Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Hiyo ni habari ya leo, au ww leo ndio umeileta humu?Yupo hewani
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hiyo ni habari ya leo, au ww leo ndio umeileta humu?Yupo hewani
Siamini kuwa ni Jaji Warioba huyo huyo aliye bandika hiyo picha ya kichwa kwenye hiyo video.JAJI WARIOBA AZUNGUMZA KUHUSU KUELEKEA UCHAGUZI 2024 / 2025 , HALI YA KISIASA, MFUMO WA HAKI JINAI, KUWEPO MAJESHI MENGI, 4R ...
Yaani nchi nzima hii, kabaki mzee mmoja tu anaye sumbuliwa na hali mbovu kabisa tuliyo nayo kisiasa nchini?Utawala bora yaani mfumo wazi unaoeleweka wa haki na mifumo ya usalama ndiyo huzaa demokrasia, bila utawala bora wa kujua nani anafanya nini, mamlaka yake ni yepi na anawajibika kwa nani basi demokrasia inakuwa haipo ...
04 October 2024
JAJI WARIOBA AZUNGUMZA KUHUSU KUELEKEA UCHAGUZI 2024 / 2025 , HALI YA KISIASA, MFUMO WA HAKI JINAI, KUWEPO MAJESHI MENGI, 4R ...
View: https://m.youtube.com/watch?v=Y5z3HSDrAP4
Jaji Joseph Sinde Warioba anazungumzia uchaguzi unaokuja wa November 2024 TAMISEMI na ule uchaguzi mkuu 2025
Jaji Warioba uchaguzi wa 2019 na 2020 ulikuwa wa kipekee kwa kuwa ulipangwa uwe na dosari nchini nzima tena dosari kubwa za makusudi tofauti na miaka ya 2015 kwenda nyuma hadi 1995 ambapo kulikuwa na dosari ndogo ndogo sehemu chache za nchi.
Baada ya kusema hayo (Jaji Warioba) nataka sasa tuangazie uchaguzi wa serikali za mitaa November 2024 naona kuna taarifa za makusudi kuwakanganya wananchi wasiweze kushiriki kikamilifu uchaguzi wa November 2024.
Elimu inayosemekana inatolewa kwa mpiga kura ni potofu, inachanganya ... mfano serikali ndiyo inasimamia kupitia TAMISEMI uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji ambapo wananchi hawapewi elimu kuwa ili uweze kupiga kura November kuna daftari la mtaani ukajiandikishe ama sivyo hutaweza kushiriki November 2024 kuchagua au kuchaguliwa... hii ni kazi ya Serikali siyo Tume Huru ya Uchaguzi ya Taifa INEC
Tuna wasiwasi yale ya 2019 kuhusu wapiga kura, wagombea na mawakala kuenguliwa, kutoruhusiwa kuingia vituoni, kutoshirikishwa kuhesabu kura pia kushindwa kushirikishwa wakati wa kutangaza matokeo ..
Sheria ya kuwakamata na kuwatia ndani watu, inatumiwa vibaya na wakuu wa wilaya, nakumbuka waziri wa mambo ya ndani ya nchi jenerali Kimaro alipata pressure alitaka kuwatia ndani kina mchungaji Christopher Mtikila waliokuwa wanatofautiana na serikali wakati wa utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi.
Sisi tulikataa na kupiga kelele. Sheria ya DC kutia watu ndani, sheria hiyo bado ipo na watu wanaitafuata sana wanataka waitumie, sasa tunaelekea ktk uchaguzi sheria hiyo kandamizi bado ipo ...
Mtindo wa DC kuongozana na viongozi wa majeshi yote hayo kwa kisingizio cha kuwa mkuu wa Kamati za Ulinzi na Usalama za wilaya, ni kujaribu kuliigiza jeshi la polisi na majeshi mengine mengi ya Tanzania. Pia ni kuwapotezea muda wakuu wa Polisi wa wilaya kushindwa kufanya majukumu yao kwa kuwa wanalazimishwa kuambataba na maDC kila mahali.
Nchi ina majeshi mengi kuanzia Polisi, Misitu, TAKUKURU, UHAMIAJI, MAGERAZA, TISS n.k , Tume ya Haki Jinai imependekeza nchi iwe na jeshi moja tu yaani TPDF / JWTZ na majeshi mengi yavunjwe badala yake yawe Taasisi za Huduma.
Sasa hivi majeshi haya yasiyo TPDF yanakamata, kufunga, kutesa kutokana na muundo wao kuwa wa kijeshi jeshi na kutumika vibaya ... watuhumiwa wakikamatwa hawajulikani wapo wapi na nani kawakamata ...
Utawala bora yaani mfumo wazi unaoeleweka wa haki na mifumo ya usalama ndiyo huzaa demokrasia, bila utawala bora wa kujua nani anafanya nini, mamlaka yake ni yepi na anawajibika kwa nani basi demokrasia inakuwa haipo ...
Wazee wengine wakisema Watoto wao watakosa Teuzi. Si unajua wamesomea BA, International Relation, diplomasia na law? Bila teuzi hawatoboi.Yaani nchi nzima hii, kabaki mzee mmoja tu anaye sumbuliwa na hali mbovu kabisa tuliyo nayo kisiasa nchini?
Wengine wote wako wapi,... akina Mwandosya (hivi bado yu hai?)
Na zile NGOs; hivi wao kazi zao ni zipi hasa; kama siyo kuwaelimisha wananchi kuhusu HAKI zao?
Na hivi vyama vya siasa je? Wao wataanza lini kuwafikia wananchi na angalau kuwaeleza tu sifa zao za kuwa mpiga kura ni zipi, na kuwahimiza wajiandae sasa hivi!
Mbona CCM tayari wanafanya huko huko mitaani na vijijini?
Kama vile mxemaji wa xerikali!! Au chawa mwandamizi... dah!huenda Mzee warioba anapotoshwa, au hana taarifa za uhakika kuhusu zoezi hilo au hahudhurii mikutano inayoitishwa na viongozi wa mtaani kwake kuhusu mambo mbalimbali.
Na kwakua muda wote yeye yupo Dar es salaam, na huu ndio mkoa wa mwisho kwaajili ya kujiandikisha kwenye daftari la mtaa kwaajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa, lakini pia sambamba na hilo kutakua na zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Wataitwa watu wa kila mtaa kuelimishwa juu ya umuhimu wao kujitokeza kujiandikisha kwaajili ya uchaguzi wa mtaa2024, na kuboresha taarifa zao kwaajili ya uchaguzi mkuu 2025🐒
sio kama vile msemaji,Kama vile mxemaji wa xerikali!! Au chawa mwandamizi... dah!
CCM wakifanya inatosha gentleman kwasabb wanafanya kwa wananchi wote 🐒Yaani nchi nzima hii, kabaki mzee mmoja tu anaye sumbuliwa na hali mbovu kabisa tuliyo nayo kisiasa nchini?
Wengine wote wako wapi,... akina Mwandosya (hivi bado yu hai?)
Na zile NGOs; hivi wao kazi zao ni zipi hasa; kama siyo kuwaelimisha wananchi kuhusu HAKI zao?
Na hivi vyama vya siasa je? Wao wataanza lini kuwafikia wananchi na angalau kuwaeleza tu sifa zao za kuwa mpiga kura ni zipi, na kuwahimiza wajiandae sasa hivi!
Mbona CCM tayari wanafanya huko huko mitaani na vijijini?
ndoto za kimweri 🐒Mzee Warioba katika ubora wake.
Ila mapungufu na kasoro hizi zote alizoxitaja hazitaweza kuondoka endapo kama Ccm haitaondoka kwanza madarakani.
Wewe nilisha malizana nawe kitambo, baada ya thamani ya michango yako humu kupotea, na hasa baada ya kujua uhusika wako katika maovu mnayo wafanyia waTanzania.CCM wakifanya inatosha gentleman kwasabb wanafanya kwa wananchi wote 🐒
nimefurahi sana umeacha kuporomosha matusi mazito mazito siku hiziWewe nilisha malizana nawe kitambo, baada ya thamani ya michango yako humu kupotea, na hasa baada ya kujua uhusika wako katika maovu mnayo wafanyia waTanzania.
