Jaji Warioba: Miaka yote watu wanaelewa kujaza fomu, lakini 2020 ghafla hawajui. Siasa inataka kuingia kwenye Dini

Jaji Warioba: Miaka yote watu wanaelewa kujaza fomu, lakini 2020 ghafla hawajui. Siasa inataka kuingia kwenye Dini

Naipendatz

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2011
Posts
5,096
Reaction score
8,234
Jaji Warioba akichangia kwenye mkutano wa TCD leo Dodoma, amenena haya

Miaka yote watu wanaelewa na wanajaza fomu vizuri lakini Mwaka 2020, ghafla watu hawajui kujaza fomu (wanaenguliwa). Hapa lazima kuna namna

Msitazame Wajumbe wa Tume pekee, angalieni Mfumo mzima wa Uchaguzi. Wizi wa kura unaanzia mbali. Unaanzia kwenye Kuandikisha wapiga kura, wakati wa kupiga kura na kutangaza matokeo

Siasa inataka kuingia kwenye dini, zamani viongozi tulikuwa tunakwenda kwenye vyumba vya ibada kama waumini, unasikiliza neno la Mungu. Siku hizi viongozi wakienda wanaombwa kutoa salamu za kisiasa, hii inaweza iingiza siasa katika dini tukapata matatizo

Vyama vingi vimekuwa kama makabila, vinaanza kugawa wananchi. Wananchi walikuwa kama jumuiya lakini siku hizi mambo mengi ya kijamii tunaingiza siasa, mfano msiba ni wa jamii lakini baadhi ya misiba unakuta sare za vyama,"

Katika vyama jumuiya zetu nazo zinakuwa kama za uhasama, badala ya kutuleta pamoja. Hali tuliyo nayo sasa utamaduni umetikiswa kidogo na tunapozungumzia maridhiano, nia yake kuturudisha kwenye utamaduni tuliokuwa nao

Viongozi wa kisiasa wangehubiri amani kama walivyofanya viongozi wa dini miaka michache iliyopita, nchi isingekuwa na malalamiko yanayolalamikiwa hivi sasa “kama wangetenda kama viongozi wa dini, nadhani matatizo haya tunayozungumza tusingekuwa nayo.

warioba.jpg
 
Tulipitia kipindi kigumu Sana najiuliza why uwachukie wapinzani kiasi hicho km ww ni mwana mwema wa nchi
Alikuwa mnafiki na muovu, kwa mtu anayeitakia mema nchi yake na ambaye siyo fisadi Wapinzani na vyombo vya habari huru ni taasisi za kuzikumbatia maana zinakusaidia kufichua maovu, na maovu mengine hata watu unaowaamini wanaweza kukuficha kulinda matumbo yako lakini hayo makundi mawili huwa hayana cha kupoteza
 
Kwa nini hawakuenda mahakamani?
Kubaki unalialia umeonewa wakati hakuna kesi hata moja mahakamani ya kupinga uchaguzi ni upuuzi na kupoteza muda.
Zaidi ya Nusu za kata nchi nzima CCM ilipita bila kupingwa sasa mahakamani unaenda kufungua kesi Gani wakati hata uchaguzi haukufanyika?

NEC watu walipeleka rufaa zilikaa zaidi ya wiki 2 mpaka 3 huku CCM ilishaanza kampeni ghafla unaambiwa rufaa Yako imefeli!!! Then what?? Hiyo kesi mpaka iishe si inabaki wiki moja kwenda uchaguzi!!!

Nmefurahi kusikia Kinana anakiri kuwa Haki na Demokrasia havikuwepo, na ndio mwanzo mzuri kupata chaguzi zenye matakwa ya wananchi Ili kuleta viongozi wenye tija kwenye maendeleo yao
 
Back
Top Bottom