Jakaya Kikwete: Wazee tulikataa kubadili Katiba muhula wa Urais kutoka miaka 5 kuwa miaka 7

Nchi yetu ina viwango, hapa ilipofikia heshma yake kubwa ni kuheshimu vipindi viwili vya miaka mitano, wakianza hawa na miaka 7 huko tunakokwenda siko.
Duh; nchi hii!

Kwamba ili mradi wanazingatia vipindi viwili hata wakiiba mapesa ya umma kama walivyozoea wataendelea kuheshimiwa.
 
Mbona ameongea kimafumbo? Si amtaje Jina la huyo kiongozi alietaka kuongeza miaka 7 kutoka 5
 
Juma nkamia Kuna siku alitamka maneno haya

"Unajua bwana yule alipenda Sana sifa , na mm Kuna mambo hayakwenda vizuri nikaona njia ya kuepuka n kumsifia "

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Huo ndio tunaita ujuha pro max.

Kwamba kwa kuwa tu unataka kupalilia la kwako basi hat ukiona Wenzako wanatobolewa macho wewe unashangilia tu "watoboe Mkuu" ili afurahi na wewe uendelee kula wali na nyama?.
 
Kwa akili zako unafikiri wazee wangekaa kujadili kitu alichoropoka Juma Nkamia kama kulikuwa hakuna tishio la kweli?
Umenielewa kweli mkuu ? Mimi nimeongea kitu tofauti na wewe, nimesema Nkamia aliropoka na hakutumwa na hata yeye alikiri, sijasema huo mpango haukuwepo, yeye aliusikia na kuruka nao tu ila hakutumwa
 
Akiwa kwenye mahojiano na kipindi maalum cha Clouds leo aliyekuwa Rais wa awamu ya Nne Jakaya Kikwete amesema kuwa mchakato uliokuwa mgumu zaidi kwake ni kuzuia uhuni wa kubadili muhula wa uongozi ndani ya CCM kutoka miaka mitano kuwa saba.

Jakaya anasema mjadala ulipoletwa ulikuwa ni moto ila tayarI CCM kulikuwa na utaratibu wa miaka mitano na uamuzi huo uheshimiwe.

======

KUONGEZA MIAKA YA URAIS
Kikwete:
Kuna kipindi walianza sana mjadala wa kubadili katiba sijui iwe miaka 7, pale wazee tulishauriana tukasema hapana, huku wanapotaka kutupeleka hawa sipo.

Nchi yetu ina viwango, hapa ilipofikia heshma yake kubwa ni kuheshimu vipindi viwili vya miaka mitano, wakianza hawa na miaka 7 huko tunakokwenda siko.

Nakumbuka tulikutana wazee na siku hizi hamna haja kukutana hata kwa simu mnaunganisha, tukakubaliana hawa lazima tuwaambie vijana hawa.

Magufuli ameondoka ametuachia roho ya uchawa. Sifia tu ili upate cheo.
 
Waliotaka miaka 7 ni akina nani ?
 
Back
Top Bottom