Jaji Warioba aishangaa Tume ya Uchaguzi kwa kitendo cha kuengua Wagombea wa Vyama mbalimbali vya upinzani bila kufuata utaratibu

Jaji Warioba aishangaa Tume ya Uchaguzi kwa kitendo cha kuengua Wagombea wa Vyama mbalimbali vya upinzani bila kufuata utaratibu

Jaji Joseph Sinde Warioba ameishangaa tume ya uchaguzi ya Tanzania kwa kitendo chake cha kuengua wagombea wa vyama mbalimbali vya upinzani bila kufwata utaratibu...
Kikwete alimdhulumu sana huyu mzee, Kikwete alaaniwe
 
Lkn bora huyu aliyesema kuliko wale walio Kimyaa
 
Anaongelea Mambo ambayo hayawezi badilika yameshatokea.ongea kuhusu covid 19, na Ndugai acha unafiki babu.ongea kuachiwa waliokamatwa Kama kule liwale wakati na baada ya uchafuzi
Hayawezi kubadilika kivipi, kwani huu Uchaguzi ni wa mwisho,kwani Rais Magufuli ni wa milele, kwani Tanzania ndio inaisha baada ya huu utawala....Mzee ameongea maneno ambayo yataishi vizazi na vizazi..hajawaza tumbo lake amewaza hatma ya Taifa letu.
 
  • Thanks
Reactions: bne
Mbona sikunyingi anapenda kuona haki inatendeka
Jaji Joseph Sinde Warioba ameishangaa tume ya uchaguzi ya Tanzania kwa kitendo chake cha kuengua wagombea wa vyama mbalimbali vya upinzani bila kufwata utaratibu...
 
Kila mtu anaishangaa tume sio Warioba pekw yake, labda mazuzu tu ndio wanaoweza kuona sawa lakini wenye akili timamu wanajiuliza hawa viongozi wa tume wana akili gani maana mambo wanayofanya hata mtu wa la saba b hawezi kufanta
Kati ya vitu vinavyonifanya nimwone Mahera ni takataka isiyostahili hata kuhifadhiwa kwenye shimo la takataka ni namna alivyouharibu uchaguzi wa mwaka huu.

Siku ambayo nchi yetu itapata uongozi mzuri, uongozi unaosimamia haki kwa mujibu wa katiba, Mahera hataonekana mahali popote katika serikali au taasisi, panapohitaji mtu mwenye akili na aliye genuine.
 
Jaji Joseph Sinde Warioba ameishangaa tume ya uchaguzi ya Tanzania kwa kitendo chake cha kuengua wagombea wa vyama mbalimbali vya upinzani bila kufwata utaratibu....
Atajibiwa na Ngudai, mwenyekiti wa kamati ya roho mbaya inayosimamia sheria, haki na utawala mbovu.
 
Hana lolote yalipokuwa yanatendeka sialikuwepo? kwanini hakusema ili kuzuia anasema Leo ikiwa athari zimekuwa kubwa

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
Sio kwamba hakutaka kusema mkuu, ila wakati huo angesemea wapi? Ni dhahiri mazingira yote ya habari kwa sasa hapa Tanzania tunayajua.

Kwa hiyo bora hata huyu alipopata nafasi kaamua kusema ukweli kuliko na yeye angeongea kama ambavyo wangefanya wenzie.

Kwa hili mimi binafsi nampongeza mzee Sinde Warioba.
 
Hata mimi kwa hili nimemsifu kwani Kwasasa kuikosoa Serikali ya mungu mtu inahitaji roho ngumu Kama ya paka
 
Alikuwa na nafasi ya kuzungumza hilo hata kabla ya uteuzi wa uchaguzi lakini hakufanya hivyo.Nadhani kuna wakati kukaa kimya ni bora zaidi.It is too late,uchaguzi umepita,walioshinda wameapishwa,tume imeshatoa tathmini ya uchaguzi na changamoto zilizotokea na bahati mbaya uenguaji wa wagombea wengi kwao haikuwa changamoto.
Nchi ni yakijani na "magunzi hakuna"radio itanguruma!!
 
