TANZIA Jaji Projest Rugazia afariki dunia. Kuzikwa Ijumaa Agosti 9, 2019 Kijiji cha Rwamashonga, Kata ya Mugana wilaya ya Missenyi

TANZIA Jaji Projest Rugazia afariki dunia. Kuzikwa Ijumaa Agosti 9, 2019 Kijiji cha Rwamashonga, Kata ya Mugana wilaya ya Missenyi

Manyerere Jackton

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
2,438
Reaction score
4,456
pic+kuzikwa.gif

Tunapokwenda Kanisani naomba tuiombee Roho ya ndugu yetu na rafiki wetu mpendwa Judge Projest Rugazia. Ameaga dunia. Mwenyezi Mungu aitakase Roho yake ampe uzima wa milele. Ni majonzi makubwa sana.

-----
07/08/2019

Mwili wa Jaji Mkuu mstaafu wa nchini Tanzania, Projest Rugazia utazikwa Ijumaa Agosti 9, 2019 katika Kijiji cha Rwamashonga, Kata ya Mugana wilaya ya Missenyi mkoani Kagera.

Jaji Rugazia alifariki dunia alfajiri ya kuamkia Jumapili Agosti 4, 2019 alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa shughuli za mazishi, Charles Gabikwa alisema saa 6.30 mchana mwili wa Jaji Rugazia utatolewa nyumbani kwake Kinondoni kuelekea Kanisa Katoliki la Mtakatifu Peter lililopo Oysterbay.

Gabikwa alisema Ibada itaanza Saa 7 mchana hadi saa 9 mchana na kuanzia saa 9:05 hadi saa 10, zitatolewa salamu za rambirambi.

“Watu watatoa heshima zao za mwisho kanisani baada ya hapo, mwili wa marehemu Jaji Rugazia utapelekwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) na kesho Alhamisi Agosti 8, 2019 utasafirishwa kuelekea kijijini kwao Rwamashonga, Wilayani Missenyi mkoani Kagera.

Amesema Ijumaa Agosti 9, 2019 wakazi wa eneo hilo watatoa heshima zao za mwisho na baadaye mwili wake utapumzishwa kwenye nyumba yake ya milele.

Chanzo: Mwananchi
 
Kuna mwenye taarifa zake? Kuna maneno yanasambazwa kwamba hatunaye. Naomba kujuzwa.
Justice Projestuce Rugazia alipokua Hakim Mkuu Mkazi wa Mahakama y Kisutu kapiga watu mvua sana

Mara ya mwisho kumsikia ni miaka kadhaa nyuma alipopata ajali ya gari na kusababisha kifo cha mtu mmoja

Anyways he was bold and tough and sometimes rough too

Kama habari hizi si zakweli Mungu Ampe umri mrefu na afya njema
Kama ni habari za kweli, may his soul rest in eternal peace
 
Justice Projestuce Rugazia alipokua Hakim Mkuu Mkazi wa Mahakama y Kisutu kapiga watu mvua sana

Mara ya mwisho kumsikia ni miaka kadhaa nyuma alipopata ajali ya gari na kusababisha kifo cha mtu mmoja

Anyways he was bold and tough and sometimes rough too
Yes, he was harsh at Kisutu, but I guess within the law!
 
Kama alipokuwa anapiga watu mvua alikuwa anasimamia haki tunamuombea aende pema peponi, lakini kama ni wale wala rushwa kisha kutoa hukumu za uonevu basi atakuwa amechelewa kufa na hiki kifo chake tutamuona ni mzoga kama mizoga mingine.
 
Yes, he was harsh at Kisutu, but I guess within the law!
He was a no nonsense Magistrate, though I keep forcing my brain to believe he was acting within the law atleast in two incidences when he was presiding over the cases of people I happened to know
 
He is dead. I am a family member and we are here Kinondoni after coming from Muhimbili where his unexpected demise occurred!
Duuh pole mkuu....
hv mpaka anafariki bado alikuwa anahudumu kama judge !!?
ama alikwisha stahafu...
 
Back
Top Bottom