Pre GE2025 Jaji Warioba: Jeshi la Polisi limeingizwa kwenye Siasa, linatoa matamko ya Kisiasa, liachwe lifanye kazi yake

Pre GE2025 Jaji Warioba: Jeshi la Polisi limeingizwa kwenye Siasa, linatoa matamko ya Kisiasa, liachwe lifanye kazi yake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hivi watu wa CCM mna shida gani yaani kwa maelezo aliyoyatoa mzee mi mpaka mwili ulikuwa unanisisimuka. Kaongea kizalendo sana, tatizo Ccm mnadhani hii nchi ni yenu peke yenu. Hayo mnayoyafanya linaligharimu sana taifa.

Huyu mzee ana akili kubwa sana na hana uoga na kaonyesha uzalendo mkubwa kwa taifa lake tofauti na kina JK kazi yao kuchekacheka tu kijinga wakati wanaona kabisa nchi inapelekwa hovyo.
.."ana akili kubwa sana" ndio shida za kutaka kuongea mbele za watu wakati gongo ya juzi haijatoka kichwani.
 
CHAWA wanamkashifu
Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba, amewataka wanajeshi kuepuka kuingilia siasa, akisisitiza kuwa kazi yao ni kulinda usalama wa nchi. Akizungumza na wanahabari Disemba 4, 2024, Warioba alikumbusha historia ya machafuko kutoka nchi jirani na kusema jeshi lilifanikiwa kudhibiti mikoa ya mipakani kama Katavi, Kigoma, na Kagera. Alionya kuwa kuingiza jeshi katika siasa kunaweza kuhatarisha usalama, akitoa mfano wa ufanisi wa jeshi katika vita ya Uganda.

"Tangu Uhuru watu wa Kongo, Burundi, Rwanda wamekuwa na machafuko, wananchi wa huko walikuwa wakikimbilia huku na wengine wakitaka kuendeleza harakati zao kutoka ndani ya nchi yetu, jeshi letu lilidhibiti mikoa mbalimbali hasa ile ya mipakani kuanzia Katavi, Kigoma, Kagera kukawa salama kabisa."

"Mnajua chokochoko iliyotokea Uganda, na mnajua kazi iliyofanywa na jeshi, tulipoteza vijana wengi sana, wale wameapa kuifia nchi na waliifia nchi, tusije tukawaingiza kwenye haya matatizo ya kisiasa, wananchi wakaanza kuwaona nao wanapendelea upande mmoja. Mimi ninaomba kabisa jeshi la ulinzi lisije likaingizwa kwenye mambo ya siasa, siyo kazi yake, kazi yake ni kulinda usalama wa nchi".

CHAWA wanamkashifu Mzee Warioba kuonyesha hawapo tayari kufanya haki.
 
Kosa ni Wanasiasa kuwalazimisha vyombo vya usalama kuwasaidia kwenye Siasa.
 
mtanzania anakwepa kodi, then analalamika barabara mbovu, huduma za kijamii haziridhishi, HAKUNA HAKI BILA WAJIBU, ushoga huwezi kuona threat now, hii ni mbegu brother inamea taratibu, na inakuja kwa gia hizo hizo za demokrasia,
Kodi inaliwa na wahuni, mafisadi na familia zao labda na wewe kama upo kwenye ulaji. Ufisadi, wizi ujambazi utakuwa mnufaika wa wizi wa kodi za nchi.
 
Huyu alikuwa waziri mkuu kwa Nini asiende kiwashauri viongozi wa Sasa Hadi aongee hadharani au kulikoni. Yeye wakati wake ilikuwaje.
Muhimu kuongela hadharani kupunguza uhuni, utekaji, uenguaji, mauaji.
 
Ukweli mtupu au Tlaatlaah unasemaje

Ova
ni muhimu sana Mzee akawajibika kulea wajukuu zake na akaacha na wengine wakawajibika kulingana na majukumu yao ya kazi.

vinginevyo wanaomtumia huyu mzee wanamuhangaisha na wanamuhadaa kwa fedheha sana..

hata hivyo,
huenda hasira na kinyongo cha kushindwa vibaya uchaguzi kule bunda kipindi kile bado anapata kiwewe na mawenge 🐒
 
Ehh kweli hamna heshima

Ova
 
Ehh kweli hamna heshima

Ova
nadhani hilo la kila moja kuheshimu wajibu wake ni muhimu zaidi.

wazee waheshimu wajibu wao wa kulea na kucheza na wajukuu nyumbani..

na vijana hodari wachape kazi kwa bidii kujenga na kulinda Taifa

nadhani hilo ni la maana sana 🐒
 
M
demokrasia ya kazi gani?, CHINA wamepiga hatua kimaendeleo kwa kufuata misingi ya demokrasia za magharibi?, FIKIRI NJE YA BOX, usikariri,
kuu twende huko nje ya BOX,hivi huko Korea na China mtu akifanya ufisad anafanywaje?anahamishwa kitengo!?au anashushwa cheo af mshahara wake wa nafas yake ya awali unaendelea kuingia as usual!?.Je kiwango chao cha ufisadi kikoje na je, sisi tuna demokrasia kubwa kiasi cha kuchelewesha maendeleo!?na vep katika humuiya ya africa masharik nchi gani yenye demokrasia kama kenya!?je,nchi ipi inaizid kenya hapa EAC!?
 
demokrasia ya kazi gani?, CHINA wamepiga hatua kimaendeleo kwa kufuata misingi ya demokrasia za magharibi?, FIKIRI NJE YA BOX, usikariri,
Kama Haina umuhimu vyama vifutwe sasa, nasio watu watekane na kuuwa wenzao. Tubaki na chama Kimoja tu.
 
mtanzania anakwepa kodi, then analalamika barabara mbovu, huduma za kijamii haziridhishi, HAKUNA HAKI BILA WAJIBU, ushoga huwezi kuona threat now, hii ni mbegu brother inamea taratibu, na inakuja kwa gia hizo hizo za demokrasia,
Kama tunalipia kodi na bado zinatumika kufadhir watekaji na kuzigawa kwa Simba na Yanga, kisha mambo ya muhimu kama majanga unatuambia tuchangie faida yake nini hizo kodi?. Ningeweza kuzikwepa ningekwepa hasa hizi direct tax.
 
Back
Top Bottom