Jaji Rwegasira: Nimeagizwa na ngazi ya juu kuulinda mkataba wa LUGUMI

Jaji Rwegasira: Nimeagizwa na ngazi ya juu kuulinda mkataba wa LUGUMI

Muda si mrefu utasikia mamlaka zinasema suala la mkataba wa Jeshi la polisi na kampuni ya Lugumi halitakiwi kujadiliwa na chombo chochote cha habari, kwani kwa mujibu wa sheria ya rushwa namba kumi na moja ya mwaka 2007, jambo lolote ambalo lipo mezani kwa Takukuru likisubiri kufikishwa kwa DPP halitatakiwa kujadiliwa ili kuepusha kuvuruga uchunguzi, na pia kwa mujibu wa sheria ya usalama wa taifa ya mwaka 1970, jambo lolote linalohusiasa na masuala ya kijeshi hayatajadiliwa hadharani ili kulinda usalama wa taifa, tarajia sakata hili kuzimwa muda wowote kuanzia sasa.

Rejea sakata la kashfa ya Meremeta, lilizimwa mpaka bungeni, kila aliyetaka kulichokonoa aliambiwa, wee usihusishe majeshi kwenye jambo lolote kwani utahatarisha usalama wa nchi. Kwa bahati mbaya maslahi ya Umma hutafsiriwa na mamlaka na siyo Umma. Naona dalili za sheria hizi mbili kulizima sakata la kashfa ya Jeshi la polisi na kampuni ya Lugumi muda wowote kuanzia sasa.
 
Lugumi....imekuwa maarufu week 2 hizi! Haya bana mnatuona sisi mamburula mnaeuza geuza story! Nadhani jipu lipo sehemu mbaya hata mpwawe...atatumbuka!
 
Kwenye eneo la majeshi ni ngumu sana kutumbua majipu ndiyo maana hata CAG huwa hakagui sana kwenye eneo hilo na hasa JWTZ
Kama majeshi hayakaguliwi basi wasitumie fedha za wananchi wajitafutie fedha zao wenyewe. Huko ndio watu wanajichulia fedha wanavyopenda
 
we kwel mgogo,huna akili kama wagogo wenzako,kichwan peupe peee,kwahyo ukiambiwa mkataba ndo unajua ni hzo details? Paka kwel wewe,kama unatetea ugal wako jitahd kuwa deep kdogo angalau
Daah umenisikisha sana, sijasema hayo maneno ndo mkataba, na wala sijatetea chochote kwahiyo uache kukurupuka na kutukana watu ovyo.

Nia ya kuandika hayo maneno, ni kuonyesha tatizo lilipo sio mkataba ..!!

Umenikera sana
 
Chonde chonde Magufuli kama unataka kuendelea na nafasi yako ya urais wa nchi hii, achana na mpango wako wa kuanzisha mahakama ya majizi kwani utaingia kwenye mgogoro na chama chako bure kwa kuwa majizi wote hutokea huko. Utakiua chama ama watakufukuza uanachama.
Mkuu hii ni kweli tupu yaani MAJIZI YOOTE NI MADE IN CCM!
 
Katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani jaji Projest Rwegasira ametoa ya moyoni kuhusu mkataba iliyopewa Lugumi Enterprises Ltd kusambaza vifaa maalum vya kuchukua alama za vidole kwenye vituo vyote vya jeshi la polisi nchini mwaka 2011.

Ndugu Rwegasira amesema kuwa ameagizwa na mamlaka ya juu kuuzuia mkataba kati ya Lugumi Enterprises Ltd na jeshi la polisi kwa madai kuwa kuutoa hadharani kwa wasio husika nao ni kukiuka taratibu za jeshi hilo.

Aidha ndugu Rwegasira amesema kuwa watakaoruhusiwa kuuona mkataba huo ni kamati ya bunge yenye mamlaka na jeshi la polisi nchini ambayo ni ya mambo ya nje, ulinzi na usalama na si vinginevyo.

Bila katiba mpya Raisi Magufuli Watamshinda Tu au atawaonea wale ambao hawana Makundi
sasa hapo issue ya Lugumi hata mtoto wa DaRasa la Tatu anajua kuna wizi umefanyika
Hii Nchi kwa sheria zilizopo kama huna Ndugu Kigogo hupati kazi Na ukiwa na kesi Lazima ufungwe
 
People feel happy to write anything about Lugumi since it is the talk of the town,na wanataraji wengi watacomment.
Andika ata source basi mtoa mada maana usije ukawa umelisha maneno jemedali wetu.
 
Tatizo mnaingiza uwongo mwingi na udaku kwenye suala hili mpaka linakosa hata maana nzima au watu wengine wenye fikra pana wanaanza kujiuliza na kuangalia kilichoko nyuma ya suala zima.

Ninaamini habari umeitoa hapa halafu ukaiongezea uwongo na udaku kwa faida ya ajenda zako;

Hivi huwa mnapata faida gani mnapoleta thread zenye hoja za uwongo au udaku?
Njoo tena na lingine!
 
Sawa lakini masuala ya Kampuni ya Lugumi hayana uhusiano wowote wa manunuzi ya silaha au mambo mengine nyeti ya kijeshi, ni project ya kawaida tu hakuna mambo ya usiri au nini sijui.

Wasitake kuficha maovu kwa kisingizio chochote kile vifaa vya biometric, cctv cameras na servers zake nk havina unyeti wowote na haviwezi kuchukua zaidi ya miaka mitano kukamika kufungwa na kuanza kutumika, kuna kitu kimekaa ndio sivyo pale, we kampuni inawezaje kulipwa asilimia 90% wakati kazi ilivyo fanyika so far haizidi asilimia ishirini 20% hii inaingia akilini kweli? Na wala siamini kama Jaji Rwegasira anaweza kutoa kauli tajwa - watu watakua wamemzulia tu.
Unaweza kutuwekea hapa kwa uhakika list ya items zilizo kuwa supplied kwa polisi?
 
Chezeya mtu anaitwa Lugumi weye! ana bulungutu la mabilioni chungu nzima kwenye bank accounts mbali mbali halafu nyuma yake kuna mtu mnene sana nchini ambaye ni UNTOUCHABLE akiguswa tu nchi inaweza kupotea katika uso wa dunia 🙂🙂

Alisema siku anaapishwa kwamba ATATULINDA sasa nashangaa watanzania mnashangaa tunavyolindwa.Tuachieni wenyewe,majipu mengine ya kutumia antbiotics tu
 
20160416_042439.jpg


Maagizo kutoka juu!!!

Hivi huko "juu" huwa ni wapi?!
 
Hivi nyie UKAWA mna nini lakini? mbona mmelishikia bango sana hili suala? Fisadi mko nae CHADEMA na mmemuuzia chama mngaenza na hili kwanza
 
Haya magazeti ya kufungia maandazi bora yapigwe marufuku kwa kupotosha jamii
 
Hivi nyie UKAWA mna nini lakini? mbona mmelishikia bango sana hili suala? Fisadi mko nae CHADEMA na mmemuuzia chama mngaenza na hili kwanza
Mliongea sana na mlimtukana sana sasa dunia inawaumbua mchana kweupeee.
Kila kashfa ni nyie sasa sijui nae ni Lugumi au?
 
Hivi nyie UKAWA mna nini lakini? mbona mmelishikia bango sana hili suala? Fisadi mko nae CHADEMA na mmemuuzia chama mngaenza na hili kwanza
Kwa hiyo wewe unaona ni sahihi bilioni 5 kama inavyoripotiwa kama ni kweli kutumika kama malipo ya mafunzo ya watu watano?
 
Back
Top Bottom