Jakaya Kikwete: Wazee tulikataa kubadili Katiba muhula wa Urais kutoka miaka 5 kuwa miaka 7

Jakaya Kikwete: Wazee tulikataa kubadili Katiba muhula wa Urais kutoka miaka 5 kuwa miaka 7

Katiba gani, mbona kila baada ya miaka kumi rais akiwa ametoka bara zamu inayofuata ni visiwani wakati haimo kwenye katiba? Mbona rais akiwa mkristo akimaliza muda wake anayefuata anauwa na jina la kiislamu?

Hakuna katiba yoyote waliyolinda sababu ni kwamba miaka ingekuwa mingi sana ya wao kutopata fursa ya kutafuna rasilimali za nchi bila kuhojiwa na mtu mwenye ujasiri
Mkapa,kikwete,magu...nani mzanzibar hapo!?
 
Akiwa kwenye mahojiano na kipindi maalum cha Clouds leo aliyekuwa Rais wa awamu ya Nne Jakaya Kikwete amesema kuwa mchakato uliokuwa mgumu zaidi kwake ni kuzuia uhuni wa kubadili muhula wa uongozi ndani ya CCM kutoka miaka mitano kuwa saba.

Jakaya anasema mjadala ulipoletwa ulikuwa ni moto ila tayarI CCM kulikuwa na utaratibu wa miaka mitano na uamuzi huo uheshimiwe.

======

KUONGEZA MIAKA YA URAIS
Kikwete:
Kuna kipindi walianza sana mjadala wa kubadili katiba sijui iwe miaka 7, pale wazee tulishauriana tukasema hapana, huku wanapotaka kutupeleka hawa sipo.

Nchi yetu ina viwango, hapa ilipofikia heshma yake kubwa ni kuheshimu vipindi viwili vya miaka mitano, wakianza hawa na miaka 7 huko tunakokwenda siko.

Nakumbuka tulikutana wazee na siku hizi hamna haja kukutana hata kwa simu mnaunganisha, tukakubaliana hawa lazima tuwaambie vijana hawa.

Wazee wengine ni Aibu ya Taifa.
 
Hapo inatafutwa mbinu ya kuhalalisha wizi unaondelea sasa.

Hakuna jambo litafanyika kuhalalisha matumizi mabaya ya Rasilimali za Watanzania.
Hivi huo wizi uko wapi, au lini ulikua haupo?

hebu tuanze na wewe, unafanya shughuli gani hivi sasa?
 
Huyu nae muhuni tu kama wahuni wengine...rasimu aliipiga teke imetufikisha wapi? Kuwa madarakani hata miaka mia sio hoja, hoja ni nini umetufanyia...full stop. Kagame mwaka wa ngapi leo? Mbowe, Museven? Bibi yenu alikaa 70years so hoja sio kukaa madarakani hoja ni maendeleo ya watu na vitu kwa ujumla wake umesimamiaje? Njia za kukuza uchumi unazopita ni zipi?, sera za kuchochea maendeleo zinapishwaje na kusimamiwaje? Ukiwa mbovu kama bi tozo na JKY hata mwaka mmoja tu hutufahi.
Sawa, sasa kama alifanya mambo mazuri ya maendeleo yanayukubaliwa na Wananchi, alikuwa na hofu gani hata akafikiri kujiongezea muda na kuwanyamizisha vyama siasa kwa mtutu.

Na hata uchaguzi ulipofika alitumia nguvu nyingi kununua wapinzani, kutisha watu kufunga watu na wengine kupigwa risasi.
 
Huyu nae muhuni tu kama wahuni wengine...rasimu aliipiga teke imetufikisha wapi? Kuwa madarakani hata miaka mia sio hoja, hoja ni nini umetufanyia...full stop. Kagame mwaka wa ngapi leo? Mbowe, Museven? Bibi yenu alikaa 70years so hoja sio kukaa madarakani hoja ni maendeleo ya watu na vitu kwa ujumla wake umesimamiaje? Njia za kukuza uchumi unazopita ni zipi?, sera za kuchochea maendeleo zinapishwaje na kusimamiwaje? Ukiwa mbovu kama bi tozo na JKY hata mwaka mmoja tu hutufahi.
Na ile iliyojadiliwa kwa kuundwa bunge maalum la katiba ilikuwa ni nini kama siyo hiyo rasimu unayosema aliipiga teke?
 
Kwa tamko hili ni bayana sasa ni kweli ana mkono kwenye serikali hii na kwamba walimzima mwamba kwa kujifanya wao ni wamiliki nchi..............................days are chronologically numbered when time materializes, he will denounce his statement
Inashangaza sana...Daah public confession, duuh Mungu fundi!
 
Kwa tamko hili ni bayana sasa ni kweli ana mkono kwenye serikali hii na kwamba walimzima mwamba kwa kujifanya wao ni wamiliki nchi..............................days are chronologically numbered when time materializes, he will denounce his statement
Kwa tangazo lipi?

Sasa wewe ulikuwa huelewi kama Kikwete yupo kwenye jopo la wazee wanaofanya maamuzi mazito ya CCM, inapobidi?

Wengine huwa mnaandika utumbo tu.
 
Kwa tangazo lipi?

Sasa wewe ulikuwa huelewi kama Kikwete yupo kwenye jipo la wazee wanaofanya maamuzi mazitonya CCM inapobidi?

Wengine huwa mnaandika utumbo tu.
Endelea ku bold madam, si yetu macho na masikio...
 
Endelea ku bold madam, si yetu macho na masikio...
"Ku bold" ndiyo mdudu gani? Sikuelewi.

Ulifikiri hayo "macho na nasikio" ni yenu tu? Watu wengine hamueleweki kabisa.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Alitumia nguvu za kishetani akimtumaini shetani kama kinga mwokozi wake infact ali bi partisan his soul half to Satan and half to Almighty as public mirror! (complex issue)
 
Back
Top Bottom