Manyerere Jackton
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 2,438
- 4,456
-----
07/08/2019
Mwili wa Jaji Mkuu mstaafu wa nchini Tanzania, Projest Rugazia utazikwa Ijumaa Agosti 9, 2019 katika Kijiji cha Rwamashonga, Kata ya Mugana wilaya ya Missenyi mkoani Kagera.
Jaji Rugazia alifariki dunia alfajiri ya kuamkia Jumapili Agosti 4, 2019 alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa shughuli za mazishi, Charles Gabikwa alisema saa 6.30 mchana mwili wa Jaji Rugazia utatolewa nyumbani kwake Kinondoni kuelekea Kanisa Katoliki la Mtakatifu Peter lililopo Oysterbay.
Gabikwa alisema Ibada itaanza Saa 7 mchana hadi saa 9 mchana na kuanzia saa 9:05 hadi saa 10, zitatolewa salamu za rambirambi.
“Watu watatoa heshima zao za mwisho kanisani baada ya hapo, mwili wa marehemu Jaji Rugazia utapelekwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) na kesho Alhamisi Agosti 8, 2019 utasafirishwa kuelekea kijijini kwao Rwamashonga, Wilayani Missenyi mkoani Kagera.
Amesema Ijumaa Agosti 9, 2019 wakazi wa eneo hilo watatoa heshima zao za mwisho na baadaye mwili wake utapumzishwa kwenye nyumba yake ya milele.
Chanzo: Mwananchi