Jaji Joseph Sinde Warioba ameishangaa tume ya uchaguzi ya Tanzania kwa kitendo chake cha kuengua wagombea wa vyama mbalimbali vya upinzani bila kufwata utaratibu.

Ameishangaa kuengua wagombea wa vyama mbalimbali bila kuzingatia katiba badala yake kutumia vigezo dhaifu ktk kumuengua mgombea.

Ameishauri tume kufwata utaratibu mpya badala utaratibu huu Usiokua wa haki.

Pamoja na hayo ameshangaa kuona viongozi wa kisiasa wanashindwa kukaa pamoja kwa ajili ya Taifa badala yake wametanguliza ubinafsi, tamaa ya madaraka na itikadi.

Amewashauri kuachana na itikadi za vyama vyao badala yake waliangalie Taifa.

Ameyasema hayo ktk maadhimisho ya haki za Binadamu Duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Huyu ni Kiongozi wa kwanza mstaafu ambae ameishaanza kuona madhaifu yetu kama nchi ambayo yanaweza kutupeleka kubaya kama nchi na hivyo kutoa tahadhari.

Amevunja ukimya na kujionesha utofauti wake na wengine ambao ni wazalendo maslahi ambao kazi yao kubwa ni kusifu na kuabudu ili kulinda matumbo yao na familia zao.
Too little too late!
 
Hayawezi kubadilika kivipi, kwani huu Uchaguzi ni wa mwisho,kwani Rais Magufuli ni wa milele, kwani Tanzania ndio inaisha baada ya huu utawala....Mzee ameongea maneno ambayo yataishi vizazi na vizazi..hajawaza tumbo lake amewaza hatma ya Taifa letu.
Maneno yanasaidia nini?...chaguzi zipo hawataongea mpaka uchaguzi upite so maneno yao ni useless

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Kati ya vitu vinavyonifanya nimwone Mahera ni takataka isiyostahili hata kuhifadhiwa kwenye shimo la takataka ni namna alivyouharibu uchaguzi wa mwaka huu.

Siku ambayo nchi yetu itapata uongozi mzuri, uongozi unaosimamia haki kwa mujibu wa katiba, Mahera hataonekana mahali popote katika serikali au taasisi, panapohitaji mtu mwenye akili na aliye genuine.
Mkuu, kuna mambo yanashangaza sana kwenye hii nchi kiasi kwamba yanatia aibu
 
CCM wanafikiri watanzania na Dunia nzima hawajui uhuni walioufanya kwenye uchaguzi mkuu, Hongera Jaji ukweli umekuweka huru ingawa wana CCM wenzako hawatapenda kauli hii.
 
Kwa kweli kila mwenye uchungu na Taifa letu lazima aguswe na kilichotokea katika Uchaguzi Mkuu!
 
Asili ya huyu Mzee ni Mkweli,huko chamani na serikalini ama katika ngazi ya jamii wasema kweli wamekuwa adimu mno na uongo/propaganda ndiyo Sera ili tule na kusaza.
Waasisi wa Taifa hili wangekuwa tamaa kama sisi leo Mwingereza/mkoloni mweupe angekuwa bado yupo.Je,wangepata fursa ya Kuja kutuona hata Mangungo angekanusha kutufahamu.
Sisi Watanzania wa leo ni vibaraka wa mkoloni mweusi mwenzetu anayejitangaza kuwa mzalendo ilhali uzalendo mtu yeyote hajipitii mwenyewe,watu wanaona bila kuvaa miwani.
Dawa ya Tanzania ni Katiba ya Wananchi kwa ajili ya Wananchi na siyo vinginevyo.
Wazee wetu mliosomeshwa kwa niaba yetu,mkatumika kuijenga Tanzania yetu msikae kimya huku nchi ikiteketezwa.Misingi yote imeng'olew,kutakuwa na ustawi tena?
 
Back
Top Bottom