kipindi cha Magu hao mambwa walikimbia nchi. Mwisho wa hao nyumbu chadema ni kufutwa usajili, wameharibu vijana wetu hao ni kikundi haramu kifutiliwe mbali.
 
Vyama vilivyopo mbele yako,havina wanachama brother!
Gen Z wako watakuondoa penda usipende
We bwege hakuna chama hakina wanachama vinginevyo visingesajiliwa. Km chadema ina wanachama hai kwanini tone tone? Hiyo michango iko wapi? ACT wana wabunge, ni sehemu ya serikali kule Zanzibar mnajilinganisha na chama kisicho na hata diwani moja au hata mwenyekiti wa kitongoji? Uhai wa chadema unaoneshwa na nini?
 
Vyama vilivyopo mbele yako,havina wanachama brother!
Gen Z wako watakuondoa penda usipende
We bwege hakuna chama hakina wanachama vinginevyo visingesajiliwa. Km chadema ina wanachama hai kwanini tone tone? Hiyo michango iko wapi? ACT wana wabunge, ni sehemu ya serikali kule Zanzibar mnajilinganisha na chama kisicho na hata diwani moja au hata mwenyekiti wa kitongoji? Uhai wa chadema unaoneshwa na nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…