Jaji Warioba kujiuzulu tume ya mabadilko ya katiba

Jaji Warioba kujiuzulu tume ya mabadilko ya katiba

Aiseeeeee hii kitu hata mimi nimesikia watu wanaongea kwenye daladalaaa
 
Huyo mzee naye ameshanichosha tunashukuru kwa kazi waliyoifanya lakini juzi itendo cha kuzungumzia tume isivunjwe badala ya kwenda mbele zaidi kuzungumzia mapungufu mengine yaliopo kwenye sheria ya mabadiliko ya katiba alinishangaza sana.
 
Kuna tetesi kuwa kutokana na kushinikizwa na chama tawala kubadilisha mapendekezo ya rasimu ya katiba, Jaji Warioba yu mbioni kuachia ngazi.

sijui kama hizi tetesi zinaweza kuwa kweli kwani majuzi tu alisema hakuna mjumbe atejiuzulu!
 
Nasikia ameitisha press muda huu jamani mwenye taarifa zaidi atujuze labda anataka kubwaga manyanga kweli..
 
Huyo mzee naye ameshanichosha tunashukuru kwa kazi waliyoifanya lakini juzi itendo cha kuzungumzia tume isivunjwe badala ya kwenda mbele zaidi kuzungumzia mapungufu mengine yaliopo kwenye sheria ya mabadiliko ya katiba alinishangaza sana.

haya majanga, hukumchagua wewe, humlipi wewe. Akuchoshe wewe?
 
serikali 3, kwisha. watz(wazenji na watanganyika watarizika na watatulia, na kazi itaanza kwa ajili ya kujenga nchi zao. na km kuna watu wanahisi watakosa maslah yao, ni vyema wakajiandaa kisaikolojia km walivokua wametahadharishwa.
 
Salaam wana jukwaa,nimekumbwa na msongo wa mawazo,najiuliza itakuwaje mwenyekiti wa tume ya katiba mpya,atakapozidiwa nguvu na wenye chama kizee na kuamua kujiuzuru.Je tutaendelea na katiba nzee?je atachaguliwa mwingine na kuanzisha mchakato upya?msaada tafadhali!
 
Usijiue kwa mawazo. With CCM expect the impossible to happen...just be ready for a shock.
 
Sitapokea kwa furaha kitendo cha warioba kujiuzulu. Natoa WITO asimame imara kwa maana maoni aloyaandika na tume yake ni ya watanzania na sio ya maccm wachache.
Kujiuzulu itakuwa ni kama kuzira na kuwaacha watanzania hatima yao iamuliwe na watu wachache ndani ya ccm ambao hawawakilishi mawazo ya watanzania milioni arobaini.
 
kuna tetesi kuwa kutokana na kushinikizwa na chama tawala kubadilisha mapendekezo ya rasimu ya katiba, jaji warioba yu mbioni kuachia ngazi.

warioba , heshima na utu wako ni bora kuliko hawa akina lukuvi na wasira .
 
Katiba sio ya wabunge waliochaguliwa na watu zaidi ya milion 8,hapa tz ina watu 45m,sikilizeni maoni ya wengi kuepuka lawama na migogoro ambayo haina sababu kwa nchi kama Tz
 
Wananchi, baada ya kuelimishwa vya kutosha na serikali, vyama vya siasa na asasi za kirai kuhusu maana ya kutoa maoni yao kuhusu katiba mpya, tayari wameisha toa maoni yao kuhusu katiba mpya kwa kamati ya Warioba (iliyoteuliwa na Rais ikiwa na uwakilishi balanced na watu makini) kama ilivyo katika rasimu ya kwanza. Kwahiyo rasimu inajadiliwa tena kwa sababu zifuatazo bila kuwepo na shinikizo la chama chochote (watu wake tu waongee):
1. kutoa maoni namna ya kuboresha walichosema wananchi na siyo kamwe kubadili walichosema maana kubadili kutahitaji watu wananchi waridhie kwamba watu wachache wenye akili wameona wananchi walikosea.
2. kuongeza maoni juu ya kilichosahaulika kuwekwa na wananchi au Tume kwekwa katika rasimu ya kwanza, mfano kuhusu mipaka katika maziwa nk.

Haya ndiyo maoni yamgu kama mwananchi wa kawaida.
 
haya majanga, hukumchagua wewe, humlipi wewe. Akuchoshe wewe?

Uhahakika unacho kinena kama kama unayo sawa lakini kodi yako, yangu, yetu ndiyo inayotumika sasa kama tunamlipa tunahaki ya kuhoji kazi ambayo wajua ni kwa aili ya katiba yetu.
 
Makelele ya vyura hayamzuii punda kunywa maji. Mzee warioba hapaswi kusikiliza kelele za watu. Asimamie kazi alopewa.

Mzee simama kama wasomi wa kale walivokuwa.
 
Back
Top Bottom