Wananchi, baada ya kuelimishwa vya kutosha na serikali, vyama vya siasa na asasi za kirai kuhusu maana ya kutoa maoni yao kuhusu katiba mpya, tayari wameisha toa maoni yao kuhusu katiba mpya kwa kamati ya Warioba (iliyoteuliwa na Rais ikiwa na uwakilishi balanced na watu makini) kama ilivyo katika rasimu ya kwanza. Kwahiyo rasimu inajadiliwa tena kwa sababu zifuatazo bila kuwepo na shinikizo la chama chochote (watu wake tu waongee):
1. kutoa maoni namna ya kuboresha walichosema wananchi na siyo kamwe kubadili walichosema maana kubadili kutahitaji watu wananchi waridhie kwamba watu wachache wenye akili wameona wananchi walikosea.
2. kuongeza maoni juu ya kilichosahaulika kuwekwa na wananchi au Tume kwekwa katika rasimu ya kwanza, mfano kuhusu mipaka katika maziwa nk.
Haya ndiyo maoni yamgu kama mwananchi wa kawaida.