Jaji Warioba kujiuzulu tume ya mabadilko ya katiba

Jaji Warioba kujiuzulu tume ya mabadilko ya katiba

Kama maccm yanampigia kelele kila kukicha bora ang`atuke tu,maana mpaka wakina nepi wamekosa adabu wanawaombea kifo wazee wa watu ni hatari sana.
 
Unajua CCM wanaandaa katiba ya nchi nzima wanataka mambo yao lazima yaingie wajumbe wa kwenye wilaya wamelishwa sumu yaani kama ccm walijua haya hata umuhimu wa katiba mpya haukuwa wa lazima
 
Kuna tetesi kuwa kutokana na kushinikizwa na chama tawala kubadilisha mapendekezo ya rasimu ya katiba, Jaji Warioba yu mbioni kuachia ngazi.
sisi wachache wenye akili zetu tulijua toka mwanzo kwamba CCM hawakuwa na nia ya dhati ya kutupatia katiba mpya;

Ndani ya CCM kuna kakundi kadogo sana kanakotawala nchi hii, kakundi haka ni hatari sana kwa ustawi / usalama wa taifa letu

Jaji warioba si mtu wa kuburuzwa buruzwa na ndiyo maana aliaminiwa na mwalimu kuwa waziri mkuu wake;

Hongera mzee wetu tunakuomba utupatie katiba mpya ili vizazi vijavyo vikukumbuke, kama wanataka ufuate wanavyotaka YES waachie mchakato wao kaa pembeni ule pensheni yako taratibu.

Lakini kumbuka uko na support kubwa sana ya watanzania, hako kakundi ka watu ambao hata hawafiki 500 hawawezi kuyumbisha mchakato uliyo nyuma ya watanzania milioni zaidi ya 50.

Mungu ibariki Tanzania..na hawa wanaoshinikiza vitu wanavyoona vina manufaa kwao washindwe kabisa;
 
Swali zuri sana. Rasimu imetokana na maoni ya wananchi. Kama vipi tuanze na hili tuone wananchi wanaaamuaje?. Swali liwe hivi: Chagua jibu moja tu, unataka serikali (a) 1 (b) 2 (c) 3?

Jibu ni 'C'
 
suluhisho la watanzania,sisi tunataka serikari-3,hayo mengine ni matakwa ya wajinga wachache,kwa ajili ya maslahi yao na watoto wao.
 
Serikali moja tu.

Kutokana na mazingira ya wakati ule (enzi ya mpito kutoka kupata uhuru, na siasa za ukombozi) serikali mbili zinaweza kuwa zilikuwa "justifiable", lakini kwa mazingira ya sasa(uchumi ndo muhimu zaidi) ukweli ni kwamba (na mara zote kama ilivyo tiba ya mwili ni mchungu sana) serikali moja ndo suluhisho.

Kwa sasa tunazungukwa na uwoga tu!!!! Huwezi kuwa na nchi moja inayotokana na muungano wa nchi mbili halafu eti ukabaki na nchi zote mbili au nchi moja na nusu(mapendekezo ya CCM). Kama tunaona hakuna manufaa kufanya muungano (na maanisha pande zote mbili zijipime) basi na tuuvunjilie mbali huu muungano. Labda kwa kuuvunja sasa tutapata nafasi ya kuunda tena upya katika mazingira ya leo!!! ("I doubt it very much though")

"Route" tunayotaka kuchukua ya serikali 3 au serikali 2(kama CCM inavyotaka kutuaminisha) ni sawa sawa kabisa, narudia ni sawa sawa kabisa na kuuvunja muungano kwa kutumia njia ndefu yenye milima na mabonde mengi pengine yatakayoleta hata machafuko. Kuliko kuenda hiyo njia ndefu na tukapoteza muda mwingi ni bora tuka uvunjilia mbali sasa "before its too late". Maana kinachoendelea sasa ni kama kuviziana

"Serikali moja, nchi moja au vunja muungano"
 
Namshauri Warioba asijiuzuru,asimame imara mpaka mwisho akitetea kile ambacho watanzania wamekipendekeza katika rasimu!Kujiuzuru ni kama kuwapa nafasi ya kuteka zaidi mchakato huo na kutupatia katiba mbovu.Serikali tatu ni maoni ya wananchi wengi sasa hilo la serikali mbili limetoka wapi?Hakuna wa kuzuia kurudi kwa Tanganyika,tumevumilia kwa zaidi ya miaka 50 sasa tukiwa kwenye kivuli cha muungano feki,kwa hiyo kama lengo lilikuwa kwenda kwenye serikali moja ila kwasababu Kuna baadhi ya wendawazimu hawataki sie watanganyika tuendelee kuvumilia upuuzi huo mpaka lini?Tunaitaka Tanganyika yetu full stop
 
kwa sisi tuliosoma arafu hatuna kazi na kazi zenyewe kwa kujuana kama vip hata serekari 10 mm poa tumeshachoka kaulimbiu zisizokua na msingi. kama mzee wanamzingia aache mana ccm sio watu wazuri.
 
Mwenye taaluma yoyote akikimbilia siasa basi ujuwe alishaanguka kitaaluma.
Kweli mkuu maana mzee huyu utamsikia jambo la kisheria ambalo hata asiyeelewa sheria anajua lipo vipi basi mzee huyu atalopoka kama katoka usingizini.
 
hivi uraia wa nchi mbili mnauelewaje? someni ibara ya 5 (56)(2)&(3)
 
Kama atafanya hivyo atakumbukwa daima kuliko kuendelea kufanya mambo ambayo siyo maoni ya wananchi.

Yule mzee dah tutamkumbuka sana anataka kumaliza maisha yake vizuri zaidi ya mzee aliye tangulia mungu ampe afya njema alinifurahisha sana pale alipo mwambia mjumbe aliye taka kusoma waraka wa ccm alipo mwambia kama ni wa ccm kachini wala usijisumbuwe sisi tiari tunao!!
Nadhani nepi aliumia sana hapo!!
Mzee warioba ni mtu msafi sana nahuu ni mda wake wa kuweka usafi wake wazi !!
Hana kashifa za ajabu wala hapendi dhuluma kwa jinsi nilivyo pata kumfaham wala hana ufisadi wa kijinga !!
 
Salam wana jukwaa,

nimekuwa nikifuatilia yanayozungumwa kwenye majukwaa na viongozi wa CCM, mfano jana Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Abdallah Bulembo.

CCM wameteka mjadala wa katiba mpya na kuzungumzia kwenye majukwaa na vyombo vya habari, na hivyo kuathiri wenye mitazamo tofauti

inavyoonekana CCM wanataka serikali mbili kwa gharama zozote kwasababu makundi tayari yalishajipanga kwa uraisi wa muungano.

Kwahiyo CCM itatumia uwepo wake kwenye dola kuhakikisha kura ya maoni inasema serikali mbili.

naona mchakato huu umekosa maana kwa kuingiliwa na wanasiasa hivyo kulinda heshima namshauri Warioba ajiuzulu
 
naendelea kuwa tomaso hadi atakapotmiza, nimechoka kuskia wakitishia nyau.
 
Back
Top Bottom