Jaji Warioba aomba jengo la Maabara Jumuishi SUA kuitwa Samia, Rais Samia aridhia

Jaji Warioba aomba jengo la Maabara Jumuishi SUA kuitwa Samia, Rais Samia aridhia

My Take
Chadema wataumia sana Kwa hili.

In fact hata Mzumbe wanatakiwa Waite mojawapo ya majengo Yao Jina la Rais Samia kama mwana Alumnai wa Mzumbe.

Rais kama Samia Huwa hawapatikani Kila mahala na Kila mda.

----

RAIS SAMIA ARIDHIA JENGO LA MAABARA JUMUISHI SUA LIITWE KWA JINA LAKE



"Hili jengo liitwe Samia lakini na mimi niwaombe hilo jengo linalomalizika liitwe Chibunda (Prof. Raphael Chibunda, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo- SUA) amefanya kazi nzuri sana hapa ndani"- Rais Samia.

Rais Samia ameyasema hayo baada ya kuzindua jengo la Maabara Jumuishi la Chuo Kikuu Cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kilichopo Manispaa na wilaya ya Morogoro mkoani Morogoro siku ya Jumanne Agosti 06, 2024.
Nchi ya kishamba hii. Kila kitu Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli, Samia.
Kama nchi pia tujifunze kuwa majina ya vitu wakati mwingine ni utalii tosha.
 
nimeshusha vyeo vyote vya warioba. zamani niliamini ndiye mccm pekee mwenye akili. kumbe walewale. gongo ishaharibu akili ya mzee wetu.
 
Mwalimu Nyerere alisema ukipewa ushauri wa kijinga na wewe ukaukubali basi ujue aliyekupa huo ushauri amekuona wewe ni mbumbumbu kuliko mbumbumbu wote.
Maua yako Mkuu
 
Mchango wa Nyerere unaulinganisha na Samia?! Serious kabsa?! Nyerere na Samia?!
Kila Kiongozi ana mchango Kwa nafasi yake na awamu yake.

Ukiniuliza Mimi nitampa Samia credit zaidi Kwa sababu zifuatazo
1.Mapinduzi ya Kilimo
2.Mapinduzi ya Barabara Vijijini
3.Mapinduzi ya sekta ya Afya
4.Mapinduzi sekta ya maji(kumtua mama ndio kichwani)
5.Mapinduzi sekta ya elimu-Mitaal mipya na majengo ya Watoto na Walimu.
6.Maelfu ya Ajira,JK akasome
7.Mapinduzi ya Biashara,

Kimsingi hayo ni machache sana kati ya Mageuzi makubwa aliyofanya Samia Kwa huu mfupi na alama.ambazo hazitafutika.

Huwezi jua Kwa sababu hakuna Cha maana unafuatilia.

Namheshimu na natambua mchango wa Baba wa Taifa.
 
Itachukua muda mwingi sana kumpata Rais kama Samia. Ameipitisha nchi kwenye nyakati ngumu sana na kila kitu kinaenda tena bila watu kuumizwa. Hongera zake.
Mimi napenda lugha yake ya staha. Mama hanaga ubabe usio na maana. anajua ku value watu. Tatizo ni watanzania wengi ni waongo, wasanii na watu wasio waaminifu.
 
Back
Top Bottom