Goliath mfalamagoha
JF-Expert Member
- Aug 3, 2012
- 602
- 2,506
Muda si mrefu utasikia mamlaka zinasema suala la mkataba wa Jeshi la polisi na kampuni ya Lugumi halitakiwi kujadiliwa na chombo chochote cha habari, kwani kwa mujibu wa sheria ya rushwa namba kumi na moja ya mwaka 2007, jambo lolote ambalo lipo mezani kwa Takukuru likisubiri kufikishwa kwa DPP halitatakiwa kujadiliwa ili kuepusha kuvuruga uchunguzi, na pia kwa mujibu wa sheria ya usalama wa taifa ya mwaka 1970, jambo lolote linalohusiasa na masuala ya kijeshi hayatajadiliwa hadharani ili kulinda usalama wa taifa, tarajia sakata hili kuzimwa muda wowote kuanzia sasa.
Rejea sakata la kashfa ya Meremeta, lilizimwa mpaka bungeni, kila aliyetaka kulichokonoa aliambiwa, wee usihusishe majeshi kwenye jambo lolote kwani utahatarisha usalama wa nchi. Kwa bahati mbaya maslahi ya Umma hutafsiriwa na mamlaka na siyo Umma. Naona dalili za sheria hizi mbili kulizima sakata la kashfa ya Jeshi la polisi na kampuni ya Lugumi muda wowote kuanzia sasa.