Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 15,835
- 23,776
Kwanini ‘Jaji wa Kimkakati’ Elinaza Luvanda anasikiliza kesi ya Mbowe?
Hana hatia, huenda anatekeleza maagizo toka juu kama ilivyo kwa Msajili /Registrar Simba wa Mahakama kuu amewekwa Kisutu kwa mikakati maalum.
Juzi Jaji Elinaza Luvanda alitupilia mbali pingamizi la awali ambalo lilikuwa limewekwa na mawakili wa upande wa utetezi katika kesi inayomkabili Freeman Mbowe, mwenyekiti wa Chadema.
Uamuzi wa Jaji Luvanda, umesababisha baadhi ya watu kutaka kumjua Luvanda ni nani, na imekuwaje akawa msimamizi wa Mahakama Kuu Division ya Uhujumu Uchumi na Rushwa.
SAUTI KUBWAi imefuatilia na inayo machache ya kueleza kuhusu wasifu wa Jaji Luvanda katika kesi za aina hii – “kesi za kimkakati” zinazofunguliwa na dola.
Kwa kifupi, huyu ndiye Jaji Elinaza Luvanda:
Mwaka 2017, Elinaza Luvanda alikuwa katibu wa Kaimu Jaji Mkuu, Jaji Ferdinand Wambari.
Mwaka 2018, aliteuliwa kuwa mjumbe kwenye Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania hadi Rais John Magufuli alipomteua kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Mwaka 2021, Jaji Luvanda aliwahukumu kifungo cha maisha Shamim Mwasha na mkewe kwa makosa ya mihadarati.
Mwaka 2020, alikuwa miongoni mwa jopo la majaji watatu ambao walikuwa na kesi ya Addo Shaibu dhidi ya Jamhuri kuhusu kupinga uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Adelardus Kilangi.
Mwaka 2021, alikuwa miongoni mwa jopo la majaji watatu waliosikiliza kesi ya Peter Msigwa na Joseph Mbilinyi (Sugu) – kesi ya kikatiba dhidi ya Kamishina Jenerali wa Magereza na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Mwaka 2019, alikuwa miongoni mwa jopo la majaji watatu katika kesi ya Zitto Kabwe dhidi ya Spika Job Ndugai na Mwanasheria Mkuu wa Serikali – kesi ya sakata la CAG Assad kuhojiwa na Kamati ya maadili ya Bunge.
asante hisani Ngurumo
Mwaka 2019, kesi ya madai ya sh.bilioni 10 ya Bernard Membe dhidi ya Musiba, ilianzia kwa Jaji Luvanda kabla hajahamishiwa Mahakama ya Ardhi na hivyo kesi ikapangwa Jaji De Melo.
Mwaka 2020, Jaji Luvanda aliwahukumu Anitha Oswald (mfanyakazi wa PPF Moshi) na Frank Moshi (dereva wa teksi) kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la mihadarati.
Mwaka 2020, Jaji Luvanda alitoa uamuzi wa kutaifisha Tsh.16.7 bilioni kuwa mali ya Serikali baada ya DPP Biswalo Mganga kuwasilisha ombi mahakamani kuwa washitakiwa waliokuwa na kosa la UPATU hawakuwahi kufika mahakamani tangu kesi ilipoanza. Washitakiwa walikuwa ni kampuni ya IMS Marketing Tanzania.
Ukiunganisha matukio haya na hukumu ambazo Jaji Luvanda ametoa, hatua kwa hatua, unaweza kuona kuwa huyu ni “jaji wa kimkakati” ambaye amekuwa anapewa kusikiliza kesi za kimkakati. Sasa anasikiliza kesi nyingine ya kimkakati inayomkabili Mbowe na wenzake watatu.
Wachambuzi na wachunguzi wetu wanaendelea kumulika mwenendo wa kesi hii na Jaji Luvanda.
UPDATES_KESI_YA_MBOWE
Jaji Luvanda anakubali kuwa kweli hati ya mashitaka kwenye kesi Freeman Mbowe na wenzake ni batili ila haoni haja ya kuifuta kesi badala yake anaomba upande wa Jamhuri waende wakairebishe na kuondoa baadhi ya makosa.
Mawakili wa Utetezi wakiongozwa na Peter Kibatala wanakataa wanasema kama hati ya mashitaka ni batili kisheria kesi inapaswa kutupiliwa mbali na sio kuwapa fursa upande wa Jamhuri kwenda kurebisha makosa yao.
Jaji Luvanda anakataa kufuta kesi anaendelea kusisitiza kuwa upande wa Jamhuri waende warekebishe hati ya Mashitaka.
Baada ya Jaji Luvanda kutupilia mbali mapingamizi yote ambayo yaliwekwa na upande wa Utetezi licha ya yeye mwenyewe kukuri kuwa mapingamizi yao yalikuwa halali na hati ya mashitaka ni kweli inamapungufu makubwa ambayo yanaifanya iwe batili.
Mhe. Freeman Mbowe anasimama na kusema hana imani na Jaji Luvanda hivyo anaomba ajitoe kusikiliza kesi hii ili kulinda heshima yake na Heshima ya Mahakama.
Mawakili wa Jamhuri pamoja na Jaji wanatoa macho ka mjusi kabanwa na mlango.
Mahakama ipo kimya kwa muda kama shetani kapita hivi
Baada ya ukimya wa dakika kadhaa Jaji Luvanda anamuomba Wakili kibatala aseme Jambo.
Wakili Kibatala anasimana, anasema upande wa Utetezi hawana chochote cha kuongezea kwa sasa ni swala la Muajiri wake kupata anachokitaka na si vinginevyo.
Kibatala anasema mteja wao bado anaimani na Mahakama ila hana Imani na Jaji na moja ya kanuni za Mahakama inasema katika Mazingira kama haya ni vyema au ni sahihi kwa Mahakama kumsikiliza kwa ufasaha na tija.
Baada ya Kibatala kusema hivyo anakaa chini
Jaji anawauliza Mawakili wa Serikali mnachochote cha kuzungumza.?
Mawakili wa Jamhuri wanasem hapana.
Nb. Uamzi wa Mhe. Mbowe umewashtua sana upande wa Serikali, hawakujua kama itakuwa hivi so hawakujipanga wala muda wa kupokea maelekezo haupo
Mahakama inakuwa kimya kwa muda
Baada ya mvutano wa dakika kadhaa kati Jaji na Mawakili wa Utetezi, Jaji Luvanda anasema uamuzi wa Mhe. Mbowe msingi wake ni swala la hisia/ ramli na katika hili yeye hawezi kujitetea sana.
Jaji Luvanda anasema anaona ni busara yeye akae pembeni aje Jaji Mwingine kusikiliza kesi hii.
Jaji anachukua fursa hii kuwashukuru wote ikiwemo Mawakili wa utetezi na Jamuhuri
Shauri linahairishwa kusubiri kupangiwa Jaji mwingine
Polisi anapiga kelele Coooooooooooort
Jaji anatoka katika ukumbi wa Mahakama na watu wote wanatawanyika.