Jaji Warioba aishangaa Tume ya Uchaguzi kwa kitendo cha kuengua Wagombea wa Vyama mbalimbali vya upinzani bila kufuata utaratibu

Jaji Warioba aishangaa Tume ya Uchaguzi kwa kitendo cha kuengua Wagombea wa Vyama mbalimbali vya upinzani bila kufuata utaratibu


Jaji Joseph Sinde Warioba ...

Amewashauri kuachana na itikadi za vyama vyao badala yake waliangalie Taifa.

...
Amesema vyema.

Lakini kuna tatizo kubwa la hiyo kauli niliyoinukuu. Ni budi tuelewe maana sahihi ya neno "itikadi". Ni kama vile tunafikiri itikadi ni majina ya vyama; kwamba kuna itikadi ya CCM, CHADEMA, ACT, CUF, n.k. WRONG.

Tofauti za kiitikadi ndio utambulisho wa vyama; ndio msingi wa vyama vya siasa. Ukiondoa itikadi basi hakuna sababu ya kuwa na "vyama vya siasa". Inabidi kiwe kimoja tu. US kuna Republicans wenye itikadi ya mlengo wa kulia na Democrats wenye itikadi ya mlengo wa kushoto. UK kuna Conservatives wenye itikadi ya mlengo wa kulia na Labour wenye itikadi ya mlengo wa kushoto. Pia kuna vyama vingine vinavyocheza kati ya itikadi hizo kuanzia kushoto mwisho (extreme left) hadi Kulia mwisho (extreme right).

Umoja wa kitaifa unatokana na katiba ya nchi inayolazimisha vyama vya siasa kujadiliana kupitia Bunge na Utawala (serikali) na kufikia MUAFAKA wa kiitikadi katika vipaumbele vya maendeleo ya kiuchumi na kijamii vya taifa. Kura za wananchi huwezesha hilo kutokea kupitia chaguzi halali. Bungeni ndipo itikadi na sera mbalimbali ushindanishwa kwa mijadala na taratibu za maamuzi.

Ukiwaambia viongozi wa kisiasa waachane na itikadi zao na kuliangalia taifa ni kama unawataka kuwanyima wananchi fursa ya kuchagua mwelekeo wa uongozi wanaoutaka na kuruhusu utawala wa aina moja tu (totalitarianism) kama ilivyo Korea ya Kaskazini na, kwa kiasi fulani, China, Urusi na madikteta wengine waliojificha.
 
Pamoja na kwamba maji yakimwagika hayazolewi, lakini kauli ya mzee warioba kuhusu madudu ya Tume ya uchaguzi katika uchaguzi uliopita inasitahili Kuungwa Mkono na wazalendo wa kweli wa nchi yetu. Nadhani ni busara tukajadili Hoja badala ya Mtoa hoja.
 
Naona
magoti kasogezewa kazi.
Uraia wake
Ni kweli, Warioba kwa kutoka hadharani na kumkosoa Magufuli hadharani na moja kwa moja kama hivi, wengi wanajiuliza noni kitafuata.

Binafsi najiuliza, hatimaye Warioba kakusanya chembe za ushujaa, na "kujitoa ufahamu" kiasi hicho? Nilishakata tamaa kwamba nchi hii haina wazee wa kuisemea. Lakini ukisoma kitabu cha Mkapa, ni wazi alishaanza kuwa kinyume na Magufuli. Msekwa naye, angalau kaonesha ujasiri wa kusimamia misingi badala ya kujiunga na kwaya ya waimba mapambio ya kumsifu na kumwabudu mfalme.

Sasa Warioba kasema kama ni mbwai na iwe mbwai.

Au kwa sababu Magufuli kafuta upinzani rasmi bungeni na kuwafanya Lema na Lissu waikimbie nchi?

Kwa vyovyote, hiki ni kitendo cha kishujaa. Hongera sana Warioba
 
Anaongelea Mambo ambayo hayawezi badilika yameshatokea.ongea kuhusu covid 19, na Ndugai acha unafiki babu.ongea kuachiwa waliokamatwa Kama kule liwale wakati na baada ya uchafuzi
Angalau ameanza kuongea. Tumhimize aendelee, asiishie hapo
 

Jaji Joseph Sinde Warioba ameishangaa tume ya uchaguzi ya Tanzania kwa kitendo chake cha kuengua wagombea wa vyama mbalimbali vya upinzani bila kufwata utaratibu.

Ameishangaa kuengua wagombea wa vyama mbalimbali bila kuzingatia katiba badala yake kutumia vigezo dhaifu ktk kumuengua mgombea.

Ameishauri tume kufwata utaratibu mpya badala utaratibu huu Usiokua wa haki.

Pamoja na hayo ameshangaa kuona viongozi wa kisiasa wanashindwa kukaa pamoja kwa ajili ya Taifa badala yake wametanguliza ubinafsi, tamaa ya madaraka na itikadi.

Amewashauri kuachana na itikadi za vyama vyao badala yake waliangalie Taifa.

Ameyasema hayo ktk maadhimisho ya haki za Binadamu Duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Huyu ni Kiongozi wa kwanza mstaafu ambae ameishaanza kuona madhaifu yetu kama nchi ambayo yanaweza kutupeleka kubaya kama nchi na hivyo kutoa tahadhari.

Amevunja ukimya na kujionesha utofauti wake na wengine ambao ni wazalendo maslahi ambao kazi yao kubwa ni kusifu na kuabudu ili kulinda matumbo yao na familia zao.
You are putting words in his mouth, he did not say that. Kasema kitu amani kimevunjwa pamoja haki za binadamu shauri ya wapinzani kudai wanachoita haki za binadamu. Katoa mifano ya Libya na Misri na Syria ambako harakati za kudai haki zimevuruga taifa. Kuhusu Tume yetu amesema vigezo hubadilika mara kwa mara kujifunza kwa uzoefu. Pia kasema vyama vya siasa vinatakiwa vijue kuwa wapiga kura wanajuana, ukiwaletea viti maalum toka moshi arusha hawatakuelewa, au ukileta madiwani wa Tarime kutoka Kenya hawatakuelewa. Halafu kasema sheria Zimbabwe, kama uchaguzi wako ni tarehe 28 huwezi kunganganiza upige kura tar 27.
 
Huyu mzee aache unafiki, alikuwa wapi wakati haya mambo yanafanyika? Bure kabisa
 
Hahahhaaa yani upinzani mtazalauriwa na kukejeliwa mpaka lini? 😂😂 yani warioba ndo ameona jana vitendo hivi??
Hii inaonyesha ni jinsi gani mnavyokejeliwa na serikali 😂😂😂
Hongera we kuwa ccm huenda maisha yako ni Bora sana
 
Wewe je hukuliona hilo?
Hahahhaaa yani upinzani mtazalauriwa na kukejeliwa mpaka lini? 😂😂 yani warioba ndo ameona jana vitendo hivi??
Hii inaonyesha ni jinsi gani mnavyokejeliwa na serikali 😂😂😂
 
Waziri mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba ametaja kasoro 4 zilizojitokeza katika uchaguzi mkuu wa 2020.

Jaji Warioba ametaja kasiro hizo wakati akiongea na viongozi wa dini na miongoni mwa kasoro hizo ni:
1. Vyama vya siasa kuwaengua baadhi ya wagombea wanaokubalika kwa wananchi.

2. Tume ya uchaguzi kuwaengua baadhi ya wagombea wa vyama vya upinzani.

3. Tume ya uchaguzi kutokuwa na uwazi nk

Source Eatv habari!
 
Back
Top Bottom