Pre GE2025 Jaji Warioba: Jeshi la Polisi limeingizwa kwenye Siasa, linatoa matamko ya Kisiasa, liachwe lifanye kazi yake

Pre GE2025 Jaji Warioba: Jeshi la Polisi limeingizwa kwenye Siasa, linatoa matamko ya Kisiasa, liachwe lifanye kazi yake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
warioba alishindwa ubunge akiwa waziri mkuu masuala ya uchaguzi atuache
 
..Nani amewazuia Amiri Jeshi Mkuu, na Igp, kulitoa jeshi la Polisi kwenye siasa?
 
Jeshi la Ulinzi (JWTZ) ndio taasisi pekee yake iliyobaki kwa uadilifu, kwa uzalendo, kwa nidhamu. Tusije tukawaingiza kwenye haya matatizo ya kisiasa, wananchi wakaanza kuwaona nao wanapendelea upande mmoja. Mimi ningeomba kabisa Jeshi la Ulinzi lisije likaingizwa kwenye mambo ya siasa, sio kazi yake, kazi yake ni kulinda usalama wa nchi," ameeleza Jaji Warioba akiongea na waandishi wa habari leo Disemba 04,2024.Na kuongeza:

"Polisi ni chombo muhimu sana, ndicho kinalinda wananchi na mali zao na kinatakiwa kifanye kazi na wananchi wote. Katika miaka michache iliyopita tumeliingiza Jeshi la Polisi katika siasa, linatoa matamko ya kisiasa na hii italeta mgawanyiko, wananchi watagawanyika."
View attachment 3168783
"Lisije kuingizwa kisiasa" aliyemwambia linaingizwa kisiasa nani? kwa hiyo taasisi zote hazina maadili? hebu anukuu hayo matamko ya polisi ya kisiasa. Mchawi anawanga mchana. Ndio mwana chama pekee wa CCM anayeomba chama chake kishindwe. Anaongea kama nani huyu mzee.
 
Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba, amewataka wanajeshi kuepuka kuingilia siasa, akisisitiza kuwa kazi yao ni kulinda usalama wa nchi. Akizungumza na wanahabari Disemba 4, 2024, Warioba alikumbusha historia ya machafuko kutoka nchi jirani na kusema jeshi lilifanikiwa kudhibiti mikoa ya mipakani kama Katavi, Kigoma, na Kagera. Alionya kuwa kuingiza jeshi katika siasa kunaweza kuhatarisha usalama, akitoa mfano wa ufanisi wa jeshi katika vita ya Uganda.

"Tangu Uhuru watu wa Kongo, Burundi, Rwanda wamekuwa na machafuko, wananchi wa huko walikuwa wakikimbilia huku na wengine wakitaka kuendeleza harakati zao kutoka ndani ya nchi yetu, jeshi letu lilidhibiti mikoa mbalimbali hasa ile ya mipakani kuanzia Katavi, Kigoma, Kagera kukawa salama kabisa."

"Mnajua chokochoko iliyotokea Uganda, na mnajua kazi iliyofanywa na jeshi, tulipoteza vijana wengi sana, wale wameapa kuifia nchi na waliifia nchi, tusije tukawaingiza kwenye haya matatizo ya kisiasa, wananchi wakaanza kuwaona nao wanapendelea upande mmoja. Mimi ninaomba kabisa jeshi la ulinzi lisije likaingizwa kwenye mambo ya siasa, siyo kazi yake, kazi yake ni kulinda usalama wa nchi".

JK alishatoa taadhari tena akiwa rais kuwaambia wenzie wasiwategemee kuna siku watawakataa
 
Toka aanze kuongea public matukio ya aina hii..s there any impact recorded??? mwenye mtindio wa akili ndio anasikiliza hizi garbbage, na juha anakimbia kupost hapa!
Beneficiary at work, ujinga ni mzigo!!

Siku UKIBINYWA PUMBU ndo utakuja kuelewa,
 
Mzee wa Walioba ameongea kweli. Lakini naona humu watu wengi mnamjaza mzee uwogo, unafikili yeye hajui kuwa na kuminywa ukiikosea serikali. Mzee yuko real . MUNGU amlinde ndio mzee aliyepaki kulipambania taifa. Wazee wengine wote wamekaa kimya wanakula pension. Tumuombee mzee wetu aendelee na afya njema na ulinzi wa MUNGU uwe juu yake azidi kutema cheche
 
Back
Top Bottom