PreGE2025 POTOSHI Jaji Warioba asema CHADEMA kususia uchaguzi ni kujifuta kwenye Ramani ya siasa

PreGE2025 POTOSHI Jaji Warioba asema CHADEMA kususia uchaguzi ni kujifuta kwenye Ramani ya siasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
POTOSHI_WARIOBA_5MEI25.jpg
 
Tunachokijua
Jaji Joseph Sinde Warioba alikuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia Novemba 5, 1985 hadi Novemba 9, 1990. Pia ni Mwanasheria, Mwanasiasa na Jaji maarufu anayeheshimika Kitaifa na Kimataifa kwa mchango wake mkubwa katika masuala ya Sheria na Utawala Bora.

Kadhalika aliwahi kuwa Jaji katika Mahakama ya Kimataifa ya Sheria ya Bahari ya Hamburg, Ujerumani yenye makao yake makuu nchini Ujerumani kuanzia 1996 hadi 1999. Warioba aliongoza Kundi la Waangalizi wa Jumuiya ya Madola katika uchaguzi wa Aprili 2007 Nigeria. Alitoa tathmini chanya ya uchaguzi huo, akiuona kuwa ulikuwa wa maendeleo huku pia akisema kulikuwa na dosari. Kadhalika amekuwa ni moja kati ya viongozi wastaafu ambao hawakubali kukaa kimya dhidi ya ukiukwaji wa taratibu za kidemokrasia na utawala bora, tazama hapa akitoa maoni yake juu ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Mnamo tarehe 03, Mei 2025 chama cha wanasheria Tanganyika (TLS) kiliandaa kongamano la Kitaifa kuhusu uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2025 ambapo Jaji Warioba alikuwa ni miongoni mwa wazungumzaji.

Madai

Kutokana na Kongamano hilo kumekuwapo na taarifa inayosambazwa katika mitandao ya kijamii ikidaiwa kuchapishwa na Millard Ayo kuwa Jaji Warioba alisema CHADEMA kususia uchaguzi ni kujifuta kwenye ramani ya siasa.


Je, ni upi uhalisia wa Taarifa hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia maneno muhimu (Key Word Search) pamoja na Google reverse image search ulibaini kuwa Chapisho hilo halikuchapishwa na Millard Ayo bali likisambazwa na wapotoshaji kwani ni la kutengenezwa.

Aidha kupitia Kongamano la TLS, Jaji Warioba alitumia nafasi hiyo kushauri kuondolewa kwa dosari zilizowahi kutokea wakati wa uchaguzi mwaka 2019, 2020 na 2024 ili kuwawezesha wananchi wote kushiriki uchaguzi wa mwaka 2025 kupitia vyama mbalimbali vya siasa kwani haitakuwa vizuri Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kutokushiriki uchaguzi huo kutaengua ushiriki wa baadhi ya wananchi kupitia chama hicho.

Rejea hapa kuanzia dakika ya 58:38

View: https://www.youtube.com/live/OsDzcv1mgK0?si=OnUniueRhycE5rus&t=3278​
Back
Top Bottom