Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 5,122
- 5,104
Amesema vyema.
Jaji Joseph Sinde Warioba ...
Amewashauri kuachana na itikadi za vyama vyao badala yake waliangalie Taifa.
...
Lakini kuna tatizo kubwa la hiyo kauli niliyoinukuu. Ni budi tuelewe maana sahihi ya neno "itikadi". Ni kama vile tunafikiri itikadi ni majina ya vyama; kwamba kuna itikadi ya CCM, CHADEMA, ACT, CUF, n.k. WRONG.
Tofauti za kiitikadi ndio utambulisho wa vyama; ndio msingi wa vyama vya siasa. Ukiondoa itikadi basi hakuna sababu ya kuwa na "vyama vya siasa". Inabidi kiwe kimoja tu. US kuna Republicans wenye itikadi ya mlengo wa kulia na Democrats wenye itikadi ya mlengo wa kushoto. UK kuna Conservatives wenye itikadi ya mlengo wa kulia na Labour wenye itikadi ya mlengo wa kushoto. Pia kuna vyama vingine vinavyocheza kati ya itikadi hizo kuanzia kushoto mwisho (extreme left) hadi Kulia mwisho (extreme right).
Umoja wa kitaifa unatokana na katiba ya nchi inayolazimisha vyama vya siasa kujadiliana kupitia Bunge na Utawala (serikali) na kufikia MUAFAKA wa kiitikadi katika vipaumbele vya maendeleo ya kiuchumi na kijamii vya taifa. Kura za wananchi huwezesha hilo kutokea kupitia chaguzi halali. Bungeni ndipo itikadi na sera mbalimbali ushindanishwa kwa mijadala na taratibu za maamuzi.
Ukiwaambia viongozi wa kisiasa waachane na itikadi zao na kuliangalia taifa ni kama unawataka kuwanyima wananchi fursa ya kuchagua mwelekeo wa uongozi wanaoutaka na kuruhusu utawala wa aina moja tu (totalitarianism) kama ilivyo Korea ya Kaskazini na, kwa kiasi fulani, China, Urusi na madikteta wengine waliojificha